Ciprofloxacin.
JF-Expert Member
- Apr 15, 2015
- 1,583
- 2,696
Kwa kweli imefikia mahali hamvumiliki tena, tafiti zenu uchwara zinaonekana kabisa kuwa mnatumika sana kisiasa. Kama nyie ni watafiti kweli, tuambieni hivi ni kwanini magazeti private yanauzika sana kuliko magazeti ya Serikali?
Kama nyie ni watafiti kweli, tuambieni kwanini tuna miaka 55 ya uhuru lakini nchi bado inanuka umaskini wa kupindukia.
Kama nyie ni watafiti kweli, tuambieni kwanini Serikali inaficha aibu kwa kuyapatia ruzuku magazeti yake ili yaendelee kuonekana mitaani maana hayauziki. Kama nyie ni watafiti tuambieni kwanini Serikali imekiuka katiba kwa kupiga marufuku mikutano yote ya kisiasa kwa kisingizio cha maendeleo, tangu lini maendeleo yakazuiwa na mikutano.
TWAWEZA acheni unafiki, bahati nzuri ni kwamba ukweli haujawahi na kushindwa wala hauna historia ya kushindwa. Nyie kila kitu mnasifia tu hata kwenye hamna, halafu mnakuja hadharani na kusema eti ni watanzania wamesema, tulisema wapi. Tanzania siyo kijiji, ni nchi kubwa ki eneo kuliko hata Nigeria, nyie mnakusanya CCM na kisha mnawauliza wakisema ndiyo, mnaibuka na kudai eti ni Tanzania nzima. Acheni kabisa kutudhalilisha nyie watu, mnachefua sana na hako ka taasisi yenu.