Tundu Lissu yuko sahihi: Majaji wengi hawajahitimu vyuo na elimu zao ni za mitandaoni

Hivi huyu Werema AG (SIC!), akisikia jambo kutoka kwa LS kwanini asijiridhishe kwa kufanya ka UTAFITI kidogo kuliko ku opt kumtukana LS?

Sasa hivi hata Idara ya mahakama inamchukia Werema, pale alipopinga hoja ya TL, kwamba budget ya mahakama itolewa in percetange 3%? au 2%, kama ilivyo Bunge na Vyama vya siasa hiyo ingesaidia kuondoa ukata ktk idara ya mahakama. Lakini Werema akapinga kwa HOJA YA NGUVU! As usual Magamba wenzake waka mu support. Idara ya mahakama inaona CDM wana VISION kuliko CCM!

Kama ndio Hivyo basi Watende Haki na Mungu atakuwa Upande Wao!! Ila kwa issue ya kuwa na Majaji wasiokuwa na hata Vyeti vya elimu Hiyo sasa ni soo!!
 
Hili gazeti watalifungia sasa hivi kwa KUIUMBUA serikali ya Wadhaifu.

CHEZEA DHAIFU WEYE.....
 
FDR.Jr

Wewe umepitwa na wakati UDSM ilikuwa zamani enzi tulizosoma za Mwalimu. Kigezo katika ajira kama ni graduate anatakiwa iwe sawa lakini si kuangalia ametoka chuo gani.Vyuo vikuu vingi iwe UDSM,TUMAINI na vinginevyo graduate wengi siku hizi wanachakachua kwenye mtihani ili kupata GPA nzuri.

Unakuta mtu ni graduate ana GPA nzuri ila uwezo hata wa kujieleza na kuongea Kiingereza sahihi ni wa kubahatisha pia hata kufundishika kwenye kazi wanapoajiriwa mara ya kwanza inakuwa ngumu sana.
 
Kama ndio Hivyo basi Watende Haki na Mungu atakuwa Upande Wao!! Ila kwa issue ya kuwa na Majaji wasiokuwa na hata Vyeti vya elimu Hiyo sasa ni soo!!

Kamwe hawawezi tenda haki hao, wengine tunawajua toka wakiwa chini maofisini kwao ni watu ambao hawakuwa wasafi ktk kutimiza wajibu wao achilia mbali uzoefu na elimu duni anayoongea Lissu, nikiangalia kwa macho ya makengeza hawa wametayarishwa mahususi kwa kesi kama ile ya Lema Arusha, Kesi za Ramadhani,Kova na Ulimboka, Yona na Mramba na muhimu zaidi kesi za uchaguzi 2015, majaji hao ni shield ya serikali mambo yanapokuwa magumu, angalia siku hizi serikali inavyokuwa ya kwanza kukimbilia Mahakamani utafikiri iko Olympic 2012? Madaktari...Mahakamani, Walimu ..Mahakamani

Ona kesi ya Dr Ulimboka walivyoifanyia timing Bungeni isiongelewe kwa kutengeneza comedy halafu chap chap ikakimbilia mahakamani, Akina Mnyika wakitaka Bunge liongelee, Lukuvi anapinga kwa sababu Kesi ipo Mahakamani, na Bi Kiroboto na Ndugai wanaunga mkono harakaharaka kuisevu serikali kutimiza malengo ya aliyewaweka hapo,

Hivyo ukiangalia kwa undani JK ndie anaeoongoza na kusimamia mihimili yote mitatu,..Mahakama, Bunge na Serikali
 
huyo ndungai na mwanasheria mkuu na wengine wote waliomponda tundu,kweli wanatumia nywele zao kuwaza,espacially mwanasheria mkuu,yeye si anajua huu uozo uliooneshwa na tundu,ninawasiwasi na usomi wake huyo kilaza.au alijua tundu hatopata information????
AIBU KWA TAIFA.Hata rusiojua sheria inabidi tuanze kufatilia.
 
uko sahihi kaka,gpa za tumaini kimeo,nimesoma nao law skul,wengi wanababaisha tu.

Lengo si kukandia chuo chochote.Wote ni Watanzania na tunajua mfumo wa elimu wa nchi yetu.Kama mwanafunzi anamaliza darasa la saba na unaambiwa kafaulu mtihani na mwanafunzi huyohuyo hajui kusoma wala kuandika wewe kwa mawazo yako unafikiriaje.Elimu ya Tanzania kwa sasa wanafunzi wamekuwa wadanganyifu kwenye mitihani kuanzia primary,sekondary hadi vyuoni hakuna chuo kisichokuwa na graduate wababaishaji iwe UDSM,TUMAINI na vyinginevyo japo kuna wachache wema ambao hawajui maana ya DESA wao chuoni kazi moja tu shule na Sala
 
majaji wa sasa wanapewa kwa kujuana na kama fadhila pia.
wapo waliopewa hawajui hata mlango wa mahakama na hawajui hata kuandika coram ya file la mahakama
hawajui hata vile vifupisho vya kesi ktk faili kama ARONBB, Maana yake accused released on bail bond
au CA//CASE ADJOURNED , hajui hata procedure za hearing of cases nani aanze nani aongee tunasema EXAMINATION IN Chief CROSS EXAMINATION NA RE/EXAMINATION sasa huyu unategemea atoe hukumu lini?
majaji walau wapewe state attorneys na mahakimu wenye sifa ambao siku zote wako mahakamani na sii vinginevyo
Yuko mama mmoja alitoa hukumu ya ajabu katika masuala ya ardhi sijui kama rufaa imekuwaje
na kuwe na tume maalumu ya kusaili majaji ikiongozwa na wabunge.
Lissu ni jembe anawajua majaji hao kwani anaingia mahakamani.
na pia niulize katika kamati ya maadili iliomhoji jana alikuwepo mwanasheria?
 
Ndugu zangu, tafadhali sana someni Gazeti Jamhuri la leo, kuna habari na orodha ya majaji vihiyo na wala rushwa. KUna jaji mmoja wa Mahakama ya Rufaa ambaye hana digrii; na sasa anasoma Chuo Kikuu Huria. tAFUTENI GAZETI HILO HARAKA MAANA LIMEANDIKA KURASA NNE!!!!
 
Kumbe Tundu Lissu alitukanwa na kutishiwa bure sababu tu ya ukweli wake na uchungu wa Taifa hili.
 
hao ndio wanaodharilisha muhimili huu wa tatu kwa kutoa hukumu zisizokuwa na ubobevu wa kimantiki kisheria kama tulivyoona juzi ktk mgogoro wa madaktari na walimu.katiba katiba tuondolee mamlaka ya rais kwa kutuchagulia vilaza kama hawa!!!
 
wewe umepitwa na wakati udsm ilikuwa zamani enzi tulizosoma za mwalimu. Kigezo katika ajira kama ni graduate anatakiwa iwe sawa lakini si kuangalia ametoka chuo gani.vyuo vikuu vingi graduate wengi siku hizi wanachakachua kwenye mtihani ili kupata gpa nzuri .unakuta mtu ni graduate ana gpa nzuri ila uwezo hata wa kujieleza na kuongea kiingereza sahihi ni wa kubahatisha pia hata kufundishika kwenye kazi wanapoajiriwa mara ya kwanza inakuwa ngumu sana.
kamuulize ex-cj samatta kilichompata kwa kuajiri tumaini graduate wengi kwa kigezo cha gpa kati ya 2000-2006, ndio utaiona hoja yangu imelala wapi.....weredi wa taaluma kama sheria unapaswa uangaliwe kwa angle nyingi zaidi.....tunashukuru mahakama na hata pale kwa ag waliligundua hilo ingawa kwa kuchelewa na ndio maana intake ya 2005-06 mahakama walienda beyond gpa na kujikuta wamepata watu sahihi kwa kazi zao. Bado udsm wako vizuri zaidi ya vyuo vyote tanzania ktk sheria hilo halihitaji zama za mwalimu wala kikwete. All in all ninasali kada hii ya kulinda na kuhifadhi haki na sheria za umma itawaliwe na watu makini, wenye weledi,wanopenda kujifunza na waogopa mungu japo kwa asilimia fulani; si dhambi muhimili ukaendesha kampeni ya kuwachunguza wanafunzi wa kada hii vyuoni sasa, mafunzoni na kujua nani ni nani kabla ya kuajiri tu kwa sababu soko ni huru!!!hapo nchi itakuwa salama maana taifa lisilo na haki ni mfu.
 
Have you ever wondered why mkwereee has a penchant to appoint women to key positions especially in the judiciary!!
 
@fdrJunior upo sahihi sana vyuo hivi vya binafsi nashangaa sana karibu wanafunzi wao wote wanapomaliza wanapata GPA za first and second upper class na wachovu zaidi ndio wanapata second lower ,hii inatia ukakasi hasa kwenye taasisi zenye kukimbilia kuajiri wahitimu wenye GPA KUBWA KUMBE NI MAGALASA.Mfano wakati na hakiki vyeti vya watumishi waliomaliza masomo ili wapandishwe madaraja ofsiin kwangu WAHITIMU WA SAUT walikuwa na First and second Upper class na ukiwaona ni wachovu kabisa in skills,understanding and exposure.Nilipomaliza mie UDSM vichwa ni vingi lakini GPA inakuwa regulated sana.Pass Grade ya UDSM ni sawa na First class ya Tumaini na SAUT na hakuna ubishi wowote.
Katika Utafiti na kuuliza wahitimu wa UDSM law school wengi hawataki kazi za Uhakimu na kama akienda ni muda mfupi anafanya kazi hizo na baadae anakwenda Chamber-Advocate kitu ambacho ni tofauti sana na wahitimu wa vyuo vingine kama TUMAINI,MZUMBE,SAUTambao wanalilia kazi za uhakimu amabo ni ofisi za serikali na baada ya muda ndio hao wanakuwa promoted kuwa Majaji na maafisa wa idara za mahakama wakati ni Vilaza wa kutupwa.
 
kwanza nawapongeza kwa dhati ya moyo wangu wananchi wote wa Singada Mashariki kumpeleka mtu jembe kama Comrade Kamanda Lissu Bungeni na kupata fursa nzuri na ya uhakika kutupa sisi wananchi data zenye akili na utafiti! Pili nawaomba Watz wote jamani tusipeleke watu Bungeni kwa sababu anatujengea barabara kwa hela zake kutoka mfukoni, tupeleke watu wenye elimu, wanao jiamini na wanye kudhubutu. Mhe. Lissu nimesoma makala zake toka long time hasa katika sector ya madini, ni mtu asiye na ubabaishaji katika tafiti zake, nilienda kufanya utafiti wangu mdogo kwa ajili ya kadigrii kangu sehemu hapa bongo nikakuta yote aliyokuwa akiandiaka bwana Lissu ni ya kweli. natumainia mengi kutoka kwa bwana Lissu hasa nikifurahia kuwa mwana taaluma kama yake.
 
Kuna Mgonjwa wa muda mrefu aliteuliwa kuwa judge akiwa mgonjwa,aliapishwa akichechemea kwa ugonjwa akarudi kitandani,sina hakika kama amepona kupractice ujadge wake (Mtoto wa kigogo Malecela)
Akiwa mgonjwa kitandani kwa muda mrefu tu JK akamtangaza kuwa JUDGE,hata wakati wa kwenda kuapishwa alienda akiwa anachechemea kwa ugonjwa, sasa hapo kweli aliteuliwa awe mtendaji au afaidi marupurupu kama Muungwa Tundu Lissu alivyonena ?
 
kamuulize ex-cj samatta kilichompata kwa kuajiri tumaini graduate wengi kwa kigezo cha gpa kati ya 2000-2006, ndio utaiona hoja yangu imelala wapi.....weredi wa taaluma kama sheria unapaswa uangaliwe kwa angle nyingi zaidi.....tunashukuru mahakama na hata pale kwa ag waliligundua hilo ingawa kwa kuchelewa na ndio maana intake ya 2005-06 mahakama walienda beyond gpa na kujikuta wamepata watu sahihi kwa kazi zao. Bado udsm wako vizuri zaidi ya vyuo vyote tanzania ktk sheria hilo halihitaji zama za mwalimu wala kikwete. All in all ninasali kada hii ya kulinda na kuhifadhi haki na sheria za umma itawaliwe na watu makini, wenye weledi,wanopenda kujifunza na waogopa mungu japo kwa asilimia fulani; si dhambi muhimili ukaendesha kampeni ya kuwachunguza wanafunzi wa kada hii vyuoni sasa, mafunzoni na kujua nani ni nani kabla ya kuajiri tu kwa sababu soko ni huru!!!hapo nchi itakuwa salama maana taifa lisilo na haki ni mfu.


Hapa naunga mkono
 
Kwanza nashangaa hadi muda huu uchambuzi wa majaji vihiyo katika ushahidi wake aliotoa kamati ya maadili ya Bunge haupo hapa hadi muda huu. Ushahidi mzima unapatikana gazeti la leo la jamhuri ngoja niangalie uwezekano wa ku scan. Ukilisoma lote utakubaliana na mimi Tundu Lissu ni kati ya Watanzania wachache sana (rare breed) wanaothubutu kusema yale ambayo wengine hawathubutu. Hongera sana Lissu, mwanamapinduzi
 
Kwanza nashangaa hadi muda huu uchambuzi wa majaji vihiyo katika ushahidi wake aliotoa kamati ya maadili ya Bunge haupo hapa hadi muda huu. Ushahidi mzima unapatikana gazeti la leo la jamhuri ngoja niangalie uwezekano wa ku scan. Ukilisoma lote utakubaliana na mimi Tundu Lissu ni kati ya Watanzania wachache sana (rare breed) wanaothubutu kusema yale ambayo wengine hawathubutu. Hongera sana Lissu, mwanamapinduzi

Mkuu scan haraka leta hapa. Kweli CDM tukubali wana vichwa vikali vyenye kutambua wanachokisema. Hawabahatishi. Hongereni Wakuu.
 
Back
Top Bottom