Tundu Lissu: Waliofaulu kidato cha nne 2011 ni asilimia 9.98

Mwanakili90

JF-Expert Member
Nov 24, 2010
1,568
245
"Maana halisi ya mtu aliyefaulu ni yule aliyepata daraja la kwanza mpaka la tatu, chini ya hapo amefeli. Kwa maana hii basi waliofaulu katika mtihani
wa kidato cha nne mwaka 2011 ni asilimia 9.98 pekee.

Wanafunzi 10 kati ya 100! Hao ndio waliofaulu kwa kiwango cha daraja la kwanza mpaka la tatu. Vijana wetu hawajifunzi tena. Hawa asilimia 90 wanaelekea wapi?"

Nawasilisha
 
Jamani pamoja na kwamba kuna matatizo ya kisekta watoto wetu hawasomi. Wameaminishwa/ kujiaminisha kuwa maisha ni rahisi sana. Vijana wanatumia muda wa kusoma vibaya sana. Cha kusikitisha wanapenda sana anasa za muda mfupi. Wamekuwa hedonists (Piga starehe kesho itajipa yenyewe). Hawatafaulu kwa staili hii na wanapaswa walaumiwe. Kwanza wafundishwe kuwa maisha ni magumu then wakitambua hilo watasoma.
 
Tatizo wanasoma maswali na majibu ya Nyambale Nyangwine wa CCM badala ya kusoma vitabu wapate uelewa wa kupambana na changamoto za kidunia. Mtu aliyesomea mtihani kwa miaka mi4 akifeli ujue kwishnei, either aolewe au ataishia kuwa kibaka tu. Kawambwa anaangalia tu... Au kwa kuwa Mwanaasha naye ana 4 then tubadili standards na 4 iwe ufaulu kumfuata FIRST STUDENT
 
Kaishiwa hoja huyo!siyo kila four ni zero,manake kuna div four nyingi ambazo zinaweza kwenda A-level.Kwa mfano mtu mwenye C-3 na D-6 nae hyu utasema amefeli.
Acheni kusifia kila ***** anaongea Lissu.
 
Kama ni vijana hawasomi, basi sisi wazazi na walezi ndio wenye shida! Ili kuwaje sisi tujione kuwa tulikuwa tunasoma (kwa mujibu wa andishi lako) lakini wanetu hawasomi? Mimi naamini tofauti na unavyoamini. Kuna tatizo tena kubwa tu. Miaka ya 1990 kurudi nyuma, shule walizosoma watoto wa viongozi ndiko waliikosoma watoto wa walalahoi, leo je? Ni Tanzania hii hii.

Kulikuwa na vyuo vingi na shule nyingi za kati, leo vingi vimegeuzwa vyuo vikuu sio? Tabaka la kati la watenda kazi watafundishwa wapi? Sio ajabu miaka 5 ijayo mainjinia wakawa ndio hao hao "fore men" na "washika mwiko vile. Tafakari!

Tanzania uifaidi, uwe mwanasiasa mtawala!
 
Kaishiwa hoja huyo!siyo kila four ni zero,manake kuna div four nyingi ambazo zinaweza kwenda A-level.Kwa mfano mtu mwenye C-3 na D-6 nae hyu utasema amefeli.
Acheni kusifia kila ***** anaongea Lissu.

We unafikiri wanafunzi wote wanasoma kombi mchanganyiko(art+sayansi) kwa pamoja?

Wengi wanasoma masomo 7 kwa mtiani wa form 4.
Sasa sijajua unataka kuzungumza nini.
 
jana nilikuwa na waalimu mahali.nikaleta hoja ya matokeo,mmoja akasema hiyo ni trela bado picha,tunataka matokeo yajao pasiwe na one ata moja.tuone sisi na madaktari nani? Nani zaidi.mgomo huu baridi unaua taifa
 
Tatizo wanasoma maswali na majibu ya Nyambale Nyangwine wa CCM badala ya kusoma vitabu wapate uelewa wa kupambana na changamoto za kidunia. Mtu aliyesomea mtihani kwa miaka mi4 akifeli ujue kwishnei, either aolewe au ataishia kuwa kibaka tu. Kawambwa anaangalia tu... Au kwa kuwa Mwanaasha naye ana 4 then tubadili standards na 4 iwe ufaulu kumfuata FIRST STUDENT

Kwa kweli huu mtindo wa kisasa wa kusoma maswali mimi siuelewi na siuungi mkono. Siamini kama mtu anaweza kupata ulewewa wa kina wa mambo mbalimbali kwa kusoma maswali na majibu ya mitihani. Kwa bahati mbaya siku hizi watoto wa shule wamezoezwa kusoma hivi vijitabu na wanadhani wanaelewa.
 
Pa1 na ugamba na ukakasi alionao EL aliwahi kusema vijana wanaomaliza shule na kufeli namna hio ni bomu litalolipuka siku ikifika, mimi nasema litalipuka 2015 na litaangamiza kila aliekuwa kikwazo cha elimu yao kuwa duni na katika mazingira magumu kama yalivyo sasa.
 
Kwa hiyo walimu(hasa wa cheti), ambao wengi wamepata foo kati ya 26-28 inamaanisha ni felia na kwa hiyo hawapaswi kufundisha?
 
jana nilikuwa na waalimu mahali.nikaleta hoja ya matokeo,mmoja akasema hiyo ni trela bado picha,tunataka matokeo yajao pasiwe na one ata moja.tuone sisi na madaktari nani? Nani zaidi.mgomo huu baridi unaua taifa

Nina uhakika ni shule hiyo tu ndo haitakuwa na one. Kinachofanya matokeo yawe mabovu ni ****** wa kuondoa mchujo wa mtihani wa fomu twu, mivilaza mingi imekuwa inafika fomu foo wakati zamani ilikuwa inachujwa toka fomu twu. Na hii ndio sababu zero na foo zimeongezeka.
 
Back
Top Bottom