Tusipokemea, Redio Imaan itatuvuruga

Status
Not open for further replies.
uwe unaleta na majadiliano ya maaskofu yanayojadili kukandamiza Uislam-umeanza kwa dharau kuwa kwa bahati mbaya imetokea ukasikiliza redio hii wakati ukitafuta stesheni na kwamba wewe huwa husikilizi-wote waliochangia kwa nia ya kuudhalilisha Uislam na mmelaaniwa, mlipashwa kuzungumzia redio na sio dini

mchangiaji wa mada apo juu kachangia vizuri wee ndo unataka kupotosha jamii, kwani aliyewaambia nyie waislamu msiende shule ni nani,na kuna jambo jingine la mihadhara piteni pale manzese darajani msikilize iyo ki2 inaitwa mihadhara!kama mnaona amkusoma jipangeni muende shule sasa.acheni majungu na mfanye kazi.
 
mchangiaji wa mada apo juu kachangia vizuri wee ndo unataka kupotosha jamii, kwani aliyewaambia nyie waislamu msiende shule ni nani,na kuna jambo jingine la mihadhara piteni pale manzese darajani msikilize iyo ki2 inaitwa mihadhara!kama mnaona amkusoma jipangeni muende shule sasa.acheni majungu na mfanye kazi.

Bora ungesikiliza hiyo mihadhara ukaelimika kuliko kubaki kwenye ujinga wako wa sasa na kufikiri umesoma, wewe ni huna elimu yeyote ile mtupu kabisa..nenda kawasikilize watakusaidia..ok
 
mchangiaji wa mada apo juu kachangia vizuri wee ndo unataka kupotosha jamii, kwani aliyewaambia nyie waislamu msiende shule ni nani,na kuna jambo jingine la mihadhara piteni pale manzese darajani msikilize iyo ki2 inaitwa mihadhara!kama mnaona amkusoma jipangeni muende shule sasa.acheni majungu na mfanye kazi.
bora uelewe hivyohivyo kuwa waislam hawajaenda au hawaendi shule! hao wakristo walioenda shule wako wapi au ndio ufisadi waliosomea!
 
Wadau, jana katika kubadilisha station ya radio yangu nilikutana na mjadala uliokuwa ukiendeshwa redio imani, hii ni redio ya kiislamu iliyoko mjini Morogoro. Ingawa si kawaida yangu kuisikiliza lakini nilishawishika kuwasikiliza kutokana na uzito wa mambo yaliyokuwa yakijadiliwa.

Mjadala ulihusu tamko walilotoa kuhusu maaskofu, walivilaumu vyombo vya habari – magazeti particularly mwananchi na magazeti mengine kama nipashe, Tz Daima etc kwamba yamepotosha tamko lao pamoja na kuwa waliwapa tamko hilo kimaandishi. Nilijiuliza inakuwaje magazeti yote yanakosea kitu kilekile.
Kilichonisikitisha katika mjadala huo ni uchochezi na upotoshaji wanaoueneza hawa masheikh kwa sababu wanazojua wao. Kwa mfano walisema nchi inaendeshwa kwa mfumo wa kikiristu toka enzi za Nyerere, moja ya madai yao ni kwamba waislaumu walikuwa wakifelishwa makusudi shuleni ili wasisome, bila shaka haya ni madai makubwa sana.
Mambo mengine ni kwamba ili kudhibitisha kwamba nchi inaendeshwa kikristo ni kwa nini wakristo wana university na hospitali nyingi kuliko serikali, madai mengine ni kwamba kwa nini hospitali za kikristo zilizotaifishwa na serikali zilirudishwa , bila shaka katika hili ni kwamba serikali ilishindwa kuziendesha, lakini kwa sababu wanazojua wao waliishia kulaumu mfumo wa utawala wa kikristo. Katika hili wao walikiri kwamba hakurudishiwa kitu kwa kuwa hawakunyanganywa kitu!
Baada ya kumaliza majadiliano waliruhusu wasikilizaji kutuma sms na kupiga simu studio, wengi wa wachangiaji waliwashukuru masheikh kwa hatua yao lakini pia kuna waliosema watajichukulia sheria mkononi ili kuwaadhibu waandishi, na wengine walitaka itangazwe jihad dhidi yao.
Nilivyoona mimi hakuna shabaha nyingine zaidi ya kuleta chuki miongoni mwa dini jambo ambalo si kawaida yetu watz.

Ingawa najua kwamba redio hii haina wasikilizaji wengi lakini mijadala ya uchochezi namna ile haitakiwi kupita bila kukemewa. Katika mauaji ya Rwanda redio zilitumika sana kuchochea chuki baina ya watu, hatutakiwi kufika huko, nadhani ni wakati muafaka kwa “intelijensia” ya polisi kufanya kazi sasa ili kuzuia maafa yanayoweza kutokana na uchochezi wa redio imani

Wana JF naomba kuwakilisha


Madai yao yana ukweli sana, ukisoma kitabu cha Dr. Surlivan ' KANISA KATOLIKI NA SIASA ZA TANZANIA' hapo ndipo utajua ujasusi alio ufanya Nyerere kwa waislamu ambapo mpaka sasa unaendelea !
 
Waislamu ndugu zangu, mbona tunamatatizo mengi kijamii yanayohitaji utatuzi wetu wala sio kulialia kwa wakristo, mbona tunatafuta huruma katika maswala ambayo tunaweza kutatua wenyewe ? ni ujinga kwakweli
Anaelialia hapo juu kwenye mada ni mkiristo wala si Muislam! yeye ndiye anaelia na Radio Imaan! si ukiona redio inakukera unabadili stesheni tu ya kazi gani ebo!! Mara gazeti An-Nuur mara Radio Imaan... wakimaliza huko watakuja na Radio Tumaini na gazeti la msemakweli.... kisha Kiu, Ijumaa na mengineyo!!

Hivi hakuna mambo ya msingi ya kujadili?
 
Bora wewe umeliona hili na kulileta hapa jamvin.Ipo haja kwa hiyo intelijensia kufuatilia mambo ya msingi kama haya na sio kuvunja maandamano ya aman.Radio Iman+gazet la Al nur ni vyombo vya habari vya kichochezi na visivyokuwa na maadili.Binafsi nimekuwa nikifuatilia habari zao hasa wakati wa kampeni,kwa kweli inasikitisha,sijui kwa nini yanazidi kukumbatiwa!
Huwezi kupenda kusikiliza kitu usichokipenda!!! Unafiki mtupu... hupendi kisha usikilize? ina maana unaifanyia ufisadi nafsi yako? Acheni basi kutuhadaa kuwa hamtaki huku mnakubali kwenda!!
 
Gay or no gay they think with their heads not their private parts.
Mbona top brass ya bretton woods institutions zote ni gays and yet all our national fiscal policies are dictated by them ?
yeyote anaetenda ama kutendwa kinyume na maumbile.... hayuko timamu kijinsia (akili zake haziko sawa) tafiti mbalimbali zimethibitisha hilo.
 
لداود ‎باركي يا نفسي الرب وكل ما في باطني ليبارك اسمه القدوس‎
 
Ndugu Zangu,



JANA usiku katika pekuapekua zangu za idhaa za redioni, nikakutana, kwa mara ya kwanza, na Redio Imaan FM. Inatangaza kutoka Morogoro. Nilichosikiliza kilikuwa kipindi maalum cha marudio kutoka Jumapili iliyopita. Niseme neno moja tu na kwa msisitizo: NILISHTUKA.


Hakika, kilichokuwa kikirushwa hewani ni matangazo ya uchochezi. Kuchochea uhasama baina ya Watanzania Waislam na Watanzania wenzao Wakristo. Nilijiuliza, kama taifa tunakwenda wapi? Na maswali yakawa mengi. Je, Tume ya Utangazaji inafahamu kinachoendelea au imelala usingizi? Je, watu wetu wa Intelijensia hawana taarifa za Kiintelijensia juu ya kinachooendelea?


Naam. uzoefu unatufundisha, kuwa kuwasha moto ni jambo jepesi sana, lakini, kuuzima moto, yaweza kuwa ni kazi ngumu sana.


Moto ulioanza kwenye nyumba moja ya nyasi kijijini, waweza kusambaa haraka na hata kuteketeza nyumba nyingine, mali na kuhatarisha maisha.


Nimekumbushia mara kadhaa, kuwa historia ni mwalimu mzuri. Mwezi Aprili 6, mwaka 1999 katika iliyokuwa Hoteli ya Kilimanjaro, Bi Joy Mukanyange , aliyekuwa Balozi wa Rwanda hapa Tanzania, alituambia Watanzania juu ya kile alichokiona lakini sisi Watanzania hatukukiona. Ilikuwa ni katika mjadala rasmi wa kumbukumbu ya mauji ya kimbari ya watu wa Rwanda ya mwaka 1994.


Bi Mukanyange alisema: " Naogopa., kwani nimeanza kuona dalili zinazojengeka za mgawanyiko wa kidini nchini Tanzania na eneo lote la Maziwa Makuu, hali ambayo inaweza kusababisha mauaji ya halaiki kama yale yaliyotokea nchini mwetu mwaka 1994," alisema Balozi huyo wa Rwanda kabla ya kuendelea kutoa ufafanuzi wa historia ya Rwanda na matukio yaliyosababisha maujai yale ya Wanyarwanda ya wao kwa wao. Ni kauli ya kuitafakari kwa makini.


Mimi sasa naamini, kuwa Afrika mvunja nchi si mwananchi, bali ni mwanasiasa. Ni kwa kutanguliza mbele maslahi ya kisiasa badala ya kitaifa. Masikini nchi yetu, Watanzania hawana udini ila kuna wachache, na hasa wanasiasa, walio tayari kutumia mtaji wa udini kutimiza malengo yao. Inasikitisha sana, kuwa baadhi ya wanasiasa, hata kwa kutumia udini, wameamua kutupitisha Watanzania katika njia isiyo salama. Ili mradi, malengo yao yatimie.


Watanzania tukubali sasa, kuwa nchi yetu imepatwa na bahati mbaya ya baadhi ya Watanzania wenzetu kuanza kupandikiza mbegu za chuki miongoni mwetu. Kuna wanaotaka tuanze kubaguana kwa misingi ya kidini. Hili ni jambo la hatari sana.
Taratibu tumeanza kuizoea misamiati ya sisi na wao. Mathalan, sisi Wakristo na wao Waislamu. Sisi Wachagga na wao Wazaramo. Tunasahau, kuwa katika nchi yetu hii hakuna Sisi na Wao, kuna SISI tu.Tutakapokumbwa na maafa ya kitaifa watakaoathirika ni SISI, hakutakuwa na WAO.


Hatari kubwa ninayoiona ni tatizo la baadhi ya Watanzania kuwa na ufahamu mdogo juu ya dunia tunayoishi sasa, kibaya zaidi,ufahamu mdogo wa historia yetu. Uelewa wa historia ya jamii husika ni jambo muhimu sana.
Kiumbe huwezi kuelewa ya leo, kesho na kesho kutwa kama huelewi ya jana. Kuielewa historia yako ni kuelewa ulipo na unakokwenda.


Dalili tunazoziona sasa za kupandikiza mbegu za chuki kwa misingi ya udini si dalili njema. Haya yatatupelekea kwenye maafa.


Hii ni nchi yetu. Katika ulimwengu tunamoishi kuna mamilioni ya watu wasio na nchi. Wahenga wetu walishiriki katika kuijenga nchi hii, wametutarajia sisi tuendelee kuijenga na kuilinda hadhi ya nchi hii.


Muda wetu wa kuishi humu duniani ni mfupi sana. Tuyachambue matatizo halisi ya jamii yetu. Kisha tusiishie kwenye kuyaorodhesha, hiyo ni kazi rahisi sana. Tutafute njia ya kuyatatua matatizo hayo.


Hatuna haja ya kubaguana kwa misingi ya ukabila, dini na rangi. Sisi wote ni Watanzania. Tuna historia ya kujivunia. Ni historia yetu wenyewe.
Mtanzania halisi na mkweli kwa nchi yake atazungumzia matatizo ya Tanzania kwa ujumla wake. Hatakuwa na sababu ya kunyoosha kidole kwa Wahindi, Walutheli, Waprotestanti, Wasabato, Wakatoliki, Washia, Wasunni, Waismailia, wenye kuamini jadi, Wazaramo, Wagogo au Wachagga, kwamba ndio wa kulaumiwa.
Wenye kuathirika na umasikini wa nchi hii ni wengi mno. Si Wakristo peke yao, si Waislamu peke yao, si Wapagani peke yao, si Wamachinga peke yao na si Wazaramo peke yao.


Wahenga walisema "kamba hukatikia pabovu". Kamwe huwezi kuwavuruga Watanzania na kuwafanya wachinjane kwa sababu za kudai kuna upendeleo wa ukabila au wa kisiasa. Nchi hii ina makabila zaidi ya 125 na utitiri wa vyama vya siasa.


Mahala ambapo unaweza kuwagawa Watanzania na hata kufanikiwa wachinjane ni kwenye masuala ya imani. Tusikubali dini iwe ndiyo penye ubovu kwenye kamba inayotuunganisha Watanzania. Mungu Ibariki Tanzania.
Maggid
Dar es Salaam
Januari 19, 2011
http://mjengwa.blogspot.cm
 
ndugu zangu,



jana usiku katika pekuapekua zangu za idhaa za redioni, nikakutana, kwa mara ya kwanza, na redio imaan fm. Inatangaza kutoka morogoro. Nilichosikiliza kilikuwa kipindi maalum cha marudio kutoka jumapili iliyopita. Niseme neon moja tu na kwa msisitizo: Nilishtuka.


Hakika, kilichokuwa kikirushwa hewani ni matangazo ya uchochezi. Kuchochea uhasama baina ya watanzania waislam na watanzania wenzao wakristo. Nilijiuliza, kama taifa tunakwenda wapi? Na maswali yakawa mengi. Je, tume ya utangazaji inafahamu kinachoendelea au imelala usingizi? Je, watu wetu wa intelijensia hawana taarifa za kiintelijensia juu ya kinachooendelea?


Naam. Uzoefu unatufundisha, kuwa kuwasha moto ni jambo jepesi sana, lakini, kuuzima moto, yaweza kuwa ni kazi ngumu sana.


Moto ulioanza kwenye nyumba moja ya nyasi kijijini, waweza kusambaa haraka na hata kuteketeza nyumba nyingine, mali na kuhatarisha maisha.


Nimekumbushia mara kadhaa, kuwa historia ni mwalimu mzuri. Mwezi aprili 6, mwaka 1999 katika iliyokuwa hoteli ya kilimanjaro, bi joy mukanyange , aliyekuwa balozi wa rwanda hapa tanzania, alituambia watanzania juu ya kile alichokiona lakini sisi watanzania hatukukiona. Ilikuwa ni katika mjadala rasmi wa kumbukumbu ya mauji ya kimbari ya watu wa rwanda ya mwaka 1994.


Bi mukanyange alisema: " naogopa., kwani nimeanza kuona dalili zinazojengeka za mgawanyiko wa kidini nchini tanzania na eneo lote la maziwa makuu, hali ambayo inaweza kusababisha mauaji ya halaiki kama yale yaliyotokea nchini mwetu mwaka 1994," alisema balozi huyo wa rwanda kabla ya kuendelea kutoa ufafanuzi wa historia ya rwanda na matukio yaliyosababisha maujai yale ya wanyarwanda ya wao kwa wao. Ni kauli ya kuitafakari kwa makini.


mimi sasa naamini, kuwa afrika mvunja nchi si mwananchi, bali ni mwanasiasa. Ni kwa kutanguliza mbele maslahi ya kisiasa badala ya kitaifa. Masikini nchi yetu, watanzania hawana udini ila kuna wachache, na hasa wanasiasa, walio tayari kutumia mtaji wa udini kutimiza malengo yao. Inasikitisha sana, kuwa baadhi ya wanasiasa, hata kwa kutumia udini, wameamua kutupitisha watanzania katika njia isiyo salama. Ili mradi, malengo yao yatimie.


watanzania tukubali sasa, kuwa nchi yetu imepatwa na bahati mbaya ya baadhi ya watanzania wenzetu kuanza kupandikiza mbegu za chuki miongoni mwetu. Kuna wanaotaka tuanze kubaguana kwa misingi ya kidini. Hili ni jambo la hatari sana.
Taratibu tumeanza kuizoea misamiati ya sisi na wao. Mathalan, sisi wakristo na wao waislamu. Sisi wachagga na wao wazaramo. Tunasahau, kuwa katika nchi yetu hii hakuna sisi na wao, kuna sisi tu.tutakapokumbwa na maafa ya kitaifa watakaoathirika ni sisi, hakutakuwa na wao.


Hatari kubwa ninayoiona ni tatizo la baadhi ya watanzania kuwa na ufahamu mdogo juu ya dunia tunayoishi sasa, kibaya zaidi,ufahamu mdogo wa historia yetu. Uelewa wa historia ya jamii husika ni jambo muhimu sana.
Kiumbe huwezi kuelewa ya leo, kesho na kesho kutwa kama huelewi ya jana. Kuielewa historia yako ni kuelewa ulipo na unakokwenda.


Dalili tunazoziona sasa za kupandikiza mbegu za chuki kwa misingi ya udini si dalili njema. Haya yatatupelekea kwenye maafa.


Hii ni nchi yetu. Katika ulimwengu tunamoishi kuna mamilioni ya watu wasio na nchi. Wahenga wetu walishiriki katika kuijenga nchi hii, wametutarajia sisi tuendelee kuijenga na kuilinda hadhi ya nchi hii.


Muda wetu wa kuishi humu duniani ni mfupi sana. Tuyachambue matatizo halisi ya jamii yetu. Kisha tusiishie kwenye kuyaorodhesha, hiyo ni kazi rahisi sana. Tutafute njia ya kuyatatua matatizo hayo.


Hatuna haja ya kubaguana kwa misingi ya ukabila, dini na rangi. Sisi wote ni watanzania. Tuna historia ya kujivunia. Ni historia yetu wenyewe.
Mtanzania halisi na mkweli kwa nchi yake atazungumzia matatizo ya tanzania kwa ujumla wake. Hatakuwa na sababu ya kunyoosha kidole kwa wahindi, walutheli, waprotestanti, wasabato, wakatoliki, washia, wasunni, waismailia, wenye kuamini jadi, wazaramo, wagogo au wachagga, kwamba ndio wa kulaumiwa.
Wenye kuathirika na umasikini wa nchi hii ni wengi mno. Si wakristo peke yao, si waislamu peke yao, si wapagani peke yao, si wamachinga peke yao na si wazaramo peke yao.


Wahenga walisema "kamba hukatikia pabovu". Kamwe huwezi kuwavuruga watanzania na kuwafanya wachinjane kwa sababu za kudai kuna upendeleo wa ukabila au wa kisiasa. Nchi hii ina makabila zaidi ya 125 na utitiri wa vyama vya siasa.


Mahala ambapo unaweza kuwagawa watanzania na hata kufanikiwa wachinjane ni kwenye masuala ya imani. Tusikubali dini iwe ndiyo penye ubovu kwenye kamba inayotuunganisha watanzania. Mungu ibariki tanzania.
Maggid
dar es salaam
januari 19, 2011
http://mjengwa.blogspot.cm

majjid, mbona hujasema nini wamezungumza? Weka angalau nusu tujadili, pengine wamesema kwamba maaskofu wameuchukia utwala wa jk halafu useme ndio uchochezi
 
Hawawezi kuguswa hao ni wateule wa tz wacha waendelee na uchochezi wao labda ni mafundisho yao ya dini yanawafundisha hivyo!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom