Mnataka kumbebesha Hayati Magufuli madhambi yenu?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,478
39,997
Hivi mnataka tuamini kuwa Uchaguzi Tanzania miaka yote ulikuwa unafanyika vizuri, kwa Amani, na bila makadokado ya Chama tawala na wapambe wake? Kwamba kufika 2020 mambo yakaharibika? Yaani, tuamini JPM na timu yake walivuruga uchaguzi ili washinde 2020? Kabla ya hapo mambo yalikuwa powa. Uchaguzi wa 2015 na ule wa 2010 hakukuwa na matatizo?

Mmesahau kabisa yaliyotokea 2010?
Arumeru Mashariki
Nyamagana
Igunga
Nzega
Mbeya Mjini
Arusha Mjini
Tarime
Ubungo
Kilombero
Bumbuli

Na kuwa matokeo ya uchaguzi wa Rais yalivyodaiwa kupikwa na kundi la vijana waliofadhiliwa data center kumanipulate data za Tume?

Au mmesahau jinsi vyombo vya Habari vilivyokatazwa kutangaza matokeo ya Urais kama yalivyo majimboni...

Najibiwa...
Mwanakijiji wewe ni sukuma gang...uchaguzi wa 2015 ndio JPM aliuharibu wa 2010 was the best election ever!!

Nawajibu
Hakuna mwaka Tanzania ilishuhudia damu kumwagika kwenye uchaguzi ili kuhakikisha utawala unabakia madarakani kama 2010. That's a fact not an opinion.

Nawauliza:

Nani alimwaga damu kuelekea uchaguzi wa 2020 au siku ya uchaguzi?

NB*: Nimesahihisha hapo juu miaka.
 
Uchaguzi 2020 ulikuwa wa kipuuzi huuu ni ukweli mchungu

Tatizo labda wanaosema ndio wanafiki maana walishiriki kuhujumu uchaguzi.

Zigo la democracy na uchaguzi wa hovyo litamwandama magufuli vizazi na vizazi.

Tupende kusema ukweli magufuli alikuwa ni rais wa ovyo kwenye mfumo wa vyama vingi na hasa katika kipindi hiki cha digital wewe unatawala kama mkoloni ....

Angekuwa rais bora kama angetawala Tanzania baada ya Uhuru uko sio sasa.
 
Safi sana ! Wamechokoza Nyuki binafsi nimempa za uso January kwenye ule uzi mwingine , hii ni kwa sababu huyu ameshiriki uchafu mwingi sana , ikiwemo kupitishwa bila kupingwa kwao Bumbuli
Kawaida ni kawaida tu haiwezi kuwa kawaida kawaida nyingine wakati ni kawaida ileile....mchezo wa Bumbuli wapo hausahauliki...kurudisha zile fomu...
 
Kawaida ni kawaida tu haiwezi kuwa kawaida kawaida nyingine wakati ni kawaida ileile....mchezo wa Bumbuli wapo hausahauliki...kurudisha zile fomu...

..kama kuna madaraja ya uhalifu wa kisiasa Magufuli na genge lake wako daraja la juu kuwazidi wenzao.

..kwa mfano, shambulizi dhidi ya Tundu Lissu, unaanzaje kumtetea Magufuli kwa ushenzi wa kiwango kile?
 
Hivi mnataka tuamini kuwa uchaguzi Tanzania miaka yote ulikuwa unafanyika vizuri, kwa Amani, na bila makadokado ya Chama tawala na wapambe wake? Kwamba kufika 2015 mambo yakaharibika? Yaani, tuamini JPM na timu yake walivuruga uchaguzi ili washinde 2015? Kabla ya hapo mambo yalikuwa powa.

Mmesahau kabisa yaliyotokea 2010?
Arumeru Mashariki
Nyamagana
Igunga
Nzega
Mbeya Mjini
Arusha Mjini
Tarime
Ubungo
Kilombero
Bumbuli

Na kuwa matokeo ya uchaguzi wa Rais yalivyodaiwa kupikwa na kundi la vijana waliofadhiliwa data center kumanipulate data za Tume?

Au mmesahau jinsi vyombo vya Habari vilivyokatazwa kutangaza matokeo ya Urais kama yalivyo majimboni...

Najibiwa...
Mwanakijiji wewe ni sukuma gang...uchaguzi wa 2015 ndio JPM aliuharibu wa 2010 was the best election ever!!

Nawajibu
Hakuna mwaka Tanzania ilishuhudia damu kumwagika kwenye uchaguzi ili kuhakikisha utawala unabakia madarakani kama 2010. That's a fact not an opinion.

Nawauliza:

Nani alimwaga damu kuelekea uchaguzi wa 2020 au siku ya uchaguzi?
Mwaka 2020 hakukuwa na uchaguzi bali kulikuwa na uchafuzi. Ni aibu kwa level yako kama mwana JF mkongwe kuvaa miwani ya mbao kwenye huo uwendawazimu wa 2020
 
..kama kuna madaraja ya uhalifu wa kisiasa Magufuli na genge lake wako daraja la juu kuwazidi wenzao.

..kwa mfano, shambulizi dhidi ya Tundu Lissu, unaanzaje kumtetea Magufuli kwa ujenzi wa kiwango kile?
Ilitokea wakati wa uchaguzi, siku ya uchaguzi? Kwenye kampeni? Nani alimwaga damu kuelekea uchaguzi wa 2020? Ndiyo hoja iliyowekwa mezani.
 
Najibiwa...
Mwanakijiji wewe ni sukuma gang...uchaguzi wa 2015 ndio JPM aliuharibu wa 2010 was the best election ever!!
Dogo Makamba anajua kuwa aliyemfikisha hapo alipo kiuongozi ni muuaji wa uchaguzi wa 2010, mtu huyo yupo hai Ila hawezi kumsema, na badala yake anamsema mtu ambaye hayupo duniani, huo ni utoto na uhuni mwingi.

Mtu mwenye hali kama ya dogo Makamba hafai kuwa kiongozi popote pale. Ni wakati sasa wa wahuni kuwekwa kando katika uongozi.
 
Back
Top Bottom