Tunampenda Deo Filikunjombe Ludewa (CCM)

FOE

Member
Sep 21, 2009
87
6
"SHEREHE za kusimikwa kwa Kamanda mpya wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UV-CC), Bw. Deo Filikunjombe zilitikisa mji wa Ludewa mkoani Iringa baada ya wana CCM kutoka kata zote 22 za wilaya hiyo kushiriki huku wakiwa na furaha kubwa. Shamrashamra hizo zilipambwa na wanaCCM waliokuwa wamevaa fulana zenye maandishi yanayosomeka ‘Tunampenda Deo Filikunjombe’, baadaye, Bw.Filikunjombe alikabidhi msaada wa gari la wagonjwa katika Kituo cha afya Manda kwani ilielezwa kuwa wagonjwa walikuwa wakipata shida kubwa kutokana na kukosa huduma hiyo."

Mwaka huu kazi ipo ndani na nje ya chama.

Ndio nani huyo mkuu? tupe wasifu wake ili tumpigie kura hiyo siku itakapofika.
 
Duh, jamaa anagombea ubunge?

Sina CV yake rasmi lakini alisoma Mass Communications (bachelor's degree) Makerere University Kampala na kumaliza mwaka 1999, baadae akajiunga na Wizara ya Mambo ya Ndani.

Jina kamili ni Deogratius Filikunjombe Haule. Labda kama wapo wawili
 
Mbona nasikia huyu hafai,
ana madeni mengi sana anadaiwa na nbc,
mpaka wanataka kumfilisi?
Hana nidhamu ya fedha na uchungu wa mali zake binafsi,
je maendeleo ya wananchi wake atakuwa na uchungu nayo kweli?
 
Tupeni data mnaomjua. Sisi wengine hatumjui kabisa. Tunasubiri tumjue ili tuelewe kama ni mtu safi kweli au walewale!
 
Hivi kuna watu bado wana matumaini na siasa za Tz? Kaaz kwelikweli endeleeni hivohivo kusubiria madafu yakomae, wakati mlipanda chelewa.
 
Wacha niseme kitu kimoja,

Kudaiwa na benki si dhambi.Kama ni mfanyabiashara si ajabu kudaiwa na Benki.Nidhamu ya fedha haipimwi kwa kuangalia unadaiwa kaisi gani na Benki

Pili,Huyu kijana kama ana uwezo wa kugombea na agombeee.Hebu tuone CV yake nzima tujue

Pia si yule aliyetamka kuwa hajaamua kugombea bado?Inaonekana huyu anacheza political games sasa,na anaweza kuwa na strategy nzuri ya kampeni.Anyway,ngoja muda ukifika tutajua ni mtu wa aina gani....
 
profile yake iko vip? haya mambo ya kubebana umeletwa na katibu wa chama na kuambizana mpeni kura zenu sasa yanaelekea kupitwa na wakati..
 
profile yake iko vip? haya mambo ya kubebana umeletwa na katibu wa chama na kuambizana mpeni kura zenu sasa yanaelekea kupitwa na wakati..

Unajua dada yangu haya masuala ya chama tawala,upinzani nk yananishangaza.Yaani tumezoea zima moto style ktk kutoa elimu ya uraia,yaani kipindi cha kampeni tu

Sasa hapa wananchi wakiambiwa hivi wanafanya vile vile bila kutafakari.Tafadhali wakuu mwenye CV nzima atuletee
 
Duh, jamaa anagombea ubunge?

Sina CV yake rasmi lakini alisoma Mass Communications (bachelor's degree) Makerere University Kampala na kumaliza mwaka 1999, baadae akajiunga na Wizara ya Mambo ya Ndani.

Jina kamili ni Deogratius Filikunjombe Haule. Labda kama wapo wawili

Duu yale yale..Kamaliza digrii mwaka 1999 anasimikwa ukamanda wa vijana.kazi kweli kweli.
 
Duu yale yale..Kamaliza digrii mwaka 1999 anasimikwa ukamanda wa vijana.kazi kweli kweli.

assume alimaliza degree akiwa na miaka 22.ila kwa kweli inabidi kuwe na msizitizo kipindi hiki cha uchaguzi,kuna Single moja maarufu iko hewani inaitwa ujana...hebu ufafanuzi utolewe coz it seems everbody wants to take advantage and try to forge the dancing style of this track!
 
Mkuu ninaifahamu vizuri Ludewa.Sio rahisi kwa yeye kuwa amemaliza digrii na miaka 22 kwa kuwa najua kule labda kama hakusomea huko..Darasa la kwanza kwa kipindi kile walikuwa wanaanza na umri wa miaka 8 na 9,unless kama yeye ni mrefu sana kwani ilikuwa ni lazima ujipime na mkono kwanza.Mimi siamini kama kweli atakuwa na umri wa ujana kwa mujibu wa sera ya taifa maendeleo ya vijana na hata katiba yao ya CCM
 
Duh, jamaa anagombea ubunge?

Sina CV yake rasmi lakini alisoma Mass Communications (bachelor's degree) Makerere University Kampala na kumaliza mwaka 1999, baadae akajiunga na Wizara ya Mambo ya Ndani.

Jina kamili ni Deogratius Filikunjombe Haule. Labda kama wapo wawili

EXACTLY!!!! Jamaa keshatangaza na mpinzani wake (Mbunge wa sasa) Prf. Benedict Mwalyosa analijua hilo. Kwa kifupi kwa hili tukio amemuacha mpinzania wake kwa mbali sana (apprx. 75% vs 25%). Bahati mbaya sana lile jimbo chama cha upinzani kwao ni mwiko kabisa. Ni kata moja tu ya Lupingu out of 22 ndio iliyowahi kupata walau diwani wa upinzani. Kwa hiyo ni kama yuko 55% mbunge.
 
Mimi sijajua huyu ni nani na why aje kujadiliwa na sisi wanaJF au ndio Kampeni wakuu wangu
 
  • Thanks
Reactions: Iza
Duu yale yale..Kamaliza digrii mwaka 1999 anasimikwa ukamanda wa vijana.kazi kweli kweli.

Kwa kweli sina shaka/tatizo na umri wake kuitwa kamanda wa vijana. Nahisi (nionavyo mimi) ukamanda wa vijana kwenye hiki chama hauna cut-off ya umri. Kwasababu hata Mr paul Kimiti mbunge wa Sumbawanga mjini bado ni kamanda wa vijana wilyaya ya Sumbawanga mjini (Sina hakika kama amestaafu mwaka huu). Wengi wetu tutakumbuka kijana mwenzetu Kingunge Ngombale Mwiru, alivyotumikia nafasi ya ukamanda wa vijana mpaka miaka ya hivi karibuni. Umri sio issue kabisa kule chamani!!!
 
Duh, jamaa anagombea ubunge?

Sina CV yake rasmi lakini alisoma Mass Communications (bachelor's degree) Makerere University Kampala na kumaliza mwaka 1999, baadae akajiunga na Wizara ya Mambo ya Ndani.

Jina kamili ni Deogratius Filikunjombe Haule. Labda kama wapo wawili

Injinia ulisoma MUK?
 
Mkuu ninaifahamu vizuri Ludewa.Sio rahisi kwa yeye kuwa amemaliza digrii na miaka 22 kwa kuwa najua kule labda kama hakusomea huko..Darasa la kwanza kwa kipindi kile walikuwa wanaanza na umri wa miaka 8 na 9,unless kama yeye ni mrefu sana kwani ilikuwa ni lazima ujipime na mkono kwanza.Mimi siamini kama kweli atakuwa na umri wa ujana kwa mujibu wa sera ya taifa maendeleo ya vijana na hata katiba yao ya CCM

Apart from that nasikia baada ya kuhitimu darasa la saba jamaa akapitia pre form one. Tutaona vijana wa kichina mwaka huu! hahahah
 
Back
Top Bottom