TWAWEZA, acheni kutufanya sisi watanzania ni wajinga

We ndo uache kujifanya mjinga. Tafiti hazipingwi kwa maneno bali kwa tafiti nyingine zilizokidhi matwa ya kisayansi. Hivi hujui kwamba tafiti zote zinazofanyika nchini lazima zipewe kibali kutoka NBS kwamba zimekidhi matakwa yote ya kitafiti? Hebu acha kujenga hoja bila ufahamu wowote.
Kwa maelezo haya nina Hakika Asilimia 100 wewe uelewi chochote kuhusu tafiti na ukiona mtu yoyote anatoa Hoja kama yako ujue haelewi kitu kuhusu tafiti
 
Kwa kweli imefikia mahali hamvumiliki tena, tafiti zenu uchwara zinaonekana kabisa kuwa mnatumika sana kisiasa. Kama nyie ni watafiti kweli, tuambieni hivi ni kwanini magazeti private yanauzika sana kuliko magazeti ya Serikali?
Kama nyie ni watafiti kweli, tuambieni kwanini tuna miaka 55 ya uhuru lakini nchi bado inanuka umaskini wa kupindukia.

Kama nyie ni watafiti kweli, tuambieni kwanini Serikali inaficha aibu kwa kuyapatia ruzuku magazeti yake ili yaendelee kuonekana mitaani maana hayauziki. Kama nyie ni watafiti tuambieni kwanini Serikali imekiuka katiba kwa kupiga marufuku mikutano yote ya kisiasa kwa kisingizio cha maendeleo, tangu lini maendeleo yakazuiwa na mikutano.

TWAWEZA acheni unafiki, bahati nzuri ni kwamba ukweli haujawahi na kushindwa wala hauna historia ya kushindwa. Nyie kila kitu mnasifia tu hata kwenye hamna, halafu mnakuja hadharani na kusema eti ni watanzania wamesema, tulisema wapi. Tanzania siyo kijiji, ni nchi kubwa ki eneo kuliko hata Nigeria, nyie mnakusanya CCM na kisha mnawauliza wakisema ndiyo, mnaibuka na kudai eti ni Tanzania nzima. Acheni kabisa kutudhalilisha nyie watu, mnachefua sana na hako ka taasisi yenu.
Ona huyu naye anatoa pofu utafikiri tafiti zinahoji watu wote au unataka wakuhoji wewe? Kama unataka maoni ya kukufurahisha fanya utafiti wako mwenyewe. Halafu kwa upuuzi wako unafikiri neno watanzania lina maana ya CDM. Maana ni CDM tu angalau ndo wamebaki na ujinga wa kupinga kila kitu ili ati waonekane ni wapinzani wa kweli.
 
Hapana mkuu. Nawafahamu kwa ukaribu kwani nilifanyaga nao kazi. Ni taasisi yenye ueledi kabisa.
Sasa weledi wameweka pembeni wamebakiwa na weledi wa kujipendekeza kwa watawala.
 
Kama hauziamini tafiti zao Fanya yako tuone. Slafu uturetee majibu sio kuponda tuu bila sababu za msingi

#Ni mtazamo tuu
 
Utafiti wa twaweza ni furusa kwa serekali kuruhusu maandamano ya ukuta,kwa mujibu wa shirika lisilo la kiserekali la twaweza ni kuwa wananchi wengi wa Tanzania hawajui maana YA ukuta,kwa maoni ya baadhi ya wananchi wamesema ni muda wa serekali yetu kurusu maandamano ya ukuta kwa kuwa,maandamano ya ukuta yatakuwa hayana watu
 
Unafikiri wao ni wajinga waruhusu maandamano? kwani unadhani mapinduzi ya nchi yanahitaji wananchi milion waandamane? hata watu 10000 tu wakiingia barabarani serikali inaweza kuanguka.
 
Tena uzuri ni kuwa sendeka a mesifu sana huu utafiti,amesema watu hawajui ukuta kwa hiyo wasiangaike tena kurusha ndege waruhusu tu maandano wasiogope
 
nmeipenda hiyo, na wala hayana madhara yoyote kwa chama tawala, hayatabadil upepo wa kisiasa kwa kuwa wa2 hawajui ukuta
 
Kufanyia utafiti humu kutakuwa na bias. Washiriki wengi wana access ya smartphones na internet ya kueleweka na kwa kiwango kikubwa ni wale wa mijini na kuacha sehemu kubwa ya wale walio nje ya miji. Bila kusahau jf kuna diaspora kibao wanaotumia jukwaa hili kupata dondoo za motherland. Tunarudi na sample selection problem. Twaweza kisanyansi wamekidhi matakwa yote. Tatizo ni kwamba matokeo yake ni kinyume na maono yetu.
Kwa hiyo utafiti wenu mnaufanya kwa watu wasiokuwa na uelewa wa kutosha kadri ya maelezo yako! Ninavyojua humu JF kuna aina ya makundi yote, na si JF pekee bali hata kwenye FB na hata kwenye website yenu, kwa kufanya hivyo mngekuwa mnafikia jamii zote za Watanzania tofauti na njia hii ya kupiga simu. Kwa kawaida mtu usiyemfahamu huwezi ukampa taarifa yeyoye kwa njia ya simu, mfano ukimpigia simu mtu lazima ajiulize kwanini? Nikijibu hivi sintaweza kuingia hukumuni? Mwisho wa siku mnabaki kukusanya utafiki kwa wananchi wanaoogopa nini kitatokea.
 
Kuna mdau nilitoka kumjibu hivi punde tu kuhusu hili suala. Wadau walio wengi ndani ya JF ni wa mijini na kwa kiasi kikubwa wale wenye computer na access ya internet au smartphone na bundle za internet. Vilevile watanzania walio diaspora ni wengi pia. Kama unaishi mjini, kama mimi ni rahisi sana kugeneralise vitu au kushindwa kuona hali halisi kwa jicho la tatu. Huwa nazungumza sana na kutolea mfano kwamba hii hali ngumu ya maisha tunayoiona inalalamikiwa mijini kwa kiasi kikubwa kwani huko vijijini hali ni ile ile. Hakuna tofauti sana. Alafu tunasahau pia kwamba asilimia 75 ya watanzania wako vijijini. Wa mijini ni asilimia ndogo sanaaaa. Statistically, representation ya wa vijijini ni kubwa kuliko ya wa mijini. Hivyo basi, tujaribu kukosoa utafiti kwa mapungufu yake ya kimuundo au methodology au sample size na selection, nk lakini si kwa hisia kwamba mbona jf members wote hawaungi mkono matokeo.

Pia umesahau huku JF WAMEJAA MEMBER WA CDM ,
 
Twawezi wanafanya utafiti upoteze maana,Kama tafiti zikoiv bora tufanye mambo bila tafiti!! Wastage of ETM (Efforts,Time and Money) waje tuwape shamba!! Washamba...
 
Back
Top Bottom