Tupia imani ya kale uliyowahi kusikia

Tetra

JF-Expert Member
Oct 5, 2012
1,520
764
Kuna imani za kale zilizoaminiwa na jamii ktk makabila na tamaduni mbalimbali mfano
1.UKIPALIWA KUNA MTU ANAKUSEMA
2.JOGOO AKIWIKA USIKU UJUE KUNA MTU ATAKUFA
3.MKONO WA KULIA UKIWASHA UTAPATA PESA
tupia na wewe imani uliyowahi kusikia
 
Bundi akilia karibu na nyumbani ujue mchawi amekamilisha kazi ya kuwaloga, mtapoteza mtu, huenda ni wewe.
 
ukipata kazi mshahara wote wa kwanza bila kukata kitu wapelekee wazazi
(kumbe lengo wajua unapokea sh ngapi nao wafaidi)
ukipiga sana chafya mchana ujue mtapata wageni muhimu.
ukibeba viazi vikuu kusafirisha mtapata ajali( kumbe ili usibebe viazi vyao)
 
Kuna imani za kale zilizoaminiwa na jamii ktk makabila na tamaduni mbalimbali mfano
1.UKIPALIWA KUNA MTU ANAKUSEMA
2.JOGOO AKIWIKA USIKU UJUE KUNA MTU ATAKUFA
3.MKONO WA KULIA UKIWASHA UTAPATA PESA
tupia na wewe imani uliyowahi kusikia

Pele (Mbrazil) ni Mtanzania
Mohammadi Ali ni Mtanzania (Hii ilikuwa ni miaka ya 84-85)
 
Kitovu cha mtoto kikikatika kisidondokee nanihino (hasa kwa mtoto wa kiume), vinginevyo mtoto atakuwa si rizki!

True or not, nilihakikisha hakidondoki vibaya kwa mwanangu, kwa kuwa sikuwa na cha kupoteza kwa kuhakikisha hakidondokei nanihino.......
 
Back
Top Bottom