Tulikosea kumchagua JK 2005, tungemchagua nani?

MkuyuMkubwa

Member
Sep 27, 2009
50
0
Nimepita sokoni, nikakuta watu wanajibishana.....mmoja anasema "yani huyu kikwete ndio bomu kweli, hebu angalia, maisha yanazidi kuwa magumu, uongozi umemshinda...kuongoza nchi kazi....ningejua wala nisingemchagua" ingawa ni maneno ya magengeni, lakini nijikuta napata swali gumu...kwamba pamoja na udhaifu mkubwa wa JK, hivi kwa haraka nani angekuwa bora zaidi katika wote alioshindana nao kutoka upinzani?...Lipumba, Mbowe, Mrema, Mvungi, nani angekuwa nafuu? hebu tujadili kwa kupima vigezo walivyonavyo.....wasiwasi wangu ni kwamba watanzania wanapenda upinzani kuimarisha utawala, lakini viongozi wengi wa upinzani wanapwaya mno kuaminika kwa dhamana ya kuongoza dola kama viongozi mbadala....nimeona kuna wanaosema labda ndani ya CCM kwakuwa alikuwapo Salim....lakini mimi naomba kujua katika wale walioshindanishwa na JK nani ambae tungemwamini dhidi ya JK kutokea upinzani/...au ndo tuseme upinzani ujipe nafasi zaidi kujizatiti bungeni? urais baadae kabisa?
 
kuchagua CHADEMA akigombea urais nani? au hata CHADEMA ikiweka jiwe tuchague tu?...hata hivyo mimi naomba turejee uchaguzi wa 2005 na haya yaliyotokea ndani ya utawala wa JK....tujiulize, kwakuwa ni kweli JK kachemsha, na tunaamini tulikosea, je tungemchagua nani kati ya washindani wake wale? akina Lipumba, Mbowe, Mvungi, nk?
 
Na ukisharejea then what ... utabadilisha matokeo ya uchaguzi?
 
lakini pia Magezi kumbuka kwamba CCM na JK wanashindwa kujenga taifa lenye neema kwasababu kubwa ya uongozi dhaifu...mwaka 2005 aliwekwa mbowe kwenye urais, unadhani mbowe angekuwa mbadala sahihi wa JK?...CCM na JK wanashindwa kujenga taifa lenye neema kwasababu ya udhaifu wa uongozi, unadhani kwanini tuamini mbowe huyu na cHADEMA hii ni mbadala kwa matatizo yanayotusumbua sasa, na kwamba kama tungepatia kumchagua mbowe tungenusurika na matatizo haya?
 
Umuhimu wa kurejea mazingira ya 2005 ni kwamba itasaidia kujua kama kweli tulikuwa na mbadala wa JK kutoka upinzani na hivyo iwe sahihi kujutia mamuzi ya kumchagua JK, au hapakuwa na mbadala wa JK na hivyo tusijutie mamuzi yetu..ni hivyo.
 
Niswa mwafrika...lakini JF ni kisima cha mjadala, tunajadili tulikotoka ili tusiridie kosa
 
Mwenyewe niliingia mkenge kwa kudhani JK angeleta mabadiliko ya kweli Tanzania lakini wapi!Mkuu swali lako kungekuwa na option ya kupendekeza mgombea mwingine katika ule mchujo wa ndani wa CCM basi ningechagua Salim.Sasa kwa vile hutaki twende huko mimi nadhani bora hata ya huyu JK tulienae kuliko tungefanya majaribio ya kuwapa wale wengine wa vyama vingine.Mtu na akili yako kweli umchague Mvungi awe Rais wa Tanzania au marehemu Prof.Shayo au DJ Mbowe?Labda sasa chadema wakimpitisha Dr.Slaa labda naweza nikawa na mawazo mengine.
 
Nimepita sokoni, nikakuta watu wanajibishana.....mmoja anasema "yani huyu kikwete ndio bomu kweli, hebu angalia, maisha yanazidi kuwa magumu, uongozi umemshinda...kuongoza nchi kazi....ningejua wala nisingemchagua" ingawa ni maneno ya magengeni, lakini nijikuta napata swali gumu...kwamba pamoja na udhaifu mkubwa wa JK, hivi kwa haraka nani angekuwa bora zaidi katika wote alioshindana nao kutoka upinzani?...Lipumba, Mbowe, Mrema, Mvungi, nani angekuwa nafuu? hebu tujadili kwa kupima vigezo walivyonavyo.....wasiwasi wangu ni kwamba watanzania wanapenda upinzani kuimarisha utawala, lakini viongozi wengi wa upinzani wanapwaya mno kuaminika kwa dhamana ya kuongoza dola kama viongozi mbadala....nimeona kuna wanaosema labda ndani ya CCM kwakuwa alikuwapo Salim....lakini mimi naomba kujua katika wale walioshindanishwa na JK nani ambae tungemwamini dhidi ya JK kutokea upinzani/...au ndo tuseme upinzani ujipe nafasi zaidi kujizatiti bungeni? urais baadae kabisa?

Ni vigumu kujua kama mtu anafaa uongozi au laa kabla hajapewa hiyo nafasi. Hiyo ni kwasababu kampeni za kisiasi ni kama matangazo.......bidhaa huonekana bora mpaka unapo inunua. Mfano mzuri ni huyo JK mwenyewe. So ni vigumu sana kujua nani angefaa.
 
Rais wa Tanzania atatoka ndani ya CCM na si vinginevyo kwani UPINZANI Tanzania
hauna nguvu bado.Chadema wana migogoro hata kabla hawajapewa nchi wakipewa si itakuwa balaa.Nyerere alisema rais atatoka ndani ya CCM. Wapo baadhi ya viongozi ndani ya CCM wanaweza kuiongoza nchi na kubadili mwelekeo wa CCM uliopo sasa kama akina Mwakyembe etc.ambao ni wapinzani wa mambo yanayofanyika ndani ya CCM.
 
Ni vigumu kujua kama mtu anafaa uongozi au laa kabla hajapewa hiyo nafasi. Hiyo ni kwasababu kampeni za kisiasi ni kama matangazo.......bidhaa huonekana bora mpaka unapo inunua. Mfano mzuri ni huyo JK mwenyewe. So ni vigumu sana kujua nani angefaa.

Mazee hatuwezi kwanza kuwafanyia majaribio wanasiasa wote wanaoomba kuongoza nchi kisha ndipo tujue nani anafaa na nani hatufai.Kama utaratibu ungekuwa huo basi tungekesha vizazi na vizazi kuwajua viongozi wanaofaa na wasiofaa.
 
You got me wrong. Ninacho sema mimi ni kwamba hakuna njia ya kuguarantee mtu ata kua raisi mzuri or not. Unaweza ukaangalia vigezo vyote na bado mtu ata disappoint. Ingekua as easy as you think then mara zote tunge chagua raisi anayefaa. Umenipata mkuu?
 
kuna watu walimchagua JK kwa sababu ya sura na kucheka cheka kwake, nakumbuka kipindi cha uchaguzi nilikuwa bado dent, wanafunzi wengi walisema JK atalipa kwa kuwa president mwenye sura nzuri na anapenda kusmile. Hivyo kwa kufuata sura hapo walikosea.

Ila kuhusu ugumu wa maisha sio bongo peke yake,nchi nyingi sasa uchumi mbaya. Sema tatizo la JK aliahidi maisha bora kwa kila mtanzania, lakini imekuwa kinyume wachache ndio wana maisha bora na wengi hawana hayo maisha bora.
 
kuchagua CHADEMA akigombea urais nani? au hata CHADEMA ikiweka jiwe tuchague tu?...hata hivyo mimi naomba turejee uchaguzi wa 2005 na haya yaliyotokea ndani ya utawala wa JK....tujiulize, kwakuwa ni kweli JK kachemsha, na tunaamini tulikosea, je tungemchagua nani kati ya washindani wake wale? akina Lipumba, Mbowe, Mvungi, nk?

ndio tatizo lako hilo kumbe unachagua mtu na sio chama..mkuu anasema 2010 ni kuchagua CHADEMA wewe unauliza akigombea nani?daaah pole Tanzania japo nakupenda kwa moyo wote
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom