TID awekwa jela mwaka mmoja

Amefungwa jela Mwaka mmoja na Mahakama moja ya Mwanzo Kariakoo baada ya kutiwa hatiani kwa kumshambulia mkazi mmoja wa Dar Khalid Mohamed.

Jina la kamili la TID ni Khalid Mohamed, sasa unataka kusema ameswekwa jela kwa kujidunda mwenyewe au ni coincidence tu?
 
Nazidi kupata News hapa....... Wakati anahukumiwa Alikua anatia huruma mno..huku wafungwa wenzake wakimuimbia Karibu Nyumba ya Mungu yenye Amani...akapanda kwenye Kalandinga huku wenzake waki mpeti peti...jamaa haamini kuwa ndio anaenda kuanza safari ya mwaka mmoja Gerezani ( Ila kiuraiani ni miezi sita) ...... so mpka sasa navyoituma hii post...T I d yuko Jela tayari..
 
Iende kwenye udaku...kuna maswali mengi kuliko majibu kwa sasa anapiga shoo..musoma..

Watu wanaenda kujirusha na nyota yangu...jela wapi na wapi?
 
Amefungwa jela Mwaka mmoja na Mahakama moja ya Mwanzo Kariakoo baada ya kutiwa hatiani kwa kumshambulia mkazi mmoja wa Dar Khalid Mohamed.

Haijulikani kama amekwenda Jela ama atalipa faini, lakini kwa kawaida Kosa kama hili mfungwa hupewa nafuu ya adhabu kwa kulipa faini na hasa kama utendaji wake wa kosa ni Mara ya Kwanza.

Lakini kama rekodi ndivyo inavyotaka kuoneshwa,atakuwa amekwenda jela maana anasifa ya kupiganapigana na aliwahi kuonywa, hata wakati wa Kili alitoa sambusa za makonde.

Ila kwa kawaida mahakama, huwa haioni umuhimu wa kumfunga mtu kwa kosa kama hili

Acha wakampe dose huko jela...lazima awe chakula ya wanaume huko!! Mtoto mrembo kabisa afu white...... yalah! Elimu nayo inamata wakuu.
Akirudi uraiani atakuwa amenyooka...
 
Hivi bongo hakuna zile adhabu za 'community service' au kifungo cha nje? au ni watu wa namna gani wanaopewa adhabu hizo? Kosa la kupiga nani hajawahi kufanya jamani? mbona Dudu baya amepiga watu sana, na akina nature walisambaza kinyesi nyumbani kwa Temba!
anyway inaweza kuwasaidia kupunguza ua kuacha bangi wasanii wengine.
 
Kama ilivyowekwa kwa Michuzi naiwakilisha hapa........

MSANII maarufu wa muziki wa kizazi kipya (Bongofleva), Khalid Mohamed maarufu kama T.I.D jana amehukumiwa kutumikia kifungo cha mwaka mmoja jela kufuatia kupatikana na hatia ya kushambulia na kujeruhi.
T.I.D mwenye umri wa miaka 26 alisomewa adhabu yake hiyo na Hakimu Hamisa Kalombola wa Mahakama ya wilaya ya Kinondoni baada ya Hakimu huyo kuridhika na ushahidi ulitolewa na mashahidi wanne walioletwa mahakamani na upande wa mashtaka.
Baada ya kusikiliza ushahidi huo, ndipo Hakimu Kalombola alisema ushahidi uliotolewa na mashahidi hao wanne ulithibitisha mtuhumiwa kufanya kosa hilo na hivyo mahakama inamtia hatiani kwa kosa hilo.
Mara baada ya kusema hivyo Hakimu alitoa nafasi kwa Mwendesha Mashtaka, Inspekta wa Polisi, Benedict Nyagabona ambaye alimwomba Hakimu kutoa adhabu kali kutokana na tabia iliyokithiri ya watu kujichukulia sheria mkononi kama alivyofanya mshtakiwa ili iwe fundisho kwa wengine wenye tabia kama hiyo.
Baada ya maelezo hayo ya Mwendesha Mashtaka ndipo Hakimu alitoa nafasi kwa mshtakiwa TID kutoa utetezi wake, ambaye aliiomba mahakama imhurumie kwani alitenda kosa hilo sababu ya ulevi na kuwa familia yake inamtegemea hasa mama yake.
Hata hivyo Hakimu Kalombola alitoa hukumu hiyo kwa kumwambia mshtakiwa "kwa vile huwezi kujimudu ukilewa na huwezi kujizuia kunywa sasa na kuhukumu uende jela mwaka mmoja ujifunze ili usiwe unakunywa hizo pombe"
Baada ya hukumu hiyo ambayo ilipokelewa kwa mshtuko mkubwa na msanii huyo aliyeng'ara sana katika fani hiyo ya muziki wa Bongofleva akiwa na bendi yake ya Top Band, ndugu na jamaa zake waliangua kilio mahakamani hapo wakati TID akipelekwa kwenye karandinga tayari kwenda kutumikia kifungo hicho katika gereza la Segerea.
Wakati akipelekewa kwenye karandinga hilo, TID aliishiwa nguvu na kuanguka mahakamani hapo na kubebwa na wenzake ambao baadhi yao walikuwa wamekwisha hukumiwa na wengine bado wakiwa watuhumiwa na kumwingiza kwenye gari hilo.
Kwa mujibu wa Mwendesha Mashtaka, Inspekta Nyagabona, T.I.D alimjeruhi Ben Mashiba kichwani na mkononi kwa kutumia chombo cha kuwekea majivu ya sigara 'Ash Tray' na alisomewa mashtaka hayo mara ya kwanza Julai 10 mbele ya Hakimu Kalombola. .
Mwendesha Mashtaka huyo aliiambia mahakama kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo Julai 2 mwaka jana saa sita na nusu usiku katika hoteli ya Slipway iliyopo maeneo ya Msasani jijini Dar es Salaam .
 
hapo ndo ninapokukubali kamanda wangu kana ka nsungu.
coz mambo ya udaku udaku yasiyokamilika we huna nafasi nayo.
thanks kwa kuingia chimbo na kutuletea taarifa yenye harufu ya ukweli.
 
TIDjela.jpg

Habari zaidi kuhusu hukumu ya huyu bwana mdogo ziko hapa Mwananchi

Msanii maarufu TID atupwa jela mwaka kwa kujeruhi

Mwanamuziki wa kizazi kipya au Bongo Fleva,Khalid Mohammed au TID yaani 'Top In Dar' ameanza kutumikia kifungo jela mwaka mmoja baada ya kupatikana na hatia mahakamani.
Na Elizabeth Suleyman

MAHAKAMA ya Wilaya ya Kinondoni imemhukumu kifungo cha mwaka mmoja jela msanii wa muziki wa kizazi kipya, Bongo Fleva, Khalid Mohammed 'TID' baada ya kutiwa hatiani kwa kujeruhi.

TID, 26, mkazi wa Kinondoni Hananasif, Dar es Salaam alitiwa hatiani jana katika mahakama hiyo iliyokuwa imefurika watu mbalimbali, wakiwamo ndugu wa msanii huyo, wazazi na baadhi ya marafiki zake, wote wakitaka kujua hatima ya msanii huyo.

Hakimu mfawidhi wa mahakama hiyo, Hamisa Kalombola kabla ya kutoa hukumu hiyo alisema kwamba kesi hiyo, kwa upande wa mlalalamikaji ilikuwa na mashahidi wanne na ushahidi waliota mahakamani, umeonyesha wazi kuwa msanii huyo alitenda kosa hilo.

Hakimu Kalombola aliendelea kusema kuwa, kulingana naushahidi uliotolewa umeonyesha wazi mtuhumiwa alitenda kosa kwa makusudi, hivyo kuishawishi mahakama kumtia hatiani.

Kwa upande wa mshtakiwa hakuwa na shahidi , kwani shahidi aliyepaswa kutoa ushahidi alielezwa kuwa alikuwa ni rafiki yake wa kike ambaye alikuwepo katika tukio, lakini ilielezwa mahakamani hapo kuwa alikuwa safari na hivyo kumsababisha rafikie kukosa shahidi.

Kabla ya kutoa hukumu, mahakamani hapo, Hakimu Kalombola alisoma maelezo ya awali ambako ilidaiwa kuwa Julai 2 mwaka jana , saa 6:30 usiku katika Hoteli ya Slipway, eneo la Masaki wakiwa katika ukumbi wa burudani, mtuhumiwa alimpiga mlalamikaji Ben Mashibe kwa kutumia trei la chupa za bia na kumsababishia maumivu makali.

Ilidaiwa kuwa kitu kilichomsabisha msanii huyo kuanzisha fujo ni kutokana na begi alilokuwa ameshika rafiki wake huyo wa kike,kutoonekana kwa muda huo, hivyo kusababisha watu waliokuwapo mahali pale ikiwa ni pamoja na mlalamikaji kuanza kushambuliwa.

Baada ya kusoma maelezo, Hakimu alimpa nafasi mtuhumiwa kujitetea, ambako alisema kwamba alikuwa amepitiwa siku ya tukio kutokana na pombe alizokuwa amekunywa, hivyo akaiomba mahakama iahirishe kutoa hukumu hiyo.

Mtuhumiwa alijitetea kuwa anayo familia inayomtegemea katika kuwalea, isitoshe mama yake mzazi hana kazi, naye pia anamtegemea kwa kila kitu.

Kwa upande wake, Mwendesha Mashtaka, Inspekta wa Polisi, Benedict Nyagabona alidai kuwa kutokana na ushahidi uliotolewa mahakamani umeithibitishia kuwa mtuhumiwa alitenda kosa, hivyo anastahili adhabu kali ili iwe fundisho kwa watu wengine.

Inspekta Nyagabona alidai kuwa kuwa kitendo cha mtuhumiwa kunywa pombe kupita kiasi hadi kuwasababishia watu madhara, ni kinyume na sheria, hivyo anatakiwa apewe adhabu kali kwa kuvunja sheria na pia kuleta madhara kwa jamii.

Hata hivyo, wakati akiondolewa mahakamani hapo, msanii huyo alionyesha dhahiri uso wa majonzi huku ndugu zake nao wakionyesha kufadhaika.

Kabla ya kupanda karandinga, TID alikabidhi mali zake ikiwamo simu ya mkononi kwa mtu ambaye alidaiwa ni msanii mwenzake, ambaye hata hivyo alisikika akimweleza asikate tamaa ya maisha, ataweza kumaliza kifungo chake.
 
hapo ndo ninapokukubali kamanda wangu kana ka nsungu.
coz mambo ya udaku udaku yasiyokamilika we huna nafasi nayo.
thanks kwa kuingia chimbo na kutuletea taarifa yenye harufu ya ukweli.

Thanks Kana Ka Nsungu kwa kutupa habari kamili za TID
Sasa naona wataanza kutia adabu sasa hawa wasanii
Bado Kikosi,Dudubaya na wenzao
 
Sidhani kama Assault pekee tu imempeleka jela kijana huyu, je ni kigezo gani kilichomfanya hakimu asitoe adhabu ya faini? hii ni sawa na kujaza magereza kwa kesi za wizi wa kuku,na kwanini kesi ndogo kama hii ilichukua muda mrefu bila kupewa nafasi ya kuongelewa nje ya Mahakama? Kwanini asipewe kifungo cha nje? Parole tunaomba wafanye kazi zao kuangalia haki za mhalifu huyu kwani adhabu ni kubwa kulingana na tulivyozoea kuona ndani ya mahakama zetu, nakuwa na wasiwasi sana na nguvu za Mlalamikaji kwa kuweka azimio au kushinikiza Hakimu ili adhabu fulani itolewe na hata kama baadaye atatoka lakini awe amewahi kuvaa gwanda la ukonga kwani watanzania ndivyo tulivyo na tumezoea hivyo wakati fulani
 
Sidhani kama Assault pekee tu imempeleka jela kijana huyu, je ni kigezo gani kilichomfanya hakimu asitoe adhabu ya faini?

Sasa wewe ulitaka hakimu afanyaje na kama ushahidi umetolewa na watu 4.
Ulitaka hakimu amhurumie?yeye mwenyewe kakili alitenda kosa kwa sababu ya ulevi kwa hiyo mahakama imemtia hatiani akakalie ndoo mwaka mzima ili iwe fundisho kwa wengine kama wewe unaye ona kama hawajamtendea haki hakuna mtu aliye juu ya sheria.Tena amehukumiwa kifungo kidogo ilitakiwa apigwe na faini juu na kuchapwa viboko.Linakuwa fundisho kwa vishololo vingine vinavyo tunanyanyasa mitaani.Na bado wengi tu wata mfuata huko kushika mic za wanaume.
 
KM,
Huyu TID sio kosa lake la kwanza kupiga watu, kama walivyo wanmuziki wengine kama Ze duduz,Kikosi n.k
Iliwahi kuripotiwa kuwa alikuwa na kesi mahakama ya kisutu kwa ubakaji, sijui hiyo kesi iliishaje.
Kwa upande wa pili adhabu ya kifungo cha mwaka mmoja jela ni sawa kabisa.Binafsi nimeshuhudia mtu wangu wa karibu akipigwa mvua kama hiyo ya TID kwa kosa kama hilohilo la TID.
Vilevile tukumbuke kuwa mahakama inao uwezo wa kumhukumu kifungo cha jela au faini ama vyote, lakini hiyo itategemea kama litakuwa ni kosa lake la ngapi.
Kwa mtazamo wangu, nadhani hakimu hakumpa option ya kulipa faini labda ana rekodi ya kutenda kosa/makosa kama hayo.
Labda wataalam wa sheria wanaweza kutusaidia kutoa ufafanuzi zaidi wa sheria iliyomhukumu, maana hapa JF wapo wengi tu,kama mtakumbuka mjadala wa ibara ya 30:5 ulivyojadiliwa kwa umahiri hapa.
 
Jamaa anasingizia ulevi...hahahaa vichekesho.
Bado akafanywe zeze tu huko segerea...kudadeki..cant imagine how its gonna be.
Pole sana T.I.D. be more careful next time you get yourself drunk and
start throwing tantrums!!!!
 
Masikini anatia huruma ila siku zote majuto ni mjukuu.... Pole akitoka sijui atakuwa wapi katika ulimwengu wa Mziki na nyota yake ilokuwa iking'ara:(
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom