Tulikosea kumchagua JK 2005, tungemchagua nani?

kuchagua CHADEMA akigombea urais nani? au hata CHADEMA ikiweka jiwe tuchague tu?...hata hivyo mimi naomba turejee uchaguzi wa 2005 na haya yaliyotokea ndani ya utawala wa JK....tujiulize, kwakuwa ni kweli JK kachemsha, na tunaamini tulikosea, je tungemchagua nani kati ya washindani wake wale? akina Lipumba, Mbowe, Mvungi, nk?
naamini and i hope wapo wengine kama mimi kwamba si kwamba mpinzni wake angetoka kambi tofauti bali ndani ya CCM there were other candidates better suited for the job...yaani the mistake was made in the partys selection of a candidate
 
Wanatamba na kusema CCM hata wakisimamisha ng'ombe kugombea urais atapata tu ngoja tuone 2010
 
Wanatamba na kusema CCM hata wakisimamisha ng'ombe kugombea urais atapata tu ngoja tuone 2010
Si kwamba wanatamba bila sababu, wao wenyewe wanajuwa kuwa wameshawahi kutuwekea malofa na bado tukayachagua hivyo wanakijuwa wanachokisema.
 
Aliyebora kupita wengine wote mwaka 2005, alikuwa Prof. Lipumba, lipumba na CUF angeweza kuwa rais bora kuliko kikwete mara nyingi sana....wengine aliobaki ni pasua kichwa akiwemo kikwete mwenyewe.
 
Hivi mbiu ya maisha bora kwa kila mtanzania ilitolewaje tolewaje? mbiu za chama huwa zinafanyiwa mchakatio wa kueleweka ili kuzuia wanadi wasinadi kitu kisichowezekana i.e. wasitoe too much ambition? Kama huwa zinahakikiwa ni nani huifanya hivyo kazi? Maana nakumbuka hii ilikuwa mbiu ya maisha bora kwa kila mtanzania kama sikosei ni ya chama na si ya kikwete kama kikwete au nimekosea?

Najiuliza tu isijekuwa tunamhukumu kwa makosa yasiyoyake !
 
katika kupima mafanikio ya mtu, lazima tuangalie yale yalio ndani na nje ya uwezo wake!! kwa mfano suala la 'kuanguka kwa uchumi duniani' limeathiri uchumi wetu kwa kiasi fulani na hivyo kuathiri maisha ya mtanzania!!! lakini katika suala la ufisadi??!! lazima, mafisadi wawajibike!!! tusiwe rahisi wa kulaumu pasipo kwanza kutathmini kwa kina hoja inayozungumzwa!!!!
 
naamini and i hope wapo wengine kama mimi kwamba si kwamba mpinzni wake angetoka kambi tofauti bali ndani ya CCM there were other candidates better suited for the job...yaani the mistake was made in the partys selection of a candidate
Hakuna chema kinachotoka kwenye uozo mh kelelee, kama msafi mmoja yupo kati ya wachafu 100, atawezaje kuongoza asichafuke na wakati wachafu hao hao ndo watendaji wake?

chagua chama, yes, angalia kisicho na uozo, au kisichofungia uozo ndani na kukana kuwa hakuna harufu mbaya labda inatoka kwa jirani yake wakati inzi wanaonekana wanaizunguka nyumba yako wakitafuta pa kuingilia.

heshima mbele.
 
Lipumba ni Msomi mzuri hivyo anafaa kuwa Rais wa TZ lakini tatizo kubwa anatumiwa na Wapemba kama chambo na CUF yao. Nani anakubali kutawaliwa na Wapemba??? CUF ni CHAFU kwa Udini/ Uisilam na Upemba wao. Ni chama kinachonuka kwa uchafu huo.Hayo yanaeleweka jamani. Labda Lipumba ashauriwe kuhamia CHADEMA.
 
Utawajua waliotumwa na Maaskofu na wenye chuki na uislamu kwa maneno yao. Je tuseme CHADEMA ni Chafu kwa Udini (Ukristo) /Uchaga wao. Ni chama kinachonuka kwa uchafu huo. hayo yaneleweka Jamani. Labda Slaa/Mbowe ashauriwe kuhamia CCM. Hivyo ni unavyotueleza uliyoficha kwenye roho yako ni mabaya zaidi kwa jamii ya kiislamu. Lakini ndugu jinyonge sisi tunatesa. na siku ya kiama tutatesa zaidi.
 
Nimepita sokoni, nikakuta watu wanajibishana.....mmoja anasema "yani huyu kikwete ndio bomu kweli, hebu angalia, maisha yanazidi kuwa magumu, uongozi umemshinda...kuongoza nchi kazi....ningejua wala nisingemchagua" ingawa ni maneno ya magengeni, lakini nijikuta napata swali gumu...kwamba pamoja na udhaifu mkubwa wa JK, hivi kwa haraka nani angekuwa bora zaidi katika wote alioshindana nao kutoka upinzani?...Lipumba, Mbowe, Mrema, Mvungi, nani angekuwa nafuu? hebu tujadili kwa kupima vigezo walivyonavyo.....wasiwasi wangu ni kwamba watanzania wanapenda upinzani kuimarisha utawala, lakini viongozi wengi wa upinzani wanapwaya mno kuaminika kwa dhamana ya kuongoza dola kama viongozi mbadala....nimeona kuna wanaosema labda ndani ya CCM kwakuwa alikuwapo Salim....lakini mimi naomba kujua katika wale walioshindanishwa na JK nani ambae tungemwamini dhidi ya JK kutokea upinzani/...au ndo tuseme upinzani ujipe nafasi zaidi kujizatiti bungeni? urais baadae kabisa?

Kwa jinsi JK alivyotuongoza kwa kipindi hiki cha miaaka minne, then naanza kuamini kuwa urais siyo ugumu kama tunavyofikiria na kila Mtanzania anaweza kuongoza kama atapewa nafasi including mimi na wewe!!!
 
Urais rahisi sana...tatizo nikupata..nenda kagombee uone kasheshe yake..kama uko kwenye system tengeneza mtandao na sera zako tukuchambue...
 
I think mbowe and all his colleagues at Chadema will make a good leadership. we need to change the mindset of thinking that CCM is the only "ruling party" in Tanzania.
 
Mwaka 2005 ni mwaka pekee ambao Watanzania tulimchagua Rais bila shinikizo kutoka kwa Mwalimu JK Nyerere.

Ni rais pekee ambaye katika utawala wke hakuna confrotation iliyojitokeza hadi sasa kusababisha matumizi ya nguvu kwa raia.

Ni Rais pekee ambaye ameweza kuanzisha mpango wa shule za sekondari kwa kila kata.
Ni Rais pekee aliyeamua kuunganisha mikoa ya kufungua Mikoa iliyoko nyuma kama Kigoma na Rukwa na kuiunganisha na barabara kuu,ikiwa ni pamoja na ile ya Kagera hadi Mwanza ili ku stimulate biashara na uchumi katika nchi pamoja na kwamba dunia imo katika hali mbaya kiuchumi.
Ni rais pekee ambaye katika utawala wake ameweza kuwapeleka mahakamani watuhumiwa wa ufisadi wakubwa ili wapambane na sheria.
ni katika utawala huu ambao Kilimo kinapewa kipaumbele ili wakulima wetu walime kwa kutumia zana za kisasa kwa vitendo siyo blah blah.
Bila kusahau University ya Dodoma,vivuko vipya Kigamboni,Mv Misungwi na vinginevyo.
Amefanya mageuzi makubwa kwa vyombo vya habari kuwa huru na midomo ya watu kuzungumza bila vitisho.Sasa ati tulikosea! Ili kujua kuwa hatujakosea subiri muone 2010.JK atachaguliwa tena kwa kura zaidi na ataanza ngwe ya pili kwa mipango madhubuti ya maendeleo ya kweli na uhakika!
 
nadhani na akimaliza ngwe ya pili tubadili katiba ili apate awamu nyinmgine kwa sababu anafanya mambo makubwa sana
 
Mi nadhani hii nchi inatakiwa apewe dikteta mwenye vision, hakuna haja ya kupiga porojo. viongozi wetu hakuna anejua anataka afikishe nchi wapi.

Anatakiwa mtu wa style ya Kagame au Chaves

Anatakiwa mtu wa style ya Kagame au Chaves au Mrema
 
Ni vigumu kujua kama mtu anafaa uongozi au laa kabla hajapewa hiyo nafasi. Hiyo ni kwasababu kampeni za kisiasi ni kama matangazo.......bidhaa huonekana bora mpaka unapo inunua. Mfano mzuri ni huyo JK mwenyewe. So ni vigumu sana kujua nani angefaa.

So philosophical, that's why I like JF!
 
Ngoja niharibu mjadala kwa muda:

Firstlady1 nimependa avatar yako!.

Tumezidi kuwa serious. LOL
 
Utawajua waliotumwa na Maaskofu na wenye chuki na uislamu kwa maneno yao. Je tuseme CHADEMA ni Chafu kwa Udini (Ukristo) /Uchaga wao. Ni chama kinachonuka kwa uchafu huo. hayo yaneleweka Jamani. Labda Slaa/Mbowe ashauriwe kuhamia CCM. Hivyo ni unavyotueleza uliyoficha kwenye roho yako ni mabaya zaidi kwa jamii ya kiislamu. Lakini ndugu jinyonge sisi tunatesa. na siku ya kiama tutatesa zaidi.

Tumain usipoingiza udini huoni raha kabisa!
 
Tumain usipoingiza udini huoni raha kabisa!
In every action there is equal and opposite reaction
Waulize wao ambao hawaachi kuleta thread na issue za dini (kusema uislam). Tumeruhusiwa kuwajibu ikiwa wao wataanza.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom