MkuyuMkubwa
Member
- Sep 27, 2009
- 50
- 0
Nimepita sokoni, nikakuta watu wanajibishana.....mmoja anasema "yani huyu kikwete ndio bomu kweli, hebu angalia, maisha yanazidi kuwa magumu, uongozi umemshinda...kuongoza nchi kazi....ningejua wala nisingemchagua" ingawa ni maneno ya magengeni, lakini nijikuta napata swali gumu...kwamba pamoja na udhaifu mkubwa wa JK, hivi kwa haraka nani angekuwa bora zaidi katika wote alioshindana nao kutoka upinzani?...Lipumba, Mbowe, Mrema, Mvungi, nani angekuwa nafuu? hebu tujadili kwa kupima vigezo walivyonavyo.....wasiwasi wangu ni kwamba watanzania wanapenda upinzani kuimarisha utawala, lakini viongozi wengi wa upinzani wanapwaya mno kuaminika kwa dhamana ya kuongoza dola kama viongozi mbadala....nimeona kuna wanaosema labda ndani ya CCM kwakuwa alikuwapo Salim....lakini mimi naomba kujua katika wale walioshindanishwa na JK nani ambae tungemwamini dhidi ya JK kutokea upinzani/...au ndo tuseme upinzani ujipe nafasi zaidi kujizatiti bungeni? urais baadae kabisa?