Tulikosea kumchagua JK 2005, tungemchagua nani?

Tungemchagua ..SALIM AHMED SALIM.........

nafasi ya urais huu ilikuwa yake ..akadhulumiwa kwa kampeni chafu za maji ya taka za wanamtandao wakiwashirikisha zanzibar[na wanaojiita baraza la mapinduzi]....uchafu wa kampeni za wanamtandao na jk...zitaendelea kuwaandama wao kwani machozi ya waliochafuliwa kama kina ..malecela,kigoda,sumaye.,msuya....kitine,simba , na wengine wengi walioonekana tishio kwa mgombea wao...yataendelea kumuandama jk...kwa kufanya kiini macho watu na itazidi kumsaababishia laana...hasa kwa kufikia kutumia jina la mungu...kusema chaguo la mungu....JK anahitajika kutubu dhambi alizowafanyia wenzake ....kwa kuwaomba msamaha one in one....
 
labda hii inchi ikabidhishwe kwa jeshi

Hasira hasara, halafu jeshi likishindwa nchi irudishwe kwa raia tena?

Tupo kwenye njia safi tu na yenye haki ya demokrasia. Tuimarishe DEMOKRASIA mpaka ndani ya vyama vyenyewe, isiwe MAFISADI wa kakikundi kadogo ka NEC wanatuletea majina ya mgomembea uraisi.
 
Rais wa Tanzania atatoka ndani ya CCM na si vinginevyo kwani UPINZANI Tanzania
hauna nguvu bado.Chadema wana migogoro hata kabla hawajapewa nchi wakipewa si itakuwa balaa.Nyerere alisema rais atatoka ndani ya CCM. Wapo baadhi ya viongozi ndani ya CCM wanaweza kuiongoza nchi na kubadili mwelekeo wa CCM uliopo sasa kama akina Mwakyembe etc.ambao ni wapinzani wa mambo yanayofanyika ndani ya CCM.

Muumini mzuri, yaani CCM wameshindwa kwa miaka karibu hamsini lakini bado unaamini lazima TZ iwe chini ya CCM. Kama unaamini CHADEMA hawawezi kama vile CCM isivyoweza, basi sioni sababu ya kutowapa CHADEMA nafasi ya uraisi kwa msingi wa kupeana zamu tu.
Kuhusu CCM: Nyerere pia alisema CCM si mama yangu, na angekua mzima angeshahamia CHADEMA.
 
Mi nadhani hii nchi inatakiwa apewe dikteta mwenye vision, hakuna haja ya kupiga porojo. viongozi wetu hakuna anejua anataka afikishe nchi wapi.

Anatakiwa mtu wa style ya Kagame au Chaves
 
hivi kwa haraka nani angekuwa bora zaidi katika wote alioshindana nao kutoka upinzani?...Lipumba, Mbowe, Mrema,
Mbowe mkubwa,
Sera za chadema zipo kamili na chama chenyewe kina watu makini. Hakuna kama chadema ila tu hatutoshi kuwaweka madarakani lakini taratibu tunakwenda na tutashinda tu.
 
Mbowe mkubwa,
Sera za chadema zipo kamili na chama chenyewe kina watu makini. Hakuna kama chadema ila tu hatutoshi kuwaweka madarakani lakini taratibu tunakwenda na tutashinda tu.

well said..ni kweli mkuu wangu KURA HAZITOSHAGI ila kuna siku ZITATOSHA
 
Nionavyo mimi tungezungumzia uteuzi ndani ya ccm na siyo upinzani kwani 2005 hakukuwepo na mpinzani ambaye angeweza kufanya hata nusu ya Kikwete aliyoyafanya kwa kipindi cha miaka 4 madarakani. Naamini ndani ya ccm kulikuwepo na watu bora kuliko Kikwete. Salim A. Salim angepewa nafasi nafikiri tungekuwa na maisha tofauti na tuliyonayo sasa hivi. Nadhani asingekuwa anakurupuka na vijisera vya ajabu ajabu kama kilimo kwanza n.k. Ndani ya ccm wapo watu wenye uwezo ila tatizo kubwa ni kujua ni yupi msafi atakayeweza kusema sidanganyiki wala sishawishiki kwenye ufisadi.Awe na Unyerere fulani wa kuweza kukemea maovu na watu wakatikisika badala ya mtu anayetabasamu wakati anazungumzia jambo gumu linalohusu nchi.
 
Tungemchagua ..SALIM AHMED SALIM.........

nafasi ya urais huu ilikuwa yake ..akadhulumiwa kwa kampeni chafu za maji ya taka za wanamtandao wakiwashirikisha zanzibar[na wanaojiita baraza la mapinduzi]....uchafu wa kampeni za wanamtandao na jk...zitaendelea kuwaandama wao kwani machozi ya waliochafuliwa kama kina ..malecela,kigoda,sumaye.,msuya....kitine,simba , na wengine wengi walioonekana tishio kwa mgombea wao...yataendelea kumuandama jk...kwa kufanya kiini macho watu na itazidi kumsaababishia laana...hasa kwa kufikia kutumia jina la mungu...kusema chaguo la mungu....JK anahitajika kutubu dhambi alizowafanyia wenzake ....kwa kuwaomba msamaha one in one....

...................................................................................................Kwa swali husika, Salim hayupo maana alishatupwa na chama chake. Nakubaliana na mtoa mada, kuwa kama tulikosea kumchagua JK, 2005, tungenchagua nani?. Jibu ni kuwa 2005, hatukokosea kumchagua JK kwa vile hatukuyajua mambo yake, ila pia kati ya wote aliosimama nao 2005, JK was the best option.........................................................................................................Ya 2005 yamepita sasa yanakuja ya 2010, kama tulukosea, kufanya kosa sio kosa, kosa ni kurudia kosa kwa kumchagua tena JK 2010. Ili kujua tutamchagua au laa, lazima tujue atasimama na nani. Kama wapinzani hawana mtu makini wa kusimamas na JK, yakawa ni maboya matupu kama 2005, them for sure 2010 ni JK tena japo sio kwa kishindo kama cha 2005........................................................................................................Narudia kuusema msemo huu, na nitakuwa ninaurudia rudia kila mara mpaka baada ya uchaguzi........................................................................................................."Kuna wengi wanaichagua CCM, sio kwa sababu wanaipenda, bali kwa sababu hawana jinsi, hivyo kuliko kupoteza kura yako, bora kumpa mwenye nacho, anaongezewa, kuliko kumpa asiyenacho, maana atanyang'anywa hata kidogo alichonacho"........................................................................................"Na kuna wengine wengi wanaichagua CCM, kwa sababu ya kutopata fursa zaelimu ya uraia, hivyo hawajui watendalo, ndicho kilichotokea Busanda na Biharamulo, baada ya zile chaguzi ndogo, elimu imewafika, hivyo maeneo yote yenye mwamko wa kielimu, Kilimanjaro, Arusha, Mbeya, kanda ya Ziwa, CCM inakazi kidogo sio mteremko"........................................................................................................"Sehemu zenye maendeleo duni, hali ya mazingira za shida shida, kama mikoa ya Kusini, Singida, Dodoma and the like, CCM ndio baba, CCM ndio mama"........................................................................................................."Angalizo: Huu ni mtazamo wangu sina lengo la kuwatusi watu wala kufagilia mtu, 2010 ni CCM tena!".
 
...pamoja na udhaifu mkubwa wa JK, hivi kwa haraka nani angekuwa bora zaidi katika wote alioshindana nao kutoka upinzani?
Angalia pia na alioshindana nao ndani ya CCM, labda namo kuna alternative ambaye angekuwa bora kuliko yeye
 
wewe unang'ang'ania kujua nani angekuwa bora katika walioshindanishwa tu, lipumba, mbowe wote wangekuwa bora...na upande wa CCM walikuwepo watu wenye uwezo mkubwa kuongoza nchi hii...........
mimi nataka nikuulize kitu kimoja tu:
1. nini alifanya JK kikubwa kabla ya kuteuliwa kuwa mgombea katika nchi hii?
2. amefanya nini mpaka sasa kikubwa cha kujivunia? na 2010 mtamuweka tena ili aendelee kuuza zura kwa Obama.
 
Mi nadhani hii nchi inatakiwa apewe dikteta mwenye vision, hakuna haja ya kupiga porojo. viongozi wetu hakuna anejua anataka afikishe nchi wapi.

Anatakiwa mtu wa style ya Kagame au Chaves

Kwa hilo 2005 tungechagua Mrema, awapigishe kwata japo kwa awamu moja watu wawe na nidhamu. Masuala ya elimu baadae mbona Ruksa alikua ni mwalimu.
 
kuchagua CHADEMA akigombea urais nani? au hata CHADEMA ikiweka jiwe tuchague tu?...hata hivyo mimi naomba turejee uchaguzi wa 2005 na haya yaliyotokea ndani ya utawala wa JK....tujiulize, kwakuwa ni kweli JK kachemsha, na tunaamini tulikosea, je tungemchagua nani kati ya washindani wake wale? akina Lipumba, Mbowe, Mvungi, nk?
kwangu simuoni yeyote ambaye asingechemsha , nilikuwa namwamini mbowe lakini kwa haya yaliyotokea juzi kwenye uchaguzi mkuu wa chadema kanitia mashaka zaidi. hiyo CUF ndo haiko kabisa kwenye akili yangu maana huyo lipumba na mwenzie wamenichosha hata kuwaangalia kwenye Tv. na wote hawa makelele yao wanapiga huku nje wakiingia ikulu watakuwa walewale sina hata ninayemuamini bora zimwi likujuaee............................
 
wewe unang'ang'ania kujua nani angekuwa bora katika walioshindanishwa tu, lipumba, mbowe wote wangekuwa bora...na upande wa CCM walikuwepo watu wenye uwezo mkubwa kuongoza nchi hii...........
mimi nataka nikuulize kitu kimoja tu:
1. nini alifanya JK kikubwa kabla ya kuteuliwa kuwa mgombea katika nchi hii?
2. amefanya nini mpaka sasa kikubwa cha kujivunia? na 2010 mtamuweka tena ili aendelee kuuza zura kwa Obama.
Kinachonisikitisha ni kuwa wapondaji kama wewe huwa hampigi kura, lakini mko mstari wa mbele kama tai. Na hii ndiyo inayowagharimu walioko vyama vya upinzani. Maneno mengi lakini when it comes to kupiga kura hawaonekani............ akichaguliwa asiyempenda, analalamika kuwa kura zimeibiwa.

Mi nadhani hii nchi inatakiwa apewe dikteta mwenye vision, hakuna haja ya kupiga porojo. viongozi wetu hakuna anejua anataka afikishe nchi wapi.

Anatakiwa mtu wa style ya Kagame au Chaves.
Mimi nakubaliana na wewe, maana ukicheki utakuta vitu vikubwa na vyenye kuhitaji nguvu vilifanywa enzi za udikteta...eg Reli ya kati, Grid ya taifa. Kwa sasa kujenga vitu kama vile vinahitaji dikteta tuuu
 
Tunarudi pale pale chama kilichoshika hatamu kinapaswa kuliangalia swala hili kwa kuzingatia utaifa zaidi, Imefika wakati sasa waweke mgombea mwenye nia ya kujenga nchi na kuachana na ushbiki wa sura na umaarufu. Mbona huko ndani ya CCM kuna akina Kagame? Uroho wa madaraka na ubinafsi + ushamba na ulafi wa madaraka utaendelea kutuumiza
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom