Gagurito
JF-Expert Member
- Feb 11, 2011
- 5,600
- 804
- Thread starter
- #61
Niliupenda ule wimbo wa sugu wa "MIKONONI MWA POLISI", Jamaa alichana haswa, c unajua tena harakati toka kitambo enzi za "Muziki & Maisha" teh!nilikuwa muumini mzuri sana wa bwana sugu na sijawahi kukosa tape yake yoyote...nakumbuka wimbo wake ndani ya bongo alisema maneno haya...maisha ni kujirusha unataka kuleta zako zipi,maisha yenyewe ni mafupi,ndani ya bongo...hii ilikuwa korasi.kuna kipande anasema...kwako maisha ni matamu,kwangu ni magumu ndo maana nilaumu.iweje mi nirudi kijijini wakati mbunge wangu yupo mjini,anatanua na shangingi.mi nina akili nyingi toka msingi mpaka sekondariila naona hatari kwenda chuo kikuu,FFU wasijenivunja miguu nitakapogoma kusoma.mi nasema msije sema mi sikusema..Funika ilikuwa wimbo wa ndoto ambapo huwa nahisi aliota atakuja kuwa mbunge...mistari yake inasema....usiku naota ndoto napigana na shetani....mchana naota ndoto natoa hotuba bungeni..mwaka 2000 rais ni nani,ni ndoto.