Turudi kwenye unyago au tuendelee na kitchen party?

Jamani akina K mbona wengine mnakuwa wakari hvyo na wakati mleta mada mwenyewe Nazjazi ni mdada kama nyie na japo simjuhi lakini anaonekana ni muungwana,mkweli na anajiheshimu sana,simply anadisclose ukweli wa mambo nyie mnakuwa wakali,WHY??japo ukweli ni mchungu na unauma lakini kwa ukweli kabisa hamna budi kuukubali vingnevyo mtaendelea kuchezewa,kuachwa na kuumizwa in many ways
 
Mule mule kaka, tuna shida ya maadili ktk ndoa zetu ..nimeipenda hiyo samahani- imetulia!
Naz sijui napatia au nachemsha hapa
Swala sio unyago wala kitchen party

Swala zima hapa ni malezi ya watoto wetu maana watoto wanalelewa kudekezwa mpaka wanapitiliza
Utakuta msichana mkubwa kabisa au mvulana mkubwa kabisa anafuliwa nguo na house gal anaandaliwa msosi mezani na house gal na akimaliza house gal anakuja kuondoa vyombo na kuosha
Anatandikiwa kitanda na house gal

Sasa mtu kama huyo anafikiia kuwa anatakiwa kuoa au kuolewa tuseme zaidi hawa wa kuolewa. Anaenda kw amumewe hajui kupika, kufua, wala hajawahi kutandika kitanda chake mwenyewe.

Unafikiri hapo hata kama utampa mafunzo ya unyago wa mwezi mmoja au kitchen party ya masaa au wiki moja atafundishika ajue kuwa kuna kupika au kufua au kupiga deki nyumba au kumjali mumewe amtengee chakula au hata maji ya kuoga au ajue mumewe anavaa nguo gani kama sio unaleta balaa

Ndo hao sasa wanaoishia kuwa ndani ya nyumba kila kitu kinafanywa na house gal na yeye anajiweka as if majukumu ya ndani hayajui ni ya house gal
Akigeukwa na the same house gal wala hana haja ya kulalamika
Tukubali malezi ya watoto yanachangpia sana na sidhani unyago wa muda mfupi au kitchen party inasaidia kufanya lolote kwa watu wa aina hii
Nisamehe kama nimetoka nje ya mada
 
.....tuwaache tu na masomo yao....tuoe mahouse gal,ndio wanajua wajibu wa mke


Sikatai kua wanawake wengi siku hizi hawajali hayo mambo ila kuna baadhi wanajitahidi sana lakini dume halitulii. Kama mume ni mkware hata ukimsujudia bado atatoka nje. Mpaka unajiuliza hivi huyu kwa mkewe anakosa nini?
 
Back
Top Bottom