Mchokoo
JF-Expert Member
- Jul 28, 2015
- 1,179
- 1,579
Kwa moyo wa dhati najivunia hiki ulichokifanya ndugu yangu. Ni mwanzo mzuri kuliko awali ya magari mengi yaliyopo sasa duniani
Ninachokiomba kwa watanzania wenzangu; ni tumuunge mkono mwenzetu ili afanikishe maono yake.
Gari la Masoud siyo kwa ajili yake binafsi. Ni kwa faida ya taifa letu na vizazi vijavyo. Chonde serikali na wizara husika, msisubiri maziwa, mkasahau kumlisha ng'ombe.
Nasikitika kuwa hiki alichofanya kiumbe huyu, hakilingani kabisa na mapokeo tuliyokipatia kitaifa! Kama tuliweza kuzipokea ndege zilizotengenezwa katika nchi za ng'ambo kwa mafuriko;
Tunashindwaje kulipokea jambo hili kubwa alilofanya mwenzetu?
Asante Masoud, kutuondolea unyonge wa kujiona hatuwezi kufanya mambo makubwa.
Mwenyezi Mungu akupe maisha marefu, ili vipaji alivyokupatia viubariki Ulimwengu.