Tuwakumbuke waandishi wetu wa Riwaya

Ibrah

JF-Expert Member
Mar 22, 2007
2,729
528
Wadau, siku hizi moyo wa kusoma vitabu vya aina zote-vya Taaluma na Riwaya umepungua sana na imepelekea Watunzi wa Riwaya kutoandika tena vitabu. Leo nawakumbuka baadhi ya Waandishi/ Watunzi wa Riwaya wa Tanzania.

Hamie Rajab
1. Miujiza ya Mlima Kolelo
2. Dunia Hadaa

S.M.Bawji
1. Usiku wa Blaa
2. Kisiwa cha Mayuku
 
Asali Chungu, Dunia Mti Mkavu, Utengano, Kiza katika Nuru, Tata za Asumini, Babu Alipofufuka by Said Ahmed Mohamed
 
Harakati za Ukombozi-Penina Mhando (Baadaye alijulikana kama Penina Mlama)
Penina alikuwa mmoja wa waandishi wa kweli miaka ile ya sabini na mwanzo wa themanini. Pia aliandika vitabu vifuatavyo (ingawa aliegemea zaidi katika michezo ya kuigiza):

1. Hatia
2. Tambueni haki zetu
3. Pambo
4. Lina Ubani
5. Wizara ya Mitumba
6. Nguzo Mama

Waandishi wengine kipindi hicho ninaowakumbuka:
Ngalimecha Ngahyoma
1. Kijiji Chetu

Gabriel Ruhumbika
1. Parapanda
2. Uwike usiwike kutakucha

Seith Chachage
1. Sudi ya Yohana
2. Almasi za Bandia
3. Kivuli
 
Kuna ambaye amewahi kukisoma hiki kitabu, Hadithi za kiboko Hugo by Mbonde, John Pantaleon
 
Agoro Anduru (ingawa hadithi zake nyingi zilikuwa za kiingereza. Huyu jamaa pia alikuwa anachapisha hadithi zake kwenye gazeti la Sunday News la enzi hizo)

1. A Bed of Roses and Other Writings
2. Loyalty to My Friend
3. Temptation and Other Stories
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom