Habari wana JF? Tutafakari kuhusu mafanikio ya bodi ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu katika utekelezaji wa mapendekezo ya tume iliundwa na raisi JK kutafiti mfumo bora wa utoaji wa mikopo. Uundwaji wa tume ulitokana na migogoro/maandamano/migomo isiyokwisha vyuoni kutokana na mfumo mbovu wa utoaji wa mikopo.Kutokana na utekelezaji wa mwanzo wa mapendekezo ya tume,je dawa ya kumaliza tatizo imepatikana?tunaishauri ni wizara husika?