Nchi haiwezi kamwe kuwa na viongozi wazuri toka kizazi hiki, kama HESLB wamekuwa miungu watu!

Lyambalyetu

JF-Expert Member
Apr 6, 2021
265
240
Ni mbaya sana. Yaani semester ya kwanza vyuoni inamalizika lakini watoto wengi wale waliopata mikopo batch ya mwisho hawajapata. Watoto hawa wamekuwa wakiingia na kutoka Ofisi za Maafisa Mikopo vyuoni na hata kwenye Ofisi zao hao HESLB lakini hawasaidiwi chochote.

Imeniskitisha nimekutana na Mwanafunzi wa Chuo ameamua kurudi nyumbani kusikilizia kwanza kwa kuwa mkopo wake hajapewa kwani malipo toka Board hayajafanyika. Mbaya sana hii!

Huyu Badru pamoja na kutumia mifumo ya kisasa lakini kazi imemshinda kabisa.

May be kwa sababu wanaohangaika ni watoto wa maskini - angekuwa mtoto wa Waziri wetu wa Elimu pengine ni mnufaika wa hii mikopo labda pengine wangekuwa wameshalipwa.

HESLB kwa kweli inaumiza mnoo! Watoto hawa kwa kuwa wanaenda vyuoni umri mdogo tofauti na wenzao wa zamani basi wanagugumia tu na hawawezi kujitetea na wala kupigania haki zao - yaani hata niliyemwona anarudi nyumbani baada ya malipo yake kuchelewa kuingia amekonda ile mbaya.

HESLB mna dhambi sana nyie! Kweli tena!
 
Yani Heslb ni jipu watu wa diploma wengi hawajalipwa hadi sasa hivi watu wa degree ndo usiseme halafu sasa hvi wanawazuia wanafunzi kuingia ofisini kwao kwa kigezo kua wawe na referal form kutoka kwa ma loan officer na ma loan officers hawatoi izo referal wamepewa maelekezo kutoka bodi kwamba watalipwa tu huu ni mwez wa 3 sasa sentensi ni io io kwakweli bodi ya mikopo ni shida sana na wanafunzi wengi wamekaribia mitihani kimbembe kweli JamiiForums JamiiCheck tunaomba mtusaidie kupublic hii kitu wanafunzi vyuoni wanateseka
 
Back
Top Bottom