Habari kwa wana JamiiForums!
Naomba niende kwenye simulizi moja kwa moja, hii ilinikuta miaka kadhaa iliyopita. Mambo yalikuwa hivi:-
Wakati ninaanza kidato cha kwanza katika shule moja ya Serikali mkoani Mbeya kama ilivyo kwa wazazi wengi baba yangu alinipa maneno haya "soma kwa bidii, shuleni ufuate Elimu tu!", Maneno haya yalinijaa vyema kichwani mwangu, si kwamba yalinikaa kwakuwa nilikuwa msikivu ila ni kwakuwa katika familia yetu kaka yetu mkubwa ambaye ndiye mzaliwa wa kwanza kwetu alimsumbua sana mzee wetu.
Kichwani nilitaka nibadilishe imani ambayo ilianza kujengeka kwa mzee wetu kwamba "watoto wa kiume kwake tulikuwa kama mzigo", kutokana na kutoka kwenye shule za Serikali ambazo msingi wake katika somo la Kiingereza sio mzuri hata mimi nilipatwa na tatizo linalowakumba wanafunzi wengi kutoka shule za Serikali (Darasa la saba) "Ung'eng'e" uliniyumbisha sana.
Katika mkondo wetu (mkondo B) tulikuwa na wanafunzi wawili ambao walitoka shule za English Medium. Hali ya kuwa na uchu wa kujua lugha ya Kiingereza ilikuwa kubwa ila iliambatana na uoga wa kuuliza kwa mara ya kwanza. Ki-haiba nilikuwa mpole na sio kobe kobe ila upole wangu ulinifanyaa nionekane mtulivu lakini kwa bahati mbaya mtulivu ambaye hata darasani matokeo yangu yalikuwa ya kawaida tu.
Baada ya mwalimu wa English kuanza kufundisha (baada ya kozi ya miezi mitatu ya Kiingereza inayotolewa shuleni kuisha) hapa ndipo nilipoanza kupata mwangaza wa lugha ya Kiingereza. Nakumbuka mtihani wa kwanza wa Kiingereza nilioufanya tulitakiwa kuandika barua iliyokuwa ikihusu 'Pocket Money' yaani pesa ya Matumizi. Nilikuwa sijui maana ya neno "Pocket Money" na ninakumbuka niliandika ya kwamba nilisahau "Pocket Money" katika ile barua nikijiweka kwenye 'neutral ground' hapa nilikuwa nabahatisha tu 😂😂
Katika hiyo barua nilichokiandika nikikikumbuka huwa nacheka tu, hata sanduku la Posta niliandika S.L.P badala ya neno P.O BOX. Nashukuru Mungu mwalimu aliamua kukata na kuniandikia P.O BOX. Baada ya mwalimu wetu huyo kuanza kutufundisha angalau nilianza kuuona mwanga.
Siku zilisonga lakini kwa bahati mbaya licha ya kwamba shule yetu ya ilikuwa katikati ya jiji haikuwa na walimu wa Masomo ya Fizikia, Kemia, Baiolojia na Hesabu. Kwa jitihada za mkuu wa shule tulipata walimu wa ziada ambao nao walikuwa wakiondoka baada ya malipo yao kusuasua. Muda ulienda na hatimaye tukaingia kidato cha Pili, hapa mambo yalianza kuwa ya ajabu ajabu kidogo.
Sikuwa na utaratibu wa kujisomea vitu ambavyo sikufundishwa na hapa ndipo nilipopigwa na pigo la kwanza. Tulipoingia katika mtihani wa Mock wa kidato cha Pili, katika somo la Hesabu tulikuwa tumesoma mada tatu tu (Exponent and Radical, Algebra na Logarithms), mtihani ulipokuja ulitubamiza vibaya na shule yetu ilikuwa miongoni mwa shule za mwisho katika matokeo ya mtihani wa Mock, tulifanikiwa kuishinda shule moja tu na sisi tuliibuka kwenye nafasi ya pili kutoka mwisho.
Hesabu iliniangusha ila nilifaulu Fizikia, Kemia na Baiolojia katika masomo ya Sayansi (kwa marks kuanzia 55% na Kemia ndilo somo nililopata 72%) kwangu niliona ulikuwa ushindi mkubwa na nikaamua kuongea na mzazi anilipie pesa ya Masomo ya ziada ili nijifunze somo la Hesabu.
Baada ya kuanza masomo ya ziada kwa moja kati ya ma'brother' wa mtaani kwetu ambaye alikuwa mwanafunzi aliyekuwa anaendelea na Masomo ya ngazi ya juu kutoka chuo kikuu cha Dar Es Salaam--UDSM hapo angalau Hesabu zikaanza kuingia kichwani. Tulianza na mada ya 'Similarity and Congruence' hapa nilianza kuona kwamba Hesabu haikuwa ngumu kama mwanafunzi anaweza kupata mwalimu mzuri. Nilikuwa nafurahia namna ambavyo nilivyokuwa nikifundishwa na yule "brother" ambaye katika mtaa alikuwa miongoni mwa 'vipanga' ambao walikuwa wa mwanzo kufaulia shule za vipaji wakati wa kujiunga na kidato cha Kwanza.
Wakati pindi linaendelea nilianza kujinoa taratibu katika usomaji na hatimaye ikawa ni tabia yangu kusoma na hapa ikawa msuli na mimi, nakumbuka sikuwahi kuwa na timu ninayoishabikia nilikuwa na ule ushabiki wa juu wa mpira ilikuwa ni kwamba akishinda Manchester na nikapata habari basi nitakenua na kuendelea na mambo mengine. Nilikuwa napenda kusoma hadithi za Kiingereza kupata maneno mapya ili kukuza idadi ya misamiati ambayo kuna muda niliishia kuikariri tu kwani sikupata mahali pakuitumia.
Baada ya matokeo ya Kidato cha Pili kutoka na mimi nilikuwako katika idadi ya wale watu ambao walifanya vizuri ingawa sikupewa zawadi kwakuwa ufaulu watu ulionekana wa kawaida mbele ya "vipanga" wa darasa sikukata tamaa nikaona niendelee na pindi tu, mtafutaji hachoki na mimi nilikuwa nikijiapiza.
Katika ukuaji kuna baadhi ya marafiki niliowapata hapo hapo shuleni waliokuwa wakifanya ngono na kuja kutupa stori wakati wa break na wangejisifia sana, ninachoshukuru Mungu ni kwamba nilikuwa muoga muoga na nisingeweza kuongea na msichana ana kwa ana na hiyo ilinisaidia kuepukana na kutafunana kimazoea na wale warembo wa darasani. Nilikuwa nikisikia kwamba fulani alikuwa akinitaka ila sikuwa na muda nao kabisa.
Baada ya kuona shule inaendelea kukosa walimu nikaamua kumuomba mama kwa kuikandia shule niliyokuwa nikisoma na kumwambia hali halisi kwamba haikuwahi kutokea waliofaulu kuingia kidato cha Tano kufika 15 tangu shule ilipoanza hivyo nikaomba uhamisho na kuhama kabisa.
ITAENDELEA
UPDATES
Sehemu ya Pili