washasimu
Member
- Feb 25, 2024
- 7
- 2
Hellow
Kwa majina naitwa washasimu washasimu ni mtoto wa tatu kwenye familia yetu kati ya watoto wa 5 na hii ndio historia yangu kwa ufupi
MAISHA YANGU YA UTOTO
Maisha yangu ya utoto kati ya miaka 7 mpaka 13 kifupi yalitawaliwa na furaha kiujumla kwa sababu nilikuwa huru sana kuchagua marafiki na watu wa kucheza nao baba na mama yangu wote walikuwa wafanya biashara so mama anaondoka asubuhi na kuludi jioni baada ya kutoka kwenye Mishe zake na baba pia ni hivyo hivyo so nilikuwa huru sana kwenda mitaa yoyote ile kucheza na ikifika jioni naludi nyumbani naoga na kuendelea na maisha mengine katika umri huo nilikuwa napata uangalizi mkubwa sana kutoka kwa kaka zangu na rafiki wa kaka zangu so pamoja na uhuru wote lakini nilikuwa under guidance kifupi nilikuwa ni mtoto mwenye tabia njema sikuwahi tukana mtu matusi ya nguoni(hususa ni viungo vya uzazi) na niliogopa sana na pia mimi mwenyewe nilikuwa najilinda sana na makundi mabaya sababu baba na mama kila siku walikuwa wananionya
MAISHA YA SHULE
Nilianza shule mwaka X(kipindi ambacho Kikwete alikuwa yupo madarakani) sikusoma vidudu nilianza tu darasa la kwanza Hii ulinipa shida sana hasa katika maendeleo yangu ya shule coz nilikuwa sijui kusoma wala kuandika na kwaio iliniwia vigumu sana kufauru katika darasa la kwanza kipindi nipo darasa la kwanza nilikuwa na mwili mdogo sana kwaio nilikuwa naonewa na wale wakubwa ukiongeza na kutokufauru shule nikajikuta naichukia shule kiujumla hapo ndipo nikaanza kushinda porini katika umri mdgo kabisa nakumbuka ulikuwa ni mwezi wa 4 ndipo nilipoanza kushinda porini
Maisha ya kushinda porini yaliendelea mpaka mwezi wa 8 hapo bado sijui kusoma wala kuandika kuna siku nimekaa porini nimejificha nashangaa wanafunzi wenzangu wanakuja upande wangu wakiwemo na wale ambao huwa nashindaga nao porini mimi baada ya kuwaona wale washkaji zangu nikajua hakuna noma yoyote huwenda tumeongezeka idadi kumbe wametumwa na mwalimu wa darasa waje kunikamata baada ya kunikamata nikapelekwa kwa mwalimu wa darasa siku ile nilikula sana bakora na kesi ikafika nyumbani pia nikala bakora za kutosha hapo ndio nikapewa uangalizi maalum nyumbani pamoja na shule
Nyumbani nilipewa uangalizi wa kutopewa uhuru ule kama mwanzo kama nataka kucheza au kutoka nje basi niwe na kaka zangu mbali na kaka zangu siluhusiwi kwenda zaidi zaidi nibaki ndani na dada wa kazi
Shule nilipewa uangalizi na mwalimu wa darasa muda wote anataka niwepo darasani pia nikakabidhiwa mtu wa kunifundisha kusoma na kuandika alikuwa ni dada mmoja hivi mweupee anaitwa Aisha(jina halisi)
Maisha ya shule yaliendelea na Aisha alikuwa kila siku ananifundisha kusoma na kuandika coz yeye ndio alikuwa kinara wa darasa kipindi hicho na nilikuwa namuelewa sana coz alikuwa ananifundisha kwa uporeeee
Maisha yakaendelea nikaanza kuimprove katika swala zima la elimu baada ya miezi mi 2 nikawa najua kusoma na kuandika kiasi sikuwa zoba kama mwanzo ikafika mwezi wa 11 tukafanya mtihani wa kufunga shule nilikuwa wa 57 kati ya wanafunzi 74 na Aisha alikuwa ndio wakwanza rafiki zangu ambao nilikuwa naludi nao nyumbani mmoja alikuwa wa 5 mwingine wa 7 mwingine wa 12 so njiani walikuwa wananicheka mimi tu hii iliniuma sana nikajiapiza kuanzia darasa la 2 nitawanyosha
Likizo ile ya mwezi wa 12 nilitumia vizuri sana kwa kujifunza kusoma na kuandika kwa ufasaha hii kazi alikuwa anaifanya kaka yangu mkubwa alinifundisha kwa moyo wote
Nilivoelewa kusoma na kuandika akaanza kunifundisha na hesabu za kawaida zile za la kwanza pamoja na za la pili LIKIZO IKAISHA HIVO
MAISHA YANGU YA DARASA LA PILI MPKA LA SABA
Baada ya kurudi shule baada ya likizo kuisha nilibadilika sana Aisha ndie alikuwa desk mate wangu so alinifanya nipende shule pia hata darasani nikawa sishikiki tena kama sitakuwa wa kwanza basi wa pili wa kwanza Aisha tumepokezana hizi namba na Aisha mpka darasa la 5 hapa ndio wakaibuka vipanga wengine so competition ikawa kubwa but haikunizuia kuitetea namba yangu
Tulipo fika darasa la sita Aisha akahama shule na mkoa pia( baba yake alikuwa ni asistant lecture wa moja ya chuo kikubwa hapa Tanzania) so nikabaki mwenyewe
Nakumbuka kwenye competition za mitihani ya jumamosi na shule jirani nilikuwa nawaburuza sana shule jirani hasa kwa masomo kama sayansi na maarifa ya jamii nilikuwa sishikiki but hisabati nilikuwa siipendi so sikuwa na uhakika wa kuongoza pamoja na English japo kuna muda nilikuwa nawaburuza kwa masomo yote
Nilipofika darasa la saba niliendelea kukiwasha matokeo ya darasa la saba nilipata wastani wa A nikafauru moja ya shule kubwa pale jijini kwetu
Itaendeleaaaa