U-SPIKA: Sitta, Chenge wapigwa panga CCM!

Kati ya hawa ANNA ABDALLAH, ANNA MAKINDA NA KATE KAMBA sioni hata mmoja mwenye ubavu wa kuzuia matakwa ya MAFISADI yasitimizwe, ama kusimama kidete kama alivyosimama SITTA kupambana na ufisadi. Sitta alikabiliana na chuki, visa, vitisho na hata maisha yake kuwa hatarini sababu ya kuruhusu hoja binafsi na mjadala uliotoboa siri za mafisadi.

HONGERA SITTA KAZI YAKO NZURI ULIYOWAFANYIA WATANZANIA ITAKUMBUKWA DAIMA!!! sisiem na mafisadi hawakupendi sababu hukufanya kwaajili ya maslahi yao bali kwa ajili ya maslahi Watz, ndo maana wamekuangusha.

NASEMA HONGERA TENA KWA KUWEKA UTANZANIA MBELE NA SIYO USISIEM!!!

WATANZANIA NA MUNGU WAO WATASHINDA. MAFISADI WATASHINDWA NA KUAIBIKA TU !!!
 
Kamati kuu imepitisha majina matatu kugombea uspika -- Anna Makinda, Anna Abdallah, Kate Kamba. Source: Channel Ten 7pm news bulletin

Kazi ya Chenge kumuharibia Sitta imefanikiwa!

Leo Rostam Aziz, Edward Lowassa, Nazir Karamagi na Andrew Chenge hawalali kwa furaha!

Kigumu Chama Cha Mapinduzi!

Mkuu usicheze na hawa jamaa, watalala kwa furaha kabisa kwani yule mwanamke waliyetaka apite si amepita. Sasa kazi yao kubwa ni kuhakikisha huyo mwanamke aliye kwenye payroll yao ndiye anapita na kuchukua hicho kiti cha uspika then atakuwa anaendeshwa kwa remote control.

Tiba
 
Kweli ccm hawajali wanapoamua jambo hawangali cost kabsa Ofisi ya yenye hadhi ya uspika jimboni kwa sita itakuwaje?
 
Mtetezi wa waatanzania ndo anaeonekana mpumbavu! Kwa hili la sita wana ccm wajiulize na wajue kuwa Dr Slaa halopoki bali anaongea kwa uchungu kwa maslahi ya nchi yetu.
 
ANNA MAKINDA alikuwa kwenye mtandao maslai wa KIKWETE sasa atazuia vipi mafisadi akiwa waziri wa wizara ya maendeleo ya jamii jinsia na watoto aliwahi kuchukua fedha zilizotolewa na UNICEF kuhamasisha akina mama vijijini kuchanja watoto yeye akanunua mabati ciment za kwenda kuhonga wapiga kura wake akaondolewa kwa ajili ya kashifa hizo ni FISADI nzuri sana huyo,Anna Abdalah amefisadi hata hiyo nafasi ya viiti maalumu ameingia kwa kupitia NGO sijui ipi
 
Wakuu mambo yameanza hatimaye kamanda Sita katupwa rasmi. Chanzo taarifa ya habari saa mbili usiku
 
Kamati Kuu ya CCM imependekezea majina yafuatayo kugombea Uspika:

1. Anna Makinda
2. Anna Abdallah
3. Kate Kamba

Kwa hivyo Mzee wa Vijisenti out, Sitta out!!!

Source: Channel 10 News Bulletin 3 minutes ago.


Unajua sio kama Mzee wa Vijisenti (Chenge) alikuwa kaupania "Uspika" ki-hivyo No!.Lakini hizi zote zilikuwa ni tactics za kulchafua hali ya hewa ili mwisho wa siku Kamati Kuu iweze kuwaengua wote wawili yaani Sitta na Chenge kwa kisingizio cha kuwa eti imeamua "Imevunja makundi".
Binafsi nilishaliona hilo kitambo kwamba Sitta na Upika ndio byebye na yeye alivyokuwa ndumi la kuwili akazima mijadala mizito ya Kiwira, Richmond, EPA na mingineyo na hata ule wa Wabunge kutokuwa na imani na serikali tena kwa umwamba kabisa na kulivinja Bunge haraka haraka aki-bank kuwa walau CC itakuja 'kumkubuka' 2nd term lakini alikuwa very wrong. Sitta alikuwa mis calculate sana timing yake hususan baada yeye kuingia kwenye hatihati za kutaka kutimuliwa CCM mara karibu mbili.

Binafsi alinikera mno na nilitegemea sana mafisadi wangemwangamizia jimboni kwake kwanza na nilimwambia jamaa yangu mmoja tuliyekuwa tuna-debate issue ya Sitta kuwa hata akiponya ponya na kuingia Bungeni basi Sitta 'hatokuwa' Spika tena. Lakini angesimamia haki na kuachia ile mijadala mizito mpaka mwisho (hata kama wabunge wangepiga kura ya kuindoa serika ya kifisadi madarakani) na hata kama gharama yake ingekuwa kutimuliwa CCM akiwa bado Spika, leo Sitta angalikuwa 'lulu' na Shujaa wa Wa-Tanzania.
 
dah CHADEMA muuzeni MARANDO sasa ccm washachemshaaa
Sisi tulie tu, Marando atapenye wapi wakati wabunge wa CCM wanapiga kura kama chama. Wabunge wengi wa CCM hawako bungeni kwa interest za nchi bali za Chama. Kwanza wale wa viti maalum tu waliotangazwa jana wako 65 na CHEDAMA wabunge wote ni 45 tu.
 
Nasikia Dodoma ni shangwe na vifijo. Sasa kama walitaka wanawake tu kwanini waliruhusu wanaume kuapply tena eti laki tani kila mmoja duh, watu mnajua kutuibia. Mh JK this is too low
 
Kati ya hawa ANNA ABDALLAH, ANNA MAKINDA NA KATE KAMBA sioni hata mmoja mwenye ubavu wa kuzuia matakwa ya MAFISADI yasitimizwe, ama kusimama kidete kama alivyosimama SITTA kupambana na ufisadi. Sitta alikabiliana na chuki, visa, vitisho na hata maisha yake kuwa hatarini sababu ya kuruhusu hoja binafsi na mjadala uliotoboa siri za mafisadi.

HONGERA SITTA KAZI YAKO NZURI ULIYOWAFANYIA WATANZANIA ITAKUMBUKWA DAIMA!!! sisiem na mafisadi hawakupendi sababu hukufanya kwaajili ya maslahi yao bali kwa ajili ya maslahi Watz, ndo maana wamekuangusha.

NASEMA HONGERA TENA KWA KUWEKA UTANZANIA MBELE NA SIYO USISIEM!!!

WATANZANIA NA MUNGU WAO WATASHINDA. MAFISADI WATASHINDWA NA KUAIBIKA TU !!!

Yaani kwa mibange hii sijui!!!!Bora Sitta angeweza, hawa kinamama mtawaua kwa presha. Sisemi kinamama hawawezi lakini suala ni kinamama gani wanaweza nini!!

Kama Chenge & the Co waliona wanataka mtu wa kuwaminyia mbali wabunge moto moto basi hili sio chaguo sahihi, na kama ni mwanamke wa kuwasaidia kwa hilo wangemchukua Hawa Ngulume au Sofia Simba......Hapo moto ungezimwa kisawasawa mpaka bunge lilipuke puf!!!

Hawa kinamama waliopitishwa sioni 'Time Value of political wisdom' iliyozingatiwa hapa.

Yaani huku Anna nani sijui...huku Shibuda, Tundu Lissu, Zito, Halima, Mbowe, Mnyika, Sugu, mwakyembe, H. Rashid, Nyerere, Ndesamburo, Mrema, Cheyo ..enh!!!! Andaeni fungu la matibabu ya presha mara kwa mara kwenye bajeti yenu.
 
Mageuzooooooooooooooo hoyeee!! Kwangu mimi awe ni yeyote katika hao as long as MWIZI CHENGE IS OUT AM SO HAPPY. Now we are talking.
 
Hii imedhihirisha mambo mawili kwanza uwezo wa Kikwete kuwa kionmgozi wa nchi ni mdogo sana hakufaa kuwa rais sura ndiyo iliyomsaidia kufika hapo na si uwezo alistahili kuwa waziri wa michezo na utamaduni ni jambo la kushangaza kwake yeye kushindwa kusoma dalili za nyakati na kufuata matakwa ya mafisadi, pili maneno ya Mwalimu Nyerere yametimia mwalimu aliwahi kusema Rais anapowekwa madarakani na kundi la watu wachache hatawatumikia wananchi isipokuwa atawatumikia waliomuweka madarakani Kikwete anawatumikia Edward Lowassa, Rostam Aziz, Nazir Karamagi, Sophia Simba, Andrew Chenge, Yussuf Makamba, Lawrence Masha, Msabaha, Bernard Membe na wengine wengi wanamtandao waliomuweka madarakani badala ya kutumikia taifa.

Ila kuna kitu Kikwete anasahau kuwa Samuel Sitta ndiye aliyekuwa anamsaidia kisheria na kutengeneza kauli mbiu pia kuwaelimisha wazee wa chama kuwa Kikwete anafaa maana watu wengi walimuona ni mhuni na hafai kuwa rais ahata kidogo kwa maneno mengine pasipo yeye pesa za Rostam na Lowassa zisingempleka ikulu.

Kitu kimoja Kikwete na kundi lake waelewe kuwa kwa mafyongo ya kuondoa jina la Sitta kufurahisha mafisadi nchi sasa iko wazi kwa vyama vya upinzani 2015 kwa sababu wananchi wameishajua hila zote za CCM kuwa haiwatakii watanzania maisha mema isipikuwa wao CCM wameigeuza Tanzania kuwa sehemu ya miradi ya familia zao
 
wakuu!

inavoonekana ni mama Makinda ndie mamlaka za juu zinamtaka,nasoma hapa kwenye gazeti la leo kwamba kalipiwa deni lake la bilioni 1 la kampuni yake,KWELI TUNA SPIKA HAPA??????
 
Back
Top Bottom