Candid Scope
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 11,890
- 6,899
Bunge la Tanzania linahusisha wabunge wa bara na wa visiwani wakati zaidi ya theluthi mbili ya yanayojadiliwa ni ya wabara. Hali kadhalika wa visiwani wanapotunga au kubadilisha vifungu vya katiba wabara hatuhusishwi kwa maana kwamba ni ya kwao lakini wao wanahusishwa yote yahusuyo muungano na yale yahusuyo wabara tu. Hapo haki haitendeki, kwani idadi ya wavisiwani inawezi ikaathiri maamuzi yanayowahusu wabara tu.Kwa nini wabunge wa visiwani wanapojadili bajeti wanashiriki hata iwahusuyo wabara.
Na kwa nini visiwani wawe na haki sana na wabara katika kupitisha katiba yenye mambo mengi yanayowahusu wabara na kuwepo machache tu ya Muungano? Alichosema Lisu kwamba wa visiwani ingefaa wahusishwe tu katika vipengele vya muungano ni uchochezi au ni kutufungua akili wengi ambao tumedanganywa miaka yote na wanasiasa viongozi wenye kujali maslahi binafsi kama viongozi badala ya maslahi ya wananchi wote wa pande zote mbili?