Du, mkuu Spurs ni kama Cosmo!, anyway sikulaumu. Ushabiki mwingi wa mpira wa EPL hapa Tz umeanza hivi karibuni ndio maana, lakini ungechukua hata jitihada kidogo kujua historia inasemaje juu vilabu vya ligi kuu England. Kwa kawaida hivi vilabu huwa vina tabia ya kupanda na kushuka, huwezi kuamini nikikwambia kuwa klabu unayoipenda wewe ilikuwa si lolote hapo miaka ya 80 tu. Spurs nayo ilikuwa na kipindi chake cha kujidai, hapa tunazungumzia kurudi kwa nyakati zile za Spurs kutesa.Kinachonishangaza ni mdau mwenzetu kushabikia Totenham,naona kama sinema vile mtu kushabikia Cosmo!
Asante sana mkuu pamoja wengine kuanza kutambua kuwa Spurs mean business!.ebwanaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa heshima zenu spurs simchezo leo.i salute guys na mnaweza kurudi kuendelea kupost comments manake nimeenda kutoa thread yenu pg ya 2.defoe nomaaa.
9-1 simchezo
Naona Shedafa karudu (kila spurs wakishinda). Hongereni ila hao Wigan ni shamba la bibi lol,ila Chelsea alikula kichapo.
Asante mkuu kwa pongezi, hii itabaki kuwa historia kwa muda. Ingawa Arsenal ndio anayejulikana kwa kutoa dozi za uhakika lakini hawezi kuifikia rekodi hii, si mwaka huu wala ujao.Baada ya ushindi mnono ni kawaida ya vijiwe kuchangamka ila si utani hawa jamaa wanapaswa kupongezwa kuchapa 9, mbili kasoro kila mchezaji aondoke na lake duh!
tatizo wachezaji wangu huwa wana mapozi sana na ubitozi unawaharibu wanataka kufunga magoli ya show game. kama wangetoa hizo mbwembwe hapo mbona goli 9 ingekuwa kawaida kwa arsenal kwenye mechi za kijinga jinga.Asante mkuu kwa pongezi, hii itabaki kuwa historia kwa muda. Ingawa Arsenal ndio anayejulikana kwa kutoa dozi za uhakika lakini hawezi kuifikia rekodi hii, si mwaka huu wala ujao.
Timu yenu haina tatizo pale uwanjani mkuu, tatizo liko nje ya uwanja. Watu wamegundua kuwa ni rahisi kuwachezea kisaikolojia na kuwafanya mpoteze morali, ndicho mnachofanyiwa. Kwa kuwa hamjagundua mtapata taabu, sababu kimsingi hakuna timu katika premier inayoweza kusimama mbele yenu kwa kutegemea mbinu za uwanjani tu. Wazo la kuwa na mtu mzima pale uwenjani linaweza kuwasaidia hasa mnapokutana na wapinzani wakubwa, bahati mbaya ugonjwa huu mmeambukizwa hata nyie mashabiki. Watu wanawaambia timu yenu bado nanyi mnakubali kuwa kweli bado, umefika wakati mkatae kuambia kuwa bado. Kwa maoni yangu mko katika peak!, hamna sababu ya kuzihofu chelsea wala Man U.tatizo wachezaji wangu huwa wana mapozi sana na ubitozi unawaharibu wanataka kufunga magoli ya show game. kama wangetoa hizo mbwembwe hapo mbona goli 9 ingekuwa kawaida kwa arsenal kwenye mechi za kijinga jinga.
kasi ya wachezaji wenu inatisha mkuu na ukikutana na beki iliochanganyikiwa mvua ya magoli ni kawaida.
Baada ya ushindi mnono ni kawaida ya vijiwe kuchangamka ila si utani hawa jamaa wanapaswa kupongezwa kuchapa 9, mbili kasoro kila mchezaji aondoke na lake duh!
Na mkitoa draw au kufungwa unapotea.
Ni majukumu tu hatukimbii mtani, sisi tunakwenda kwa malengo so far kila kitu kinakwenda vizuri au hujui kama ligi ikiisha leo na sisi tunacheza Champions league?
Hehehe si unajua utani hauendi bila kutaniana kidogo...kuna mtu mmoja sijamuona wiki ya pili sasa anaitwa Mbu, Makalangilo (Man City) naona jukwaa lake alilikimbia kabisa.
Mvina hongera kwa ushindi wa juzi.