Tume yajiapiza Arumeru kutangaza matokeo mapema.

Mzee wa Rula

JF-Expert Member
Oct 6, 2010
8,171
3,346
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) imejiapiza kuwa itatangaza matokeo ya uchaguzi mapema kwani ndiyo dhamira yao, na kuomba ushirikiano wa vyama.
Nec ilitoa kauli hiyo baada ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kuitaka kujipanga vizuri ili kutangaza mapema matokeo ya uchaguzi mdogo wa ubunge Jimbo la Arumeru Mashariki, mkoani Arusha Jumapili ijayo, la sivyo ucheleweshaji usio na maelezo ya msingi utasababisha vurugu.

"Arumeru itakuwa nzuri kama polisi watatenda haki, msiipendelee wala kuionea Chadema, CCM wala vyama vingine vinavyoshiki uchaguzi huu," alisema John Mrema katika mkutano kati ya Nec, Polisi na viongozi wa vyama vya siasa vilivyosimamisha wagombea katika uchaguzi mdogo jimbo la Arumeru Mashariki utakaofanyika Jumapili ijayo.


Katika mkutano huo uliofanyika Makumira jana, Mrema ambaye pia ni Mkuu wa Operesheni na Uchaguzi wa Chadema, aliitaka Nec kujipanga vizuri kutangaza mapema matokeo ya uchaguzi badala ya utaratibu uliozoeleka wa kuchelewesha kutangaza matokeo kwa siku kadhaa.
Alisema ucheleweshaji huo ambao mara nyingi hauna sababu za msingi unachangia kuleta hofu kwa wapiga kura na hivyo kuzusha vurugu.

"Mjipange sawasawa kutangaza matokeo, watu watachoka kusubiri matokeo hadi siku tatu, vurugu hapo ni lazima zitatokea," Mrema aliwaambia viongozi wakuu wa Nec.

Source:

:: IPPMEDIA

Mytake.

Mpaka leo bado sielewi sababu kuu za tume kuchelewesha matokeo lakini kwa kuwa imeahidi sina haja ya kulaumu zaidi ya kusubiri.

 
Hawatakubali kuyatangaza hadi CCM wamalize kuyachakachwaaaaa lakini wakumbuke Arumeru kuna morani walinzi wa jamii ya wamaasai wasiohofu chochote
 
Back
Top Bottom