Tumuenzi Kikwete Historia isije Ikamsahau

View attachment 38509
Baada ya kutafakari sana na kutumia muda mwingi kuwaza jinsi gani kama ningepewa nafasi ya kumuenzi Rais Kikwete ningefanya nini nimejikuta na mapendekezo mengi sana yaliyonijia kwa ghafla kichwani kama maporomoko ya maji kwenye magema ya Udzungwa. Kama ukungu ukiinuka na kuachana na manyasi kwenye kona za Mlima Kilimanjaro alfajiri na mapema ndivyo fikra zangu zilivyofunguka na kutambua kuwa Rais Kikwete hajaenziwa vya kutosha kutoka na mchango wake mkubwa katika maisha, historia, hali, na hatma ya watu wetu. Hivyo mapendekezo yangu nimeyatoa kwa moyo wa furaha uliojaa tabasamu, kicheko na matumaini kuwa yatakubaliwa na wale wote wenye kuitakia mema nchi yetu ambao hawapendi kuendeleza chuki binafsi, udini, ukabila na ubaguzi wa aina yoyote.

Ni mapendekezo ya kiungwana ya kumuenzi Rais wetu wa nne.

Pale Ikulu pabadilishwe na kuitwa Kikwete House
Barabara ya Morogoro iitwe Jakaya Highway
Chuo Kikuu cha Dar-es-Salaam ambapo alisomea kibadilishwe kwa heshima yake na mchango wake katika uchumi na kuitwa Jakaya Kikwete Dar-es-Salaam University (tunaweza kuongeza "national" kwenye hiyo title)
Jengo jipya la sanaa lililojengwa na Wachina liitwe Jakaya Kikwete Center for Performing Arts
Chuo Kipya cha Kijeshi kule Kigamboni kiitwe Lt. Col. J. M. Kikwete War College
Jeshi la Wananchi ambalo alilitumikia kwa umakini na umahiri limpandishe cheo ili we Gen. Jakaya Kikwete ili kuonesha mchango wake wa jinsi alivyoliendeleza jeshi hilo hadi kukamata maharamia nane.
Kwa vile nimekuwa nikipigia sana kampeni ya kujengwa kwa hospitali ya taifa ya watoto naamini kama atalifanyia kazi wazo hili hospitali hiyo iitwe Dr. Jakaya Kikwete National Children's Hospital kwa masharti kwamba kama itatokea ikajengwa wakati hayupo basi tunaweza kuongeza neno "Memorial" humo katikati.
Kutokana na kuendelesha mahusiano yake ya karibu na viongozi mbalimbali wa dini napendekeza viongozi wa Kiislamu waangalie ni Msikiti gani maarufu nchini upewe hadhi ya Kikwete Mosque; Viongozi wa Makanisa wanaweza nao - kutokana na mambo mbalimbali ambayo amewasaidia - kutafuta mahali ambapo pangeweza kupewa jina la Jakaya Kikwete National Chapel. Kama ni kubwa sana tunaweza kuliita Cathedral! Kama ni Wakatoliki na jengo hilo lina hadhi ya Kipapa tunaweza kuita "Kikwete Basilica of Our Lady of Fatima"
Daraja linalotarajiwa kujengwa la Kigamboni kwa ushirikiano mkubwa wa serikali na NSSF laweza kupewa jina la Kikwete International Bridge (sasa hii 'international' ni kwa sababu tu watu watakuwa wanavuka kwenda ng'ambo kupitia daraja hilo).
Nimekumbuka kuwa ile Maktaba ya Taifa kwa kweli haina hadhi ya kitaifa kwani haina jina la kiongozi wa kitaifa. Hivyo naipendekeza - sidhani kama kuna watu watanipinga - iitwe Dr. Kikwete National Library. Hii ni kutokana na mchango wake wa kuendeleza usomaji nchini na huduma ya library na hasa kutokana na mipango ya miaka kumi iliyopita ya ujenzi wa maktaba mpya jijini Dar kukidhi mahitaji ya watoto wetu ambayo inatarajiwa kuanza kutekelezwa mwishoni mwa utawala wa Rais Kikwete

Ukiondoa maeneo hayo nadhani wapo watu wengine wanaoweza kufikiria maeneo, vitu na hata majengo mbalimbali ambayo yatalibeba jina la Rais Kikwete. Na licha ya hivyo wakati umefika wa kuanza kuweka picha zake sehemu mbalimbali nchini. Picha kubwa zinaweza kuanza kupambwa kuanzia uwanja wa ndege na maeneo yote ya kuingilia mijini. Kwa vile ofisi zote tayari zinapambwa na picha ya rais ndani nafikiri hii si heshima nzuri kwa maana si watu wote wanaingia maofisini humo. Napendekeza picha kubwa za rangi (zinaweza kuwa zile za kutabasamu au akimpa mtoto peremende) ziwekwe maeneo ya wazi ya nje ili ionekane.

Sasa tukiwa tunafanya hivyo napendekeza kuwa kumtaja kwa jina la Dr. Kikwete kwa kweli hakuendani hasa na hisia za Watanzania wengi. Binafsi kuanzia leo hii nitamtambulisha kama Kiongozi Mpendwa Dr. Sasa hili ni muhimu sana kusema hivi kwa sababu isije ikaonekana anachukiwa. Kwa kiingereza tunaweza kumuiwa "Dear Leader" au "Beloved Leader" ili kuonesha mapenzi yetu kwa uongozi wake mahiri na jinsi gani amegusa mioyo ya watu wetu na kuwafanya wainuke kujiletea maendeleo.

Kama unakubaliana na mapendekezo yangu nawe unaweza kupendekeza ni maeneo au vitu gani muhimu vibebe jina la Rais Mpendwa Kikwete? Sasa ni lazima viwe ni vitu vya heshima visiwe vitu vya kejeli ili tusionekane kabisa tunamdharau. Sasa kwa vile haya ni maamuzi ya wananchi wenyewe hayahitaji kibali kwani kama jina la mahali likishazoeleka sana ndivyo linavyokuwa na baadaye kutambulika hivyo.

Kwani watz mna maana???
nikikumbuka mlivyokuwa mnamshangilia nyerere na kumkashifu Mwinyi kipindi cha utawala wa awamu ya pili!!! na nikikumbuka jinsi mlivyokuwa mnamshangilia MWINY na kumtukana MKAPA kipindi cha utawala awamu ya tatu na mnavyoMSHANGILIA MKAPA na kumkashifu KIKWETWE kwenye awamu hii ya nne. napata uhakika mmoja tuu.
nao ni huu:-------------
1. watanzania hawajui wanataka na wanahitaji nini
2. hawajui nani mzuri kwao na nani ni msanii na adui kwao
3.wako tayari na watakubali kutawaliwa hata na mwendawazimu kama tu atakuwa na maneno na ahadi tamutamu
4. hawatumii vichwa vyao kufikiria bali mioyo yao(mapenzi yao kwa mtu ndo hupelekea kumkubali na kumuamini)
5 ni wadini- very sensitive on this
6. ni waroho, wala rushwa, sio wazalendo,waongo, wapumbavu, wanaedekeza ushabiki
Na cha kusikitisha zaidi....... hata MZEE MWANAKIJIJI NI Mmoja kati ya MAZUZU.
UKITAKA KUJUA WENGI WENU NI MAZUZU,,, SUBIRI TAREHE 17/10/2011 hukumu yakesi ya GODBLESS LEMA pale arusha mjini ndio utakapojua ukombozi bado uko mbali na hauwezi kuletwa na kundi dogo la CRUSADERS and pathetc tribal hardcore. if you dont wana be gratefull to himnyamaza tuu kaka kuliko kutumia nguvu nyingi.
.
 
Chuo Kikuu cha Dar-es-Salaam ambapo alisomea kibadilishwe kwa heshima yake na mchango wake katika uchumi na kuitwa Jakaya Kikwete Dar-es-Salaam University (tunaweza kuongeza "national" kwenye hiyo title)

Mkuu tukimwongezea na Jakaya Kikwete International University of Dodoma (JKIUD), tutakuwa tumemuenzi vyema. Nimependekeza international, kwa vile pale kuna ufundishaji wa lugha nyingi za kimataifa kama kichina, kiarabu na kikorea.....
 
na kwa kuheshimu mchango wake hasa kwenye michezo tuwaite taifsa stars = kikwete wanderers

Unajua hii nadhani imechelewa kwa kweli. Jinsi alivyotuletea kocha toka Brazil na kufanya vizuri sana kwa timu hiyo baada ya kuifunga Togo kwa uhakika ni muhimu kutambua mchango wake. Sijui kwanini hakuna viongozi wa michezo waliofikiria hili. Natumaini hili baraza jipya la michezo lililundwa na Nchimbi majuzi litafanya kazi yake.

Timu ya Olympic iitwaje?

Wazee nafikiri wameiita JK Boys or JK11...
 
Ili kumuenzi vizuri ningependelea UDSM waanzishe course itakayoitwa Kikwete Tourism Leadership na ile Ndege tulioambiwa kuwa tutakula nyasi apewe kama tunzo ya Kuongoza Nchi Vizuri na Upambanaji wake katika vita ya rushwa
 
Bila ya Kusahau shirika letu la Usafirishaji, UDA liitwe Kikwete Community Transportation ( KCT )
 
Sikujua kwamba Mzee Mwanakijiji ni MNAFIKI kiasi hiki. Acha utoto mzee, you are too matured to write pumbaz like these
Mkuu nilipojiunga na JF mwanzoni nilipata shida hii hii espeacially kuhusiana na threads za huyu jamaa.Ukikua utaacha...I got confused the same way.Sikulaumu however.Utajifunza mwenyewe.Kipindi kile walikuwepo kina Baba H location: magogoni, na Kakindo Master.Bongolander yupo amejitolea kukupa mwangaza kidogo.The rest is up to you.
 
Magereza je hazifai kuitwa kwa ukumbusho, vipi bahari ilikoanguka meli, namna gani jina zuri la tume ya uchaguzi je, na sehemu za starehe je, bongo flava isiitwe kwa jina la jk beats au flava?
 
Hivi wewe jamaa utaacha lini kuandika pumba? Unashindwa hata na Kubenea kwa kujenga hoja ingawa mpaka sasa hajui aliyemmwagia tindikali. Jitahidi kupunguza porojo mkuu!

Unamtindio wa ubongo
 
Kitufe cha Thanks naona kimerudi,haya,tumuenzi.
Licha ya kurudi, naona tumeanza muhula mpya wa thanks na likes kwani naona zilizokuwepo zote hazionekani. By the way mtu lazima aenziwe kulingana mchango wake. Najua ameahidi mambo mengi, mi naona chochote kinakachotekelezwa katika muda huu kimuenzi., kama meli mpya ziwa Victoria, Uwanja wa denge Kigoma, nk
 
kwanini hata nchi hii isiitwe the republic of JAKATANZANIA kuimalisha muungano zaidi!
 
"Hizo shule za kata nazo hazijatendewa haki..zipewe haki yake labda ziitwe "DR. JAKAYA KIKWETE CENTERS FOR EXCELLENCE " halafu unamalizia na kijiji kama ni kwembe haya, manyovu haya, buhigwe, nyakintonto, etc .. "

Hii nimeipenda na hususan itafaa sana kwa kijiji changu cha Katerero "DR. PROF JAKAYA KIKWETE CENTERS FOR EXCELLENCE - KATERERO"
 
Kwani watz mna maana???
nikikumbuka mlivyokuwa mnamshangilia nyerere na kumkashifu Mwinyi kipindi cha utawala wa awamu ya pili!!! na nikikumbuka jinsi mlivyokuwa mnamshangilia MWINY na kumtukana MKAPA kipindi cha utawala awamu ya tatu na mnavyoMSHANGILIA MKAPA na kumkashifu KIKWETWE kwenye awamu hii ya nne. napata uhakika mmoja tuu.
nao ni huu:-------------
1. watanzania hawajui wanataka na wanahitaji nini
2. hawajui nani mzuri kwao na nani ni msanii na adui kwao
3.wako tayari na watakubali kutawaliwa hata na mwendawazimu kama tu atakuwa na maneno na ahadi tamutamu
4. hawatumii vichwa vyao kufikiria bali mioyo yao(mapenzi yao kwa mtu ndo hupelekea kumkubali na kumuamini)
5 ni wadini- very sensitive on this
6. ni waroho, wala rushwa, sio wazalendo,waongo, wapumbavu, wanaedekeza ushabiki
Na cha kusikitisha zaidi....... hata MZEE MWANAKIJIJI NI Mmoja kati ya MAZUZU.
UKITAKA KUJUA WENGI WENU NI MAZUZU,,, SUBIRI TAREHE 17/10/2011 hukumu yakesi ya GODBLESS LEMA pale arusha mjini ndio utakapojua ukombozi bado uko mbali na hauwezi kuletwa na kundi dogo la CRUSADERS and pathetc tribal hardcore. if you dont wana be gratefull to himnyamaza tuu kaka kuliko kutumia nguvu nyingi.
.

Inaonesha tayari Magamba mnayo hukumu, Mnachotakiwa kufahamu ni kuwa Arusha si sawa na Igunga, ukiitishwa uchaguzi mdogo Arusha hata kura mlizopata 2010 hazitofikia robo.
 
kwa makala zako nyingi nilizosoma naona hii hujafanana nayo kabisaaa...!
otherwise sijaelewa kiundani maudhui ya makala yako!
 
Back
Top Bottom