Tuwakumbuke waandishi wetu wa Riwaya

Shaaban Robert
1. Adili na nduguze
2. Kusadikika

Hizo riwaya ulizoziweka hapo kwa kweli nilpokuwa Sekondari sikuwa nazielewa kabisa; no wonder Kiswahili nilipata D.

Wachangiachi wengi hapa ukiondoa Shossi na Hiba ya Wivu wametaja Riwaya ambazo tulilazimika kuzisoma ili tufaulu mitihani na sio kwa ajili ya kuburudika.

Ben R. Mtobwa alikuwa ni mmoja wa watunzi hodari sana; sina hakika kama alifaidika ipasavyo na vitabu vyake.
 
Mzimu wa Watu wa Kale, Kisiwa cha Giningi, Duniani Kuna Watu, Siri ya Sifuri, Mke Mmoja Watume Watatu, Mwana wa Yungi Hulewa, By Muhammed Said Abdulla

XP hivyo vyote uli visoma? You must be very rich! Riwaya zina utamu wake ingawa sidhani kama ukienda pale TPH Samora Avenue utavikuta hivyo vitabu
 
XP hivyo vyote uli visoma? You must be very rich! Riwaya zina utamu wake ingawa sidhani kama ukienda pale TPH Samora Avenue utavikuta hivyo vitabu
Mkuu hivyo vitabu vyote nilivisoma ndugu yangu... Mimi nilikuwa msomaji mzuri sana wa riwaya, na kwa bahati nzuri nilipokuwa shule ya msingi nilikuwa ndio mtunza maktaba ya shule, na Alhamdulillah shule niliyo soma ilikuwa na vitabu vingi sana, nadhani robo ya vitabu viliishia home kwangu... ah ah ah ah.

Nadhani tabia ya usomaji vitabu nimerithi kwa mzee wangu. Home kulikuwa na Novel za aina nyingi sana, nami nilikuwa siishi kumsumbua anisomee...! Na si vitabu tu hata nikiokota vijarida uko nje basi ilikuwa lazima nikipeleke home aidha mama au baba wapate kunisomea.... Hii ilipelekea nipelekwe shule ya vidudu kabla ya umri wangu kufika na ikasababisha mimi kujua kusoma haraka sana.
 
JAMAN NATAFUTA KITABU CHA AFTER 4.30
imendikwa na mkenya yule yaani navipenda vtabu vyake lakin navtafuta sivipaT so PLEEES KWA YEYOTE MWENYE KITABU KILICHOANDIKWA NA UYO MWANDISH ANICHEK
 
XP hivyo vyote uli visoma? You must be very rich! Riwaya zina utamu wake ingawa sidhani kama ukienda pale TPH Samora Avenue utavikuta hivyo vitabu

Nilikwenda pale TPH hawana hata nakala ya vitabu vyao vya zamani na wala hawajui vinapatikana wapi, Library nako hakuna kitu, sijui wasomaji walipungua au vitabu viliisha kwenye ma-shelf na hawakurudishia.

TPH pale Samora Av. wabebakia kama duka linalouza vitabu vya watu wengine, sina hakika kama viongozi wa ile taasisi waliopo sasa hivi ana vision juu ya future ya TPH.
 
JAMAN NATAFUTA KITABU CHA AFTER 4.30
imendikwa na mkenya yule yaani navipenda vtabu vyake lakin navtafuta sivipaT so PLEEES KWA YEYOTE MWENYE KITABU KILICHOANDIKWA NA UYO MWANDISH ANICHEK

Anaitwa David Mairu.
Aliandika After 4.30, Common man, The flesh, Unfit for human consumption na one by one.
Sasa hivi sipo nyumbani kwa hiyo sina uhakika kama bado ninavyo.
 
Kuna waandishi mmewasahau kama

1 Faraji Hussein Hassan Katalambula- Buriani, Simu ya kifo

2. John M.S Simbambwene- Je kweli unanipenda?, Kivumbi uwanjani, Asha, n,k

3. Hemedi Kimwanga- Lazima Afe, Mnuko wa damu, Kazikwa yu hai, nani kaua,

4. Kajubi D. Mukajanga-Mpenzi, tuanze lini. n.k

5. Elvis Musiba-Kufa na kupona, Kikosi cha kisasi, hofu, njama
 
Anaitwa David Mairu.
Aliandika After 4.30, Common man, The flesh, Unfit for human consumption na one by one.
Sasa hivi sipo nyumbani kwa hiyo sina uhakika kama bado ninavyo.

jaman wew naomba unisaidie
nikivpata ivyo vtabu ntafurai sana
yaan naupenda uandsh wa uyu bab acha tu
 
jaman wew naomba unisaidie
nikivpata ivyo vtabu ntafurai sana
yaan naupenda uandsh wa uyu bab acha tu

Ni vizuri kwa kweli japo vingine kama "unfit for human consumption" na "one by one" vinahitaji msome mkiwa wawili.

Uliwahi kukutana na series ya vitabu vya Anonymous? Kulikuwa na "Her", "Me", "them"
Vile vya David Mairu havioni ndani kwa hivi hapa.
 
Back
Top Bottom