TWAWEZA, acheni kutufanya sisi watanzania ni wajinga

Kwa kweli imefikia mahali hamvumiliki tena, tafiti zenu uchwara zinaonekana kabisa kuwa mnatumika sana kisiasa. Kama nyie ni watafiti kweli, tuambieni hivi ni kwanini magazeti private yanauzika sana kuliko magazeti ya Serikali?
Kama nyie ni watafiti kweli, tuambieni kwanini tuna miaka 55 ya uhuru lakini nchi bado inanuka umaskini wa kupindukia.

Kama nyie ni watafiti kweli, tuambieni kwanini Serikali inaficha aibu kwa kuyapatia ruzuku magazeti yake ili yaendelee kuonekana mitaani maana hayauziki. Kama nyie ni watafiti tuambieni kwanini Serikali imekiuka katiba kwa kupiga marufuku mikutano yote ya kisiasa kwa kisingizio cha maendeleo, tangu lini maendeleo yakazuiwa na mikutano.

TWAWEZA acheni unafiki, bahati nzuri ni kwamba ukweli haujawahi na kushindwa wala hauna historia ya kushindwa. Nyie kila kitu mnasifia tu hata kwenye hamna, halafu mnakuja hadharani na kusema eti ni watanzania wamesema, tulisema wapi. Tanzania siyo kijiji, ni nchi kubwa ki eneo kuliko hata Nigeria, nyie mnakusanya CCM na kisha mnawauliza wakisema ndiyo, mnaibuka na kudai eti ni Tanzania nzima. Acheni kabisa kutudhalilisha nyie watu, mnachefua sana na hako ka taasisi yenu.

Wewe naye ni mjinga kuliko TWAWEZA NANI KAKUTUMA KUTUSEMEA ? UNATAKA WASEME LOWASA NDIYE RAIS WAKATI UNAJUA SIYO KWELI ACHA ULIMBUKENI TAARIFA YA TWAWEZA NI YA WATU WALIOSOMA NA HAWABAHATISHI MLIMBIWA MAGUFULI ATASHINDA URAIS MKAKATAA NA KUSEMA TWAWEZA WAMENUNULIWA SWALI MPAKA UNAANDIKA UPUUZI WAKO HAPA NANI YUKO IKULU? ANGALIA BACK GROUND YA TWAWEZA KWA KILA TAFITI WANAZOFANYA WAKITOA KITU NI CHA UHAKIKA NA SIYO KWENYE SIASA TU REJEA TAFITI ZAO KUHUSU ELIMU UTAJIONA WEWE NI KIHIYO KULIKO WOTE DUNIANI UNATAKA TAARIFA ZA KUKUFURAHISHA WEWE NA WAJINGA WENZAKO TEMBE UNAITA GHOROFA POLE SANA.
 
Na wewe hujanielewa tafiti sometimes huweza kupingwa bila tafiti... Kama umesoma na kufanya reseach ... Kwa kuipitia research methodology na research data collection ya utafiti unaweza kujua credibility ya utafiti flani kuwa ni pumba ama si pumba... Kwa mfano telephonic method kama njia ya kukusanya data INA kasoro lukuki hususan kipindi hiki cha sheria ya makosa ya mtandao.... Unadhan nani anaweza kupigiwa simu na akaongea kasoro za serikali kwenye simu.... Hiyo ni kasoro moja tu...
Hiyo ni kasoro kubwa mno... UNAANZAJE KWANZA?
 
Paletu mlipomkaribisha ma Mvi mlipoteza heshima yenu. Kwasasa Watanzania wanachapa kazi nyie endeleeni kubwabwaja, Tukutane 2020.
 
Hahahaha. Unanifurahisha ndugu yangu. Jaribu kuwa open minded. Twaweza ni taasisi isiyo ya kisiasa, hela zake kwa kiwango kikubwa inapata kutoka Shirika la Hivos la Uholanzi. Hawana sababu yoyote ya kujikomba kwa serikali kwani kazi zao za uchambuzi zinakosoa sana utendaji na ubora wa elimu nchini.

Mkuu na wewe uko Twaweza nini? Kwa taarifa yako wenye maamuzi nchi hii ni wanasiasa hasa wa chama twawala. Huko kwenye elimu hakuna madhara kwao hivyo hata matokeoa yakiwa ya kukosoa sana upande wa elimu hawajali. Ila kama hawajipendi basi watoe takwimu zitakaonyesha mzee wa hapahapa na chama chake hawaungwi mkono kwa kiasi kikubwa, hapo hakuna cha waholanzi wala waasisi kwamba ndio wafadhili.
 
Wewe naye ni mjinga kuliko TWAWEZA NANI KAKUTUMA KUTUSEMEA ? UNATAKA WASEME LOWASA NDIYE RAIS WAKATI UNAJUA SIYO KWELI ACHA ULIMBUKENI TAARIFA YA TWAWEZA NI YA WATU WALIOSOMA NA HAWABAHATISHI MLIMBIWA MAGUFULI ATASHINDA URAIS MKAKATAA NA KUSEMA TWAWEZA WAMENUNULIWA SWALI MPAKA UNAANDIKA UPUUZI WAKO HAPA NANI YUKO IKULU? ANGALIA BACK GROUND YA TWAWEZA KWA KILA TAFITI WANAZOFANYA WAKITOA KITU NI CHA UHAKIKA NA SIYO KWENYE SIASA TU REJEA TAFITI ZAO KUHUSU ELIMU UTAJIONA WEWE NI KIHIYO KULIKO WOTE DUNIANI UNATAKA TAARIFA ZA KUKUFURAHISHA WEWE NA WAJINGA WENZAKO TEMBE UNAITA GHOROFA POLE SANA.

Hivi kufanya utafiti kwamba mgombea wa ccm atashinda ni utafiti? Ulitegemea matokeo gani iwapo tume ya uchaguzi inachaguliwa na ccm? Ok ngoja tukubali mnachosema, mbona huku kwenye mitandao ya kijamii iliyo huru hatuoni wangalau nusu ya wanaofagilia kama hiyo tafiti ya Twaweza? Uza huo ubongo ndugu yangu unaishi nao kwa hasara.
 
sasa we mkuu huoni hata huu uzi unakusanya majibu ya tafiti za kweli ambazo haziendani na tafit za TWAWEZA? wangapi wameenda kinyume na mtoa mada?

Good point ila kuna vigezo vya kisanyasi inabidi viwe vimekidhi kuweza kuja na matokeo yanayokubalika. Hapa watu wanatoa maoni yao. Hii inaweza kuwa moja wapo ya njia ya kukusanyia taarifa ila sio pekee.
 
Hebu jaribuni kufanya hata utafiti humu JF mlinganishe na hizo za kupiga simu

Kufanyia utafiti humu kutakuwa na bias. Washiriki wengi wana access ya smartphones na internet ya kueleweka na kwa kiwango kikubwa ni wale wa mijini na kuacha sehemu kubwa ya wale walio nje ya miji. Bila kusahau jf kuna diaspora kibao wanaotumia jukwaa hili kupata dondoo za motherland. Tunarudi na sample selection problem. Twaweza kisanyansi wamekidhi matakwa yote. Tatizo ni kwamba matokeo yake ni kinyume na maono yetu.
 
Hivi kufanya utafiti kwamba mgombea wa ccm atashinda ni utafiti? Ulitegemea matokeo gani iwapo tume ya uchaguzi inachaguliwa na ccm? Ok ngoja tukubali mnachosema, mbona huku kwenye mitandao ya kijamii iliyo huru hatuoni wangalau nusu ya wanaofagilia kama hiyo tafiti ya Twaweza? Uza huo ubongo ndugu yangu unaishi nao kwa hasara.
KWENYE CHAMA UMEONA JE KWENYE ELIMU MBONA HUSEMI NA NI TWAWEZA HAOHAO WALIFANYA UTAFITI???? NAOMBA NIKUUZIE UBONGO WANGU
 
Simple mathematics haikuitaji hata uwe una cheti chochote angalia hata hapa jamii forum ufanye research yako mwenyewe uangalie je ni wangapi wanakubaliana na ww...... I swear tangu mwanzo nafuatilia uko mwenyewe unaeunga mkono...

Kuna mdau nilitoka kumjibu hivi punde tu kuhusu hili suala. Wadau walio wengi ndani ya JF ni wa mijini na kwa kiasi kikubwa wale wenye computer na access ya internet au smartphone na bundle za internet. Vilevile watanzania walio diaspora ni wengi pia. Kama unaishi mjini, kama mimi ni rahisi sana kugeneralise vitu au kushindwa kuona hali halisi kwa jicho la tatu. Huwa nazungumza sana na kutolea mfano kwamba hii hali ngumu ya maisha tunayoiona inalalamikiwa mijini kwa kiasi kikubwa kwani huko vijijini hali ni ile ile. Hakuna tofauti sana. Alafu tunasahau pia kwamba asilimia 75 ya watanzania wako vijijini. Wa mijini ni asilimia ndogo sanaaaa. Statistically, representation ya wa vijijini ni kubwa kuliko ya wa mijini. Hivyo basi, tujaribu kukosoa utafiti kwa mapungufu yake ya kimuundo au methodology au sample size na selection, nk lakini si kwa hisia kwamba mbona jf members wote hawaungi mkono matokeo.
 
Mkuu na wewe uko Twaweza nini? Kwa taarifa yako wenye maamuzi nchi hii ni wanasiasa hasa wa chama twawala. Huko kwenye elimu hakuna madhara kwao hivyo hata matokeoa yakiwa ya kukosoa sana upande wa elimu hawajali. Ila kama hawajipendi basi watoe takwimu zitakaonyesha mzee wa hapahapa na chama chake hawaungwi mkono kwa kiasi kikubwa, hapo hakuna cha waholanzi wala waasisi kwamba ndio wafadhili.

Hapana mkuu. Nawafahamu kwa ukaribu kwani nilifanyaga nao kazi. Ni taasisi yenye ueledi kabisa.
 
Back
Top Bottom