Tuwakumbuke waandishi wetu wa Riwaya

Kuna kitabu furani kiliitwa 'Kabwe Makanika' no 1-3 kiliandikwa na Zahir Ally lakini sijui kama ndiyo huyu baba wa Banana Zorro. Kitabu hicho kilikuwa kitamu sana.

Halafu 'Ama Zangu.....' cha Hammie Rajabu pamoja na 'Kitanda cha Mauti' cha Kajubi Mukajanga, vilikuwa vitabu vya riwaya kweli.
 
Vitabu ambavyo viko katika hazina yangu. TUTARUDI NA ROHO ZETU?, ROHO YA PAKA, SALAMU TOKA KUZIMU, MALAIKA WA SHETANI, PESA ZAKO ZINANUKA, LAZIMA UFE JORAM, DIMBWI LA DAMU vya BEN MTOBWA..NJAMA, KIKOMO, KIKOSI CHA KISASI vya ELVIS MUSIBA pia ninacho MASHIMO YA MFALME SULEIMAN. Na KIJASHO CHEMBAMBA, JOGOO LA SHAMBA NA MSAKO WA HAYANI vya EDIE GANZEL. Watunzi wote wazuri wamesha fariki.
 
1)Shafi Adam Shafi
2)Shaaban Robert
3)Mathias Mnyampala
4)Penina Mlama
5)Ndyanao Balisidya
6)Hammie Rajab
7)Alistablus E Musiba
9)Ben R Mtobwa
10)Gray Mchome
11)Sam Kitogo
12)Faraji Katarambula
13)John Simbamwene
14)Hadji Konde
15)Agoro Anduru
16)Ngalimecha Ngahyoma
17)John Rutahisingwa
18)Ngugi Wa Thiong´o(James Ngugi)
19)Peter Abraham
20)Okot Bitek
21)Chinua Achebe

22)S M Bawji
23)Nico Ye Mbajo
 
mmemsahau eddie ganzel? Kulikuwa na james akeke. Huyu sijui kama ni mtunzi au la.
 
Kna baadhi ya HADIThI zilitamba magazetini enzi hizo kma vile;
Usikose kwenye Mazishi yangu-hamisi kibari
Mtoto wa R.P.C - hamisi kibari
Mzee Beka- iliandikwa na beka mfaume gazeti la Lete Raha
siku za mwisho za uhai wangu- shigongo
 
Vitabu ambavyo viko katika hazina yangu. TUTARUDI NA ROHO ZETU?, ROHO YA PAKA, SALAMU TOKA KUZIMU, MALAIKA WA SHETANI, PESA ZAKO ZINANUKA, LAZIMA UFE JORAM, DIMBWI LA DAMU vya BEN MTOBWA..NJAMA, KIKOMO, KIKOSI CHA KISASI vya ELVIS MUSIBA pia ninacho MASHIMO YA MFALME SULEIMAN. Na KIJASHO CHEMBAMBA, JOGOO LA SHAMBA NA MSAKO WA HAYANI vya EDIE GANZEL. Watunzi wote wazuri wamesha fariki.

mkuu unaweza kunisaidia walau nitoe kopi hivyo vitabu vya Musiba
 
Kuna riwaya bahati mbaya sizikumbuki majina yake ilikuwa wahusika wake wakuu walikuwa KABWE MAKANIKA na HELEN JEURI, kama sikosei kinachomhusu huyo wa kwanza kiliandikwa na ZAHIR ZORRO!
 
riwaya nyingine nzuri iliandikwa na Kezilahabi iliitwa kaptula la Max, ila baadae kilifungiwa kitabu kile na serikali. Kwa sababu kilimponda sana babu enzi hizo
 
riwaya nyingine nzuri iliandikwa na Kezilahabi iliitwa kaptula la Max, ila baadae kilifungiwa kitabu kile na serikali. Kwa sababu kilimponda sana babu enzi hizo

Ni tamthiliya, muhusika wake mkuu kuna sehemu anasema alishaanza kuiona EGALITE
 
Musiba na willy Gamba "wake" alitukamata sana wengine miaka ile,mpaka eti tukawa tunamtengeneza willy gamba vichwani mwetu kwamba ni kijana fulani mtanashati hivi..shushushu hatari mwenye uwezo wa hali ya juu wa sanaa za mapigano.Nakumbuka willy gamba na ushujaa wake kwenye vitabu vya Elvis Musiba kama:

Njama
kikosi cha kisasi
Hofu
etc
 
Back
Top Bottom