Tusipokemea, Redio Imaan itatuvuruga

Status
Not open for further replies.
Adui ya Muislamu siyo Mkiristo ni Ibilisi, na adui ya mkiristo siyo Muislamu ni Ibilisi
Tukifahamu kwamba Ibilisi ndiyo baba ya Ufisadi, ubaguzi, uchoyo, dhulma, uwongouwongo basi sisi wana wa adamu tukaungana kwa pamoja kupambana na mambo haya bila shaka tutakuwa tunamdhoofisha Ibilisi na hatimaye kusimika misingi ya amani ya kweli, fanaka na furaha.

Mwenyezi Mungu ni mmoja na ni wetu sote, Askofu akikemea maovu yatupasa kuwaunga mkono, Mashehe wakikemea maovu yatupasa kuwaunga mkono.
Mwenyezi Mungu anasema katika Qur'an (nukuu isiyo rasmi) [" tuliandika katika Zaburi kwamba Hii Ardhi itarithiwa na waja wetu watenda mema"],
na ukisoma Zaburi ya 37 inasema (nukuu isiyo rasmi) ["The earth will be inherited by the humble"].

sasa hii hali ya kuzodoana, kunyoosheana vidole ya nini?, kwa nini tusitafute kujenga kwa kutumia njia nzuri, za mazungumzo, za kuheshimiana?.
 
... Adui ya Muislamu siyo Mkiristo ni Ibilisi, ...
Mkuu, hiyo unasema wewe kwa kuwa unaelewa maana ya dini ya kweli. Bahati mbaya kwa waisilamu wanavyofundishana kule kwenye redio imaan FM, adui ya Muislamu siyo Ibilisi ni Mkiristo !
 
Labda turudi nyuma kidogo wakati wa kampeni za uchaguzi, ilionekana ni rahisi mno kupandikiza mbegu ya udini ili kujinufaisha kisiasa.Baada ya uchaguzi kuisha nakumbuka hotoba ya Rais bugeni aliongelea suala la udini na kutaka liishe, lakini hakujua kuwa suala hilo ni nyeti mno haliwezi kuisha kirahisi. Suala la udini lilichukuliwa kimzaha na kuingizwa kwenye siasa kama ambavyo mambo mengine yamekuwa yakichukuliwa kimzaha. Kiukweli ni kuwa linapokuja suala la migongano ya kidini hakuna aliye salama,si Serikali wala vyama vya siasa. Serikali itagawanyika ,vyama vya siasa vitagawanyika vivyo hivyo jamii. Ni wajibu wa vyombo husika kuchukua hatua madhubuti kabla mambo hayaja haribika zaidi.
 
CCM walitumia ile kanuni ya DIVIDE AND RULE, lakini wameitumia kwenye dini kitu ambacho nadhani karata yao wameicheza vibaya.
 
Nami nilisikiliza mpaka mwisho hiyo jana usiku na nilikuwa makini,
ANGALIZO: Tuelekeapo hakuna wema, hebu tujiulize hivi sasa waislamu wanataka nchi igawanywe sehemu ya WAISLAMU na sehemu ya WAKRISTO. Haya maneno yapo ktk tamko rasmi la masheikh na redio Imaan imeyarejea tena jana, je Tanganyika yetu itagawanywaje kwa mujibu wa tamko?
Ilisema; mikoa yenye waislamu wengi itaunda nchi yao na mikoa yenye wakriso wengi nao wataunda nchi yao.

ANGALIZO KWA WOTE:
Hili si tamko la radio Imaan, bali ni tamko la masheikh wenye kuiwakilisha upande wa imaan ya kiislamu. Hivyo itakuwa si kuwatendea haki radio imani kwa kurusha hewani tamko lililotolewa pale Diamond jubilee last week.
 
Nami nilisikiliza mpaka mwisho hiyo jana usiku na nilikuwa makini,
ANGALIZO: Tuelekeapo hakuna wema, hebu tujiulize hivi sasa waislamu wanataka nchi igawanywe sehemu ya WAISLAMU na sehemu ya WAKRISTO. Haya maneno yapo ktk tamko rasmi la masheikh na redio Imaan imeyarejea tena jana, je Tanganyika yetu itagawanywaje kwa mujibu wa tamko?
Ilisema; mikoa yenye waislamu wengi itaunda nchi yao na mikoa yenye wakriso wengi nao wataunda nchi yao.

ANGALIZO KWA WOTE:
Hili si tamko la radio Imaan, bali ni tamko la masheikh wenye kuiwakilisha upande wa imaan ya kiislamu. Hivyo itakuwa si kuwatendea haki radio imani kwa kurusha hewani tamko lililotolewa pale Diamond jubilee last week.

unajua kuachia watu wenye upeo mdogo au wasio na elimu kuwa viongozi wa dini ni hatari sana.inabidi waislamu tubadilike masheikh wetu wale na elimu dunia siyo ya dini tu.kwani kuna mambo mengine ni reasoning capacity.
 
Hili si tamko la radio Imaan, bali ni tamko la masheikh wenye kuiwakilisha upande wa imaan ya kiislamu..
Kwani hujui gazeti likiripoti utumbo huwa linafungiwa lenyewe kwanza bila kujali source waliitoa wapi?
 
Nami nilisikiliza mpaka mwisho hiyo jana usiku na nilikuwa makini,
ANGALIZO: Tuelekeapo hakuna wema, hebu tujiulize hivi sasa waislamu wanataka nchi igawanywe sehemu ya WAISLAMU na sehemu ya WAKRISTO. Haya maneno yapo ktk tamko rasmi la masheikh na redio Imaan imeyarejea tena jana, je Tanganyika yetu itagawanywaje kwa mujibu wa tamko?
Ilisema; mikoa yenye waislamu wengi itaunda nchi yao na mikoa yenye wakriso wengi nao wataunda nchi yao.

ANGALIZO KWA WOTE:
Hili si tamko la radio Imaan, bali ni tamko la masheikh wenye kuiwakilisha upande wa imaan ya kiislamu. Hivyo itakuwa si kuwatendea haki radio imani kwa kurusha hewani tamko lililotolewa pale Diamond jubilee last week.

Walizungumza sababu gani za kutaka kugawanya nchi Mpevu??yaelekea hili la South Sudan lime-inspire sana waislamu na sasa wanaona its possible... Au ndo zile mgawanyo sawa,tunaonewa,tunafelishwa???? We would like to know their grounds!!!
 
Watanzania lazima tuelewe kuwa hata moto wa mshumaa unaweza kuunguza ghorofa, sasa mambo haya si ya kubeza hata kidogo!!!! Mamlaka husika ni lazima zitusaidie kuzuia hatari hii inayonyemelea Taifa.
 
TCRA wako wapi? au ndo wanamgwaya mkuu wa kaya? Dini zingine ndo hivyo zilisambazwa kawa jihadi (vita) kwa hiyo chokochoko kwao ni jadi. Vyombo vyetu vya dola vifanye kazi yake jamani.
 
Of ALL THE PEOPLE! HATA WEWE MAGID UNATHUBUTU KULAUMU RADIO IIMAAN NA WAISLAMU. You are too young ndugu yangu lakini fanya tafiti nzuuuri ndio baadae uje na hadithi yako hii. Mbaya zaidi umeirusha kwenye internet!!! hii itaendelea kubaki... na ukisha maliza home work yako utarudi any day kwenye media yoyote na utoe the other side of the story.

Pole sana Maggid ngoma uichezayo hujui mpigaji ni nani?
Ma'ssalaam.
Shkh Yahya.
 
TCRA wako wapi? au ndo wanamgwaya mkuu wa kaya? Dini zingine ndo hivyo zilisambazwa kawa jihadi (vita) kwa hiyo chokochoko kwao ni jadi. Vyombo vyetu vya dola vifanye kazi yake jamani.

Mkuu nchi hii ukiwa unawaunga mkono wakubwa utakuwa juu ya sheria na utafanya mambo jinsi unavyotaka wewe, hata ukiwa jambazi utafanya uhalifu na dola itakulinda, akina Masawe wako wapi?
 
unajua kuachia watu wenye upeo mdogo au wasio na elimu kuwa viongozi wa dini ni hatari sana.inabidi waislamu tubadilike masheikh wetu wale na elimu dunia siyo ya dini tu.kwani kuna mambo mengine ni reasoning capacity.

Truly,
Lakini cha msing ni HEKIMA & BUSARA zitawale, nchi yetu hii kila sekta lazima kuna watendaji wakuu wa dini hizi mbili wapo. Hivyo wenye kutoa matamko makali kiasi hiki cha MAASKOFU NA TAMKO vs WAISLAMU NA TAMKO si muendelezo mwema wa jamii yetu tulivu, ni pande zote hizo mbili zapaswa kulaaniwa kwa matamko yao ambayo tayari yameshapenyeza mpk huko kwenye minority uswahilini. Muingiliano wa jamii yetu utaangamia tena kuliko kimbari ya Rwanda ilivyokuwa...NAFSI YANGU IPO KTK MASHAKA MAKUU KWA YATAKAYOJIRI KWA UDINI NCHINI NA HATMA YA TANGANYIKA NA VIZAZI VYETU VIJAVYO.

NAYAPINGA MATAMKO YOTE YA WAKRISTO NA WAISLAMU KWA 'KUAMSHA ARI & HISIA ZA UDINI' KWA WATANZANIA.
 
mimi wacheza bao hawanichanganyi akili hata cku moja! ingekuwa ni watu wameelimika hapo sawa ningetafakari!!! kwanza ukikutwa unalumbana na mcheza bao utaitwa bao
 
Walizungumza sababu gani za kutaka kugawanya nchi Mpevu??yaelekea hili la South Sudan lime-inspire sana waislamu na sasa wanaona its possible... Au ndo zile mgawanyo sawa,tunaonewa,tunafelishwa???? We would like to know their grounds!!!

I quote kutoka katika TAMKO:
Sisi waislamu tunapendekeza sasa nchi igawanywe kwa eneo lenye waislamu wengi liunde nchi na eneo lenye wakriso wengi liundwe nchi, ...ikaendelea...kwa nini Nyerere alishupalia issue ya BIAFRA kule Nigeria kwa upande wa Kaskazini na ule wa Kusini. Ya kwamba kuna dhulma kubwa imeegemea upande wa wakristo na kwamba serikali za Tanzania zinapochomoza kufanya jambo lenye kuathiri wakristo ...basi maaskofu huitishia serikali nayo KUTISHIKA.
Hivyo kwa kuondoa yote hayo, ndipo pendekezo ni kuigawa nchi limejiri kwa misingi ya EGEMEO LA UDINI.
 
Ndugu Zangu,



JANA usiku katika pekuapekua zangu za idhaa za redioni, nikakutana, kwa mara ya kwanza, na Redio Imaan FM. Inatangaza kutoka Morogoro. Nilichosikiliza kilikuwa kipindi maalum cha marudio kutoka Jumapili iliyopita. Niseme neno moja tu na kwa msisitizo: NILISHTUKA.


Hakika, kilichokuwa kikirushwa hewani ni matangazo ya uchochezi. Kuchochea uhasama baina ya Watanzania Waislam na Watanzania wenzao Wakristo. Nilijiuliza, kama taifa tunakwenda wapi? Na maswali yakawa mengi. Je, Tume ya Utangazaji inafahamu kinachoendelea au imelala usingizi? Je, watu wetu wa Intelijensia hawana taarifa za Kiintelijensia juu ya kinachooendelea?


Naam. uzoefu unatufundisha, kuwa kuwasha moto ni jambo jepesi sana, lakini, kuuzima moto, yaweza kuwa ni kazi ngumu sana.


Moto ulioanza kwenye nyumba moja ya nyasi kijijini, waweza kusambaa haraka na hata kuteketeza nyumba nyingine, mali na kuhatarisha maisha.


Nimekumbushia mara kadhaa, kuwa historia ni mwalimu mzuri. Mwezi Aprili 6, mwaka 1999 katika iliyokuwa Hoteli ya Kilimanjaro, Bi Joy Mukanyange , aliyekuwa Balozi wa Rwanda hapa Tanzania, alituambia Watanzania juu ya kile alichokiona lakini sisi Watanzania hatukukiona. Ilikuwa ni katika mjadala rasmi wa kumbukumbu ya mauji ya kimbari ya watu wa Rwanda ya mwaka 1994.


Bi Mukanyange alisema: " Naogopa., kwani nimeanza kuona dalili zinazojengeka za mgawanyiko wa kidini nchini Tanzania na eneo lote la Maziwa Makuu, hali ambayo inaweza kusababisha mauaji ya halaiki kama yale yaliyotokea nchini mwetu mwaka 1994," alisema Balozi huyo wa Rwanda kabla ya kuendelea kutoa ufafanuzi wa historia ya Rwanda na matukio yaliyosababisha maujai yale ya Wanyarwanda ya wao kwa wao. Ni kauli ya kuitafakari kwa makini.


Mimi sasa naamini, kuwa Afrika mvunja nchi si mwananchi, bali ni mwanasiasa. Ni kwa kutanguliza mbele maslahi ya kisiasa badala ya kitaifa. Masikini nchi yetu, Watanzania hawana udini ila kuna wachache, na hasa wanasiasa, walio tayari kutumia mtaji wa udini kutimiza malengo yao. Inasikitisha sana, kuwa baadhi ya wanasiasa, hata kwa kutumia udini, wameamua kutupitisha Watanzania katika njia isiyo salama. Ili mradi, malengo yao yatimie.


Watanzania tukubali sasa, kuwa nchi yetu imepatwa na bahati mbaya ya baadhi ya Watanzania wenzetu kuanza kupandikiza mbegu za chuki miongoni mwetu. Kuna wanaotaka tuanze kubaguana kwa misingi ya kidini. Hili ni jambo la hatari sana.
Taratibu tumeanza kuizoea misamiati ya sisi na wao. Mathalan, sisi Wakristo na wao Waislamu. Sisi Wachagga na wao Wazaramo. Tunasahau, kuwa katika nchi yetu hii hakuna Sisi na Wao, kuna SISI tu.Tutakapokumbwa na maafa ya kitaifa watakaoathirika ni SISI, hakutakuwa na WAO.


Hatari kubwa ninayoiona ni tatizo la baadhi ya Watanzania kuwa na ufahamu mdogo juu ya dunia tunayoishi sasa, kibaya zaidi,ufahamu mdogo wa historia yetu. Uelewa wa historia ya jamii husika ni jambo muhimu sana.
Kiumbe huwezi kuelewa ya leo, kesho na kesho kutwa kama huelewi ya jana. Kuielewa historia yako ni kuelewa ulipo na unakokwenda.


Dalili tunazoziona sasa za kupandikiza mbegu za chuki kwa misingi ya udini si dalili njema. Haya yatatupelekea kwenye maafa.


Hii ni nchi yetu. Katika ulimwengu tunamoishi kuna mamilioni ya watu wasio na nchi. Wahenga wetu walishiriki katika kuijenga nchi hii, wametutarajia sisi tuendelee kuijenga na kuilinda hadhi ya nchi hii.


Muda wetu wa kuishi humu duniani ni mfupi sana. Tuyachambue matatizo halisi ya jamii yetu. Kisha tusiishie kwenye kuyaorodhesha, hiyo ni kazi rahisi sana. Tutafute njia ya kuyatatua matatizo hayo.


Hatuna haja ya kubaguana kwa misingi ya ukabila, dini na rangi. Sisi wote ni Watanzania. Tuna historia ya kujivunia. Ni historia yetu wenyewe.
Mtanzania halisi na mkweli kwa nchi yake atazungumzia matatizo ya Tanzania kwa ujumla wake. Hatakuwa na sababu ya kunyoosha kidole kwa Wahindi, Walutheli, Waprotestanti, Wasabato, Wakatoliki, Washia, Wasunni, Waismailia, wenye kuamini jadi, Wazaramo, Wagogo au Wachagga, kwamba ndio wa kulaumiwa.
Wenye kuathirika na umasikini wa nchi hii ni wengi mno. Si Wakristo peke yao, si Waislamu peke yao, si Wapagani peke yao, si Wamachinga peke yao na si Wazaramo peke yao.


Wahenga walisema "kamba hukatikia pabovu". Kamwe huwezi kuwavuruga Watanzania na kuwafanya wachinjane kwa sababu za kudai kuna upendeleo wa ukabila au wa kisiasa. Nchi hii ina makabila zaidi ya 125 na utitiri wa vyama vya siasa.


Mahala ambapo unaweza kuwagawa Watanzania na hata kufanikiwa wachinjane ni kwenye masuala ya imani. Tusikubali dini iwe ndiyo penye ubovu kwenye kamba inayotuunganisha Watanzania. Mungu Ibariki Tanzania.
Maggid
Dar es Salaam
Januari 19, 2011
http://mjengwa.blogspot.cm
ANALYSIS hii uifanye kwa vyombo vyote vya habari vya kidini utaona kila chombo kinatishia amani, kwa kuwa itikadi yako si yangu na yangu si yako, kwahiyo kama umeyasikia na kuaya-analize hayo ni kwa kuwa yapo kinyume na itikadi yako achana nayo, fungua na sikiliza yale yanayokuhusu ili ufurahike na nafsi yako, ulivyokereka ndivyo wanavyokereka wa upande huo wakisiliza, kuona au kusoma ya upande wapili, kwahiyo hayo ni maoni yako binafsi, na yale ni maoni yao binafsi, acheni propaganda naona mnabadili post ujumbe ni uleule radio imaan, annur nk, kubwa hampendi kusikia waislam wamesema vyombo vya habari vya kikristo vipo tele kila kukicha mnakuja na habari mpya waraka, maoni, matamko, nk wakisema wenzenu presha zinawapanda ama kweli ingekuwa wanavyombo kama vyenu sijui ingekuwaje! maana naona JF sasa vyombo vinavyowaumiza ni annur na redio imaan na bado mmezoea kusema nyie tu! mnabadilisha post tu, content ileile! Tunawajua na tumewazoe
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom