Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,812
- 11,987
Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) ambao ndio wafadhili wakuu wa kujenga vituo vya Serikali kupitia Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wamekamilisha ujenzi wa kituo cha redio ya jamii katika Halmashauri ya Mpimbwe Mkoani Katavi chenye thamani ya zaidi ya Tsh. Milioni 200 ikiwa ni sehemu ya kusogeza huduma kwa Wananchi.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizindua redio hiyo amewataka watumishi wa Serikali kutumia Vyombo vya Habari hasa redio katika kusikiliza kero na kuzitatua kwa haraka ili kuleta msukumo wa maendeleo.
Baadhi ya wananchi wa maeneo hayo wamefurahishwa navuzinduzi wa redio hiyo ambapo awali hapakua na usikivu wa redio aina yoyote.