Tuzo ya Mpoki

Hivi na akili zako, unaamini kabisa kwenye kupiga kura? Mimi nadhani hata kama alipata kura nyingi kiasi gani, wenye akili timamu wasingempa tuzo! Maneno kama "nyoka hana kiuno ndio maana havai shanga", wewe na akili zako ungempigia kura??? CRAP CRAP CRAP!!


MZIKI NI KUELIMISHA NA KUBURUDISHA, HIVO MPOKI KASTAHILI TUNZO HIYO KWA KUBURUDISHA NA KURA ALIZOPATA.. Tusipinge bila kufikiri.
 
Kwanza mie nilijiuliza kama kweli wimbo wake ulionekana unafaa kuingizwa kwenye categories za mashindano, basi hiyo category aliyowekwa haikuwa stahiki kwa wimbo wake, bora hata wangemweka kwenye category ya "single ya msanii mwenye vipaji mbali mbali" ambayo haipo ila ingeundwa ili achomekwe. Humo angeenda kushindanishwa na akina Kingwendu, Bambo, Masanja na wengineo...ongezea kwenye list
 
anayelalamika mwenye hata kura moja hajapiga!!

watanzania bana!!
 
Kama hamkumpigia kura Mjomba mlitaka apiteje sasa.Wabongo bwana mabahili afu tunaishia kulalamika wakati hatukufanya jitihada za kufanikisha chaguo letu spate tuzo.

Hata kama Mpoto hakupigiwa kura bado waandaaji walikuwa wana jukumu la kulinda heshima ya shindano lao; Mpoki kumfananisha na Mpoto ni sawa na kufananisha mbingu na ardhi, wala hawakustahili kushindanishwa kabisa, matokeo yake ni haya lawama kwa waandaaji
 
kimtazamo Mpoki hakustahili tuzo ukimlinganisha na Mpoto lakini kura za watu zimempa tuzo,,,moki kapata airtime katika kipindi cha o.k hapo ndipo ushindi ulipo patikana.
 
mkuuu hii ni TUZO ambayo ilikosewa kabisaaaaa! yaani hakustahili kupewa tuzo hiyo! MPOKI RUDISHA TUZO MKUUU MWENYEWE UNAJUA UWEZO WAKO MDOGO.


Mkuu, hii nchi mambo ya kushangaa ni mengi sana zaidi ya hayo mambo ya tuzo za Kilimanjaro
 
CRAP kwa waandaaji huwezi kuweka gazeti la UDAKU ukalipambanisha na gazeti la Mwanahalisi, Raia mwema au Mwananchi harafu ukasema watu wapige kura kua gazeti lipi ni bora.
 
Mi nadhani tatizo si Mpoki japokuwa hastahili, hakustahili hata kushiriki ktk shindano hilo, wa kwanza wa kilaumiwa ni aliyependekeza majina ya washiriki halafu wapiga kura waliomchagua mpoki nao walaumiwe pia, wawili hawa kwa pamoja (wapendekeza majina na wapiga kura) wamefanya mzaha kwenye mambo ya msingi. Kwa nyimbo kama ya mpoki kuwa ndo nyimbo bora ya kiswahili ni AIBU kwa watanzania kuwa Hakuna wimbo wenye maneneo ya kujenga, kuburudisha, kuelimisha zaidi ya hiyo. WATANZANIA TUWE MAKINI.
 
......hata alieitwa kutoa Tuzo kwa Mpoki, Kanumba, nae alishtuka baada ya kufungua ile bahasha ya Mshindi na kuona ni Mpoki, aliguna DUUUUUH. nafikiri hakutegemea Mpoki kuchukua ile Tuzo.
 
Waeleze, hawajui kuwa tuzo ilitolewa kwa votes, hawajui kuwa huko uswahilini Mpoki ni maarufu kuliko Mjomba, hawajui kuwa wapiga kura walikuwa wakimpigia kura msanii badala ya wimbo; kwa uhakika wanaobeza tuzo ya Mpoki hawajui jamii ya wa Tz waliopiga kura ikoje.
anayelalamika mwenye hata kura moja hajapiga!!

watanzania bana!!
 
Mie naona Mpoki mnamwonea tu.....
Hii inaonyesha Mpoto pia umaarufu wake ni dhaifu kama angekuwa kweli yuko juu, watz wasinge mwangusha..............pole yake.
Bado Poto haja komaa na huenda asije kukomaa tena kwani umri nao wamtupa mkono!
 
Umri sio tatizo kwenye game,kwani mpoki mtoto mdogo kiumri? mie nipo darasa la tatu mpoki anachekesha mtaani? sema tu humtaki mpoto!
 
...".KM WANGEKUA MAJAJI WA MISS TZ BAS WANGEWEZA ATA KUMPITISHA ATA BI KIDUDE AWE MISS "

Rose1980 nimeipenda sana hiyo!
 
Kama mshindi anapatikana kwa kura, na wewe hukupiga kura, sioni kwa nini mnalaumu. Mkianza kusema, ooh waandaaji watumie akili zao si kura hapo ndo mtaharibu kabisaaa. Na mtakuja humu humu kulalamika kuwa tuzo zinatolewa ki upendeleo. Tukubali matokeo. Ndo democrasia. Hata kwenye siasa kura ya professor na ya muuza genge zote zinahesabiwa kama kura moja moja regardless who had capability to make sound judgement.




Hapo umesema! Nyie fans wa mjomba ndiyo mmechemsha wala siyo waandaaji wa tuzo hizo! Wao wanaangalia kura, Mpoki na wapambe wake wamemzidi mjomba na wapambe wake katika suala zima la kujitafutia kura
 
Alafu kwa taharifa watanzania walowengi hawapendi miziki utadhani lecture. Wanataka wacheke wafurahi. Nyimbo za mjomba zina wapenzi wachache sana waloenda shule. Kwa sababu anaongea aimbi. Mpoki yeye anachekesha kwa hiyo regardless anaimba nini watu wanafurahi
 
Back
Top Bottom