Tumuunge mkono mwanasayansi Masoud Kipanya

Mchokoo

JF-Expert Member
Jul 28, 2015
1,179
1,579
Kwa moyo wa dhati najivunia hiki ulichokifanya ndugu yangu. Ni mwanzo mzuri kuliko awali ya magari mengi yaliyopo sasa duniani

Ninachokiomba kwa watanzania wenzangu; ni tumuunge mkono mwenzetu ili afanikishe maono yake.

Gari la Masoud siyo kwa ajili yake binafsi. Ni kwa faida ya taifa letu na vizazi vijavyo. Chonde serikali na wizara husika, msisubiri maziwa, mkasahau kumlisha ng'ombe.

Nasikitika kuwa hiki alichofanya kiumbe huyu, hakilingani kabisa na mapokeo tuliyokipatia kitaifa! Kama tuliweza kuzipokea ndege zilizotengenezwa katika nchi za ng'ambo kwa mafuriko;

Tunashindwaje kulipokea jambo hili kubwa alilofanya mwenzetu?

Asante Masoud, kutuondolea unyonge wa kujiona hatuwezi kufanya mambo makubwa.

Mwenyezi Mungu akupe maisha marefu, ili vipaji alivyokupatia viubariki Ulimwengu.
 
Aungwe mkono kivipi sasa
Si aanze kuuza apate pesa

Kama katengeza kitu kisicho na soko kapoteza pesa yake halina tofauti na mdoli
 
Yeye auze tu apate pesa. Alichokifanya ni sawa na wale ambao huwa wanatengeneza ndege alafu wananyimwa ushirikiano, wapo wengi sana humu Tanzania. Vilevile huwa kuna sababu za msingi za kuwanyima ushirikiano, jamaa ame copy idea ya watu.
 
Sijui kwann ila mbona kafanya jambo la kawaida sanaa......kwani hamjai ona pikipiki za kucharge (zipo kibao hadi toyo za kucharge zipo) au kwa vile kafanya gari.

Nenda arusha kuna watu wanaunga mabody ya magari ya kitalii utashangaa na roho yako hata hapa dar wapo kibao. Very professional work, vile hawajaweka engine ya umeme...(which is something very normal)

Ujue mtu mwenye jina akifanya jambo la
Kawaida watu wataanza kustaajabu na kuona its a big deal.

Sisemi hajafanya jambo la maana ila ni la kawaida mnooo. Binafsi ule muundo na body sijauelewa.

THINK BIG
 
Sikujua kama una akili ndogo kiasi hicho. Hujui kama magari huwa yanatengenezwa kwanza, halafu namba huja baadaye! Halafu, hata bajaji hatuiti ni doli, sembuse gari zuri kama lile? Acha wivu na roho mbaya.

Nimuonee husda kwa kipi kwa hilo doli alilotengeneza ambalo hata namba ya Gari ya kutoka TRA halijapata

Lingekuwa barabarani hapo sawa
 
Kwa moyo wa dhati najivunia hiki ulichokifanya ndugu yangu. Ni mwanzo mzuri kuliko awali ya magari mengi yaliyopo sasa duniani

Ninachokiomba kwa watanzania wenzangu; ni tumuunge mkono mwenzetu ili afanikishe maono yake.

Gari la Masoud siyo kwa ajili yake binafsi. Ni kwa faida ya taifa letu na vizazi vijavyo. Chonde serikali na wizara husika, msisubiri maziwa, mkasahau kumlisha ng'ombe.

Nasikitika kuwa hiki alichofanya kiumbe huyu, hakilingani kabisa na mapokeo tuliyokipatia kitaifa! Kama tuliweza kuzipokea ndege zilizotengenezwa katika nchi za ng'ambo kwa mafuriko;

Tunashindwaje kulipokea jambo hili kubwa alilofanya mwenzetu?

Asante Masoud, kutuondolea unyonge wa kujiona hatuwezi kufanya mambo makubwa.

Mwenyezi Mungu akupe maisha marefu, ili vipaji alivyokupatia viubariki Ulimwengu.
😍
 
Tupia picha ya hilo gari, pls!
 
Back
Top Bottom