Mkuu wangu unajua mnatia hasira sana mnapoanza kutafuta mchawi.. Matokeo ya kidato cha nne mwaka huu yanadhihirisha wazi ELIMU nchini ni mbovu.. Huwezi kupata asilimia 9 ya wanafunzi walioshinda mtihani halafu mkaendelea kutafuta sababu. Nimesema sana na nitaendelea kusema tena na tena kwamba MFUMO wa ELIMU nchini ni mbovu.. Hamuwezi kuiga mfumo wa Ulaya mkauleta hapa hata kidogo na tutaendelea kushindwa kwa sababu wanafunzi wetu wengi hukariri masom na majibu kwa sababu wanasoma tu lakini hawaelemiki.. Tunafundisha elimu feki kama tunavyotumia madawa na mali feki za kichina na India..Moja shule ambazo matokeo ya kidato cha nne yalikuwa mabaya sana ni Yusuf Makamba Secondary School iliyopo jijini Dar Es Salaam. Shule hii bado inaendelea kushikilia rekodi ya kuwa na matokeo mabaya ya kidato cha nne. Katika matokeo ya mwaka 2010, kati ya wanafunzi 452 waliofanya mitihani, wanafunzi 414 walipata Division 0. Wanafunzi waliobakia walipata kati ya Division I na IV na wengine.
Matokea ya mwaka huu yanatia aibu zaidi. Ikiwa imewekwa kwenye kundi la shule zenye watahiniwa 40 au zaidi, shule hii ya Yusuf Makamba imekuwa ya 1,481 kati ya shule 3,108 ikiwa na mwanafunzi mmoja tuu aliyepata Division I, saba Division II, kumi na nane Division III, 139 Division IV na 185 Division 0.
Kama alivyose Lissu kuwa Division IV ni failure kwa mahesabu ya haraka haraka haraka ni asimilia ngapi waliofaulu kwenye hii shule?