Je, unajua ni kwanini huruhusiwi kuingia au unaingia kwa masharti yasiyo ya kawaida maeneo ya kitalii kama Antarctica na mfano wake?

Trainee

JF-Expert Member
Sep 22, 2018
2,220
2,825
Habari,

Serikali za mataifa mengi duniani zina tabia ya kuweka mazuio na masharti kwenye baadhi ya mambo halafu sababu ya zuio na masharti inafichwa

Kwa mfano kwenye nyingi ya sehemu za vivutio vya utalii hapa nchini utakuta kumewekwa visheria vya ajabu ajabu ukitaka kuingia mpaka kutoka

Utakuta sehemu unaambiwa usivae vazi fulani mfano viatu, au unaambiwa ni lazima utumie kitu fulani hapo mfano unawe maji, au upite kwa staili fulani mfano uzunguke mti, au useme maneno fulani mfano kubisha hodi nk

Vikanuni hivyo kwa maeneo mengi ni kwa sababu za kishirikina na uchawi ambapo vimebatizwa jina la mizimu na mila. Lakini leo nakupa sababu nyingine tofauti na hizo za uchawi na ushirikina

Kwanza kabisa kama wewe siyo muumini wa dini ya kiislamu au kikristo nakushauri ishia hapa hapa kusoma maana hoja ninayotaka kumalizia haiingii akilini kwa mpagani wala kafiri wala yeyote mwenye kufanana nao!

Ukisoma vitabu vya maneno ya mwenyezi Mungu utakuta kumetajwa mambo mbalimbali ya kale ambayo ukifuatilia utakuta yanadokeza majambo fulani fulani

Ukisoma kwa mfano quran utakuta kila inapodokeza jambo fulani nyeti inamalizia na maneno "kwa hili kuna mazingatio kwa wenye akili" "...kwa wenye imani" "... kwa wenye kushukuru" "...ikiwa mnajua" na maneno mengine mfano wa hayo!

Mara nyingi pia aya za quran zinamalizia kwa kutaja sifa mahsusi za mwenyezi Mungu mfano "hakika mwenyezi Mungu ni muweza na mjuzi" "... mjuzi mwenye hekima" "mkadiriaji wa mambo yote kwa kila kitu" na kadhalika

Kuna mara kadhaa tena Mola anatumia maneno"ishara zetu" na maneno mengine mengi. Ukifuatilia vizuri maneno hayo ya mwenyezi Mungu kwenye vitabu vya dini utagundua baadhi ya mambo yanayotajwa yanahitaji tafiti (kwa mwenye kutaka kujiridhisha)

Vitu kama VIJANA WA PANGONI KUTOKUOZA MIAKA ZAIDI YA MIAKA 300 WAMELALA.

HABARI YA DHU QARNAIN NA KIZUIZI ALICHOWAJENGEA JAMII YA YA'JUJ NA MA'JUJ.

HABARI ZA MUSSA NA WANA WA ISRAEL KWENYE MTO NILE
HABARI ZA MIUJIZA KEDEKEDE YA MITUME WALIOTANGULIA ZAMANI NA KADHALIKA

Mambo yote hayo yanawezekana kuyatafiti na kujifunza zaidi kuhusu uwepo wa Mungu na uweza wake Kinachotokea ni kwamba kuna waliojimilikisha hii dunia na hawataki yeyote aijue kama wao wala zaidi yao hivyo wakiona tu kuna kaupenyo kidogo ka mtu kutafiti maneno ya mwenyezi Mungu basi wanawahi kukaziba ili asifanikiwe kamwe!

Ukiniuliza lengo kubwa ni nini nitakujibu lengo ni kuficha ukweli wa Mwenyezi Mungu ili wapate kundi kubwa la kuingia nalo motoni!
 
Kwani maajabu ya Mungu yapo kwenye uumbaji wa sehemu zinazovyutia peke yake..



Mwili wako tu ni very complex ni ajabu Kuu jinsi mifumo ilivyo so mtu kama ni kuamini Mungu aamue tu mwenyewe asifikirie
 
Back
Top Bottom