Tunampenda Deo Filikunjombe Ludewa (CCM)

Deo Filikunjombe anasomesha watoto yatima kule Ludewa kama anavyofanya sasa hivi Godbless Lema. Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni.
 
IMG_2909.JPG
 
Jimbo la Ludewa kabla ya uchaguzi wa juzi lilikuwa chini ya Pro. Mwalyosi kama mmbunge,
naweza kusema Deo kapata ubunge kwa njia ya rushwa kwa sababu miaka miwili kabla kabla ya uchaguzi alianza kuto misaada ya aina mbalimbali sehem na kwa watu tofauti tofauti katika jimbo na ni misaada ya gharama kubwa wakati ndugu zake wengi hawana uwezo kwa mfano mdogo wake Majuto, Amosi, Eliza wapo tu mtaani ameweza kumsaidia mdogo wake mmoja tu anaitwa Philipo ambaye kwa sasa ni lecturer Mkwawa.
nasema amepata kwa rushwa kwa sababu kama anamapenzi ya kusaidia angeaanza kuwasaidia wadogo zake kwanza na hata hali ya wazazi wake sio nzuri.
 
Hata nchi tajiri duniani zinazotoa misaada kwa nchi maskini huwezi kuamini kuona watu maskini na homeless katika nchi zao. Nilikuwa najiuliza swali kama lako kwa nini nchi kama marekani au UK kuna maskini na walalahoi wengi na homeless afadhali ya bongo.
Si rahisi kuwasaidia ndugu kiasi unachosema wewe. Na kutoa misaada kwa ndugu unavyofikiria ni kuwapumbaza, na hawatafunguaka akili namna ya kuhangaika na maisha.
Mimi binafsi hufungua mlango kumsaidia mtu anayeonyesha dalili ya kukuza ninachomsaidia, lakini wengine wanamaliza ulichompa na kesho wanakuja tena kukinga mkono.

Deo katoa msaada wa kusaidia watu wengi na wenye matatizo ya kweli, huo ni utume. Na mbunge wa aina hiyo ndiye wanayemtaka vijiji si wale vilaza tu.
 
IMG_2784.JPG


Halafu mnaona Chuma cha Liganga huko wilayani Ludewa ni nje nje tu hakuna kuhangaika kuingia chini ya mahandaki
 
Nakumbuka nilikutana naye huyu jamaa akiwa anaandaa ambulance ilikuitoa msaada jimboni mwake hapo alinipa business card yake ambayo ilisomeka kama ni Katibu wa UV-CCM.. Nilimuuliza mkuu unataka kugombea ubunge nini? alikataa kabisa alisema huu ni msaada tu natoa.. Kambukumbu zimekaa sawia nakumbuka ilikataliwa siku anaitoa hilo gari ya wagonjwa kwani ilioneka ni kama rushwa kwani alikuwa na mpango wa kuchukuwa form za kugombea kupitishwa na CCM .

Kwani nani asiyejua CCM Bila kutoa rushwa hupati ubunge tena ukiangalia hali za watu wa Ludewa utashangaa.

Hapa mjini anabiashara gani? Anaoneka nimjanjamjanja sana.
 
Wacha niseme kitu kimoja,

Kudaiwa na benki si dhambi.Kama ni mfanyabiashara si ajabu kudaiwa na Benki.Nidhamu ya fedha haipimwi kwa kuangalia unadaiwa kaisi gani na Benki

Pili,Huyu kijana kama ana uwezo wa kugombea na agombeee.Hebu tuone CV yake nzima tujue

Pia si yule aliyetamka kuwa hajaamua kugombea bado?Inaonekana huyu anacheza political games sasa,na anaweza kuwa na strategy nzuri ya kampeni.Anyway,ngoja muda ukifika tutajua ni mtu wa aina gani....

Wajamamiiiiiiiii, duh data bado hatuna, Huyu jamaa ni mbuge wa CCM Ludewa na ni Makamu Mwenyekiti wa kamati ya zito Babwe
 
Siyo kweli kuwa huyu msheshimiwa hajali familia yake. Anaijali sana na kwa kuanzia amejenga nyumba ya familia ludewa nadhani ni nzuri sana, ametaka kumnunulia gari babake, mzee kakataa, pikipiki kakataa. Wadogo zake wanasaidiwa sana lakini ludewa hali ya vumbi linafanya watu wengine nje waonekane kama vile hawana msaada. Na bado anaendelea na mipango ya kuwasomesha ndugu zake lakini alisema ataanza kwanza na watu wasio na msaada kabisa
 
Hana historia ya ajabu, ni mjasirial mali ambaye anapenda sana kufanya kazi kwa malengo na jitihada na bidii. Huwa anafanya biashara kama msomi. Wakati mwingine anafanya biashara za kimataifa.
 
Hivi kampeni zimeanza kwa uchaguzi wa lini?. Badala ya kumtaka afanye kazi/atekeleze ahadi wapambe mnatumwa kumsifu!. Sishangai sana, ilimradi mkono uende kinywani.
 
huyo dogo bado ana mengi sana ya kujifunza, sio lazima hata kama uko ccm ufuate mfumo wa siasa za kijinga...
 
Hana historia ya ajabu, ni mjasirial mali ambaye anapenda sana kufanya kazi kwa malengo na jitihada na bidii. Huwa anafanya biashara kama msomi. Wakati mwingine anafanya biashara za kimataifa.

Anbahati sana huyu. Baadaye tusije ambiwa ni RA&co
 
masahihisho
Mzee mbunge wa iringa si mkuu wa mkoa wa arusha bali aliyekuwa mbunge wa ccm iringa mjini monica mbega ni mkuu wa mkoa wa kilimanjaro. hii ni sehem ukweli wenye utafiti si brabra
Monica Mbega alikuwa mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro si mkuu tena kwasasa na nafasi yake inakaimiwa na mkuu wa mkoa wa Tanga.
 
Kwa vyovyote zito ni mzoefu sana kuliko huyo deo, Zito ni mwanasiasa makini sana na ukimtuatilia sana utagundua kuwa zito anaakili sana na nimzalendo. Nimemfuatilia sana zito na siasa zake ni mzuri nimemkubali.

Nimemfuatilia sana pia huyu dogo baada ya kugundua chama changu cd hakina mgombea ludewa na kugundua huyu kijana kumbe alikuwa anagumbea kwa mara ya pili, na alianza mapema sana kujiandaa.

Anashomesha watoto wengi sana sekondari, takribani 500 lkn ada ni elfu (20 day) na elfu ishirini (boarding) kwa biashara zake anaweza. Alisaidia karibu kitu fulani kila kijiji, vitu kama vile, computers, kuezeka mashule, misaada makanisani na misikitini.

Kwa vyeo hivi alivyonavyo hamhitaji zito kabwe au yeyete ambebeL-

1. Ni katibu wa uchumi na fedha ccm wilaya Ludewa
2. Ni kamanda vijana wilaya Ludewa
3. Mjumbe wa kamati siasa mkoa Iringa (naafasi ya Mungai) Niligundua alimshinda mungai katika uchaguzi
4. Ni mlezi wa chipukizi Taifa kamati nadhani watu 5 mwenye taarifa anijuze. Yumo na kigoda, kinana nk
5. Sasa hivi ni mjumbe kamati fedha mashirika ya umma
6. Makamu mwenyekiti kamati tajwa hapo juu
7. Sito shangaa akichaguliwa mbunge bunge la afrika

Nilikutana naye Australia alikuja kututembelea, anaonesha kuipenda nchi yake, anaongea kiingereza kizuri sana na kiswahili fasaha.

Hautakiwi kuwa prof. kuona maendeleo endelevu na mipango ya muda mrefu. Naweza nisimpende yeye, lakini ninapenda hiyo profile jinsi anavyoipika. Tumshauri tu asimezwe na makundi kwani kweli hayatamsaidia.

Sio yeye tu, hata kama kuna kijana mwingine wa hulka yake mleteni jamvini ili tumjadili na kumuungoza kwa namna tofauti. Ukiufukia ukweli hapa, utaibukia pale.


4.
 
Nakumbuka nilikutana naye huyu jamaa akiwa anaandaa ambulance ilikuitoa msaada jimboni mwake hapo alinipa business card yake ambayo ilisomeka kama ni Katibu wa UV-CCM.. Nilimuuliza mkuu unataka kugombea ubunge nini? alikataa kabisa alisema huu ni msaada tu natoa.. Kambukumbu zimekaa sawia nakumbuka ilikataliwa siku anaitoa hilo gari ya wagonjwa kwani ilioneka ni kama rushwa kwani alikuwa na mpango wa kuchukuwa form za kugombea kupitishwa na CCM .

Kwani nani asiyejua CCM Bila kutoa rushwa hupati ubunge tena ukiangalia hali za watu wa Ludewa utashangaa.

Hapa mjini anabiashara gani? Anaoneka nimjanjamjanja sana.

Alipogombea ubunge awali mmoja wa karibu na kampeni huko kwao kaniuma sikio kulikuwa na wengi wakiwemo Mwalyosi, Filikunjombe, Mapwayula na wengine, lakini Mwalyosi aliwazidi kete ili kumpiku profesa.
Baada ya uchaguzi wa 2005 Deo na wengine wakarudi jimboni kujipanga upya pamoja na wale wengine walioangukia pua. Kati yao Deo Filikunjombe alionekana kujenga mtandao mzuri na rasilimali za kuonyesha uwezo wake wa kuwashawishi wapiga kura.

Licha kujenga mtandao huo pia jina lake linasikika vyema kutokana na kutoka ukoo wa kichifu wa mzee Filikunjombe. Ila ni kijana anahitaji bado kujenga jina zuri na kuacha jazba kwani katika siasa yahitaji uvumilivu na kuwa mstahimilivu.
 
Ni kweli the guy is smart. Ni mjanja toka tukiwa tunasoma nae kule Makerere. Yeye aliweza kusoma, jioni na mchana kufanya kazi za uandishi wa habari. he is social and hard working.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom