The rise and fall of Colonel Muamar Gadaffi

..sawa mkuu, lakini CCM walichofanikiwa ni:
  1. Kudanganya wananchi na mataifa ya magharibi kuwa wanapendeka na wananchi
  2. Kikwete anawashauri wabovu au ubishi wake, kwani huwa hawamuambii hali halisi, wanachofanya
  3. Ni kuhakikisha wanaiba kura (kama walivyofanya igunga na kwenye halmshauri nyingene kwenye udiwani), halafu
  4. Wanamdanganya mzee tumefanya kazi mpaka tumeshinda,
Na hii ndiyo hatari tuliyo nayo kama taifa, "Watanzania ni waongo sana"
Uongo hufariji kwa muda fulani lakini ukweli huja kujulikana na ukweli umeanza kujulikana na ndio maana wadai mabadiliko wanazidi kuongezeka kila siku.
Bob Marley quated " You can fool some people for sometime but you cant fool all the people all the time" - Mambo yameshabadilika watanganyika wataki tena kufanywa wajinga
 
Wale Mabaeberu hatimaye wameweza kufanya waliyokusudia nacho ni kufurahia kutoa uhahi wa Shujaa wa Africa, Haitoshi wanaudhihirishia ulimwengu kwamba Unyama ndiyo jadi Yao, Muhamar Gadafi Daima utakumbukwa kwenye Historia ya Maendeleo na Mageuzi ya kisiasa na kiuchumi Barani Africa, Kapumzike salama Mbele ya haki wasalimie Nkuruma, Nyerere, Abdul Nasser,Chachage na Samola Machel, waambie Bara la Africa limetawaliwa na makuwadi wa Ubeberu Mamboleo. AMEN
 
hapa usa . Hao wote mnaowaona anchors wa channel hii mara hii wote wazazi wao ni walikuwa magovernor mara senator .
sasa mbona hawawashambulii
 
Gadaffi ni kati ya viongozi imara ndani ya afrika, hakika atakumbukwa milele, sikatahi ana udhaifu wake kama binadamu. Gadaffi alipenda nchi yake, alipenda bara la afrika, binafsi bora kuwa na kiongozi aina ya Gadaffi kuliko kuwa na mizoga kama; president Mwinyi, president Mkapa, na huyu ****** wa kujichekesha chekesha aliyezomewa jana udsm na bado wakamtunuku shahada!! Aibu tupu.
 
Kifo cha Ghadafi kimeacha pengo kubwa la kisiasa kwa Afrika.Ikumbukwe kuwa Ghadafi alikuwa ni mojawapo wa viongozi wachache sana Afrika aliyekuwa anaweza kuukemea ulimwengu wa magharibi pale ulipoonekana kutaka kuikandamiza Afrika.Ni kiongozi aliyekuwa amefanikiwa kuwaletea uhuru wa kiuchumi watu wake kwani Libya ni nchi iliyokuwa na deni dogo sana la nje ukilinganisha na nchi nyingine za Afrika na hata dunia kwa ujumla.Ni kiongozi aliyekuwa amefanikiwa kuwamilikisha watu wake rasilimali za taifa na watu wake wakanufaika nazo kwani licha ya nchi yake kuwa jangwani lakini maji halikuwa tatizo kama nchi nyingine za Afrika kwa kuwa alisambaza mabomba makubwa yanayovuta maji toka jangwani kwa umbali wa zaidi ya kilomita elfu moja.Alianzisha ujamaa wa kiarabu kwa serikali kutoa huduma mbalimbali kwa wananchi bure ikiwa ni pamoja na kutoa ujira wa kujikimu kwa wasiokuwa na ajira yaani UNEMPLOYMENT PAY.Nje ya mipaka ya nchi yake pia alikuwa mhisani.SWALI,Ni na nani anayeweza kuisemea Afrika?KWAHERI MWANA WA AFRIKA!
 
MIAFRIKA haina maana inapelekwa tu kama mizezeta..yaani hakuna kitu kabisa haya mambo ya aibu sana Obama nakuchukia sana mjinga kabisa wewe
 
article-2051361-0E76175A00000578-996_634x837.jpg

Procession: Libyans have been flocking to the morgue, where Gaddafi's body was taken, and have been taking photographs of him


article-2051361-0E76195600000578-42_634x490.jpg

Dead: Gaddafi's son Mutassim was also killed in a firefight in Sirte today
 
Ujumbe gani?. Hauwezi kuilinganisha Gadaf na ccm. Pia Afrika tumempoteza kiongozi wa ukweli.

R.I.P Gadaf.

Mzee Pambaf!

Mijitu inayofikiri kwa kutumia Masaburi huwa haielewagi upesi.
Unaposema huwezi kulinganisha CCM na Ghadafi una maana gani? Ghadafi ametawala Libya kwa MIAKA 42, CCM wameitawala Tanzania kwa miaka 50 tangu enzi za TANU! Kwa maana hiyo CCM imekaa madarakani muda mrefu zaidi kuliko hata huyo Marhemu Ghadafi!

Mzee, for your information this is a very strong message to CCM and all other DICTATORS in Africa. Today is Ghadafy,Tomorrow is Mugabe and NEXT IS CCM. Lazima CCM hapa mpate somo kuwa KUNG'ANG'ANIA MADARAKA NI UJINGA,UPUUZI na UDIKTETA ambao hakuna mtu yeyote anaweza kuvumilia popote duniani. CCM na madikteta wote jueni kuwa watu tunataka mabadiliko na siku zenu zinahesabika.

Pamoja na Ghadafi alikuwa anawapa watu wake Elimu,Afya,Maji,Umeme na KUOA bureee kwa miaka hii 42 bado wamefikia mahali wakasema HAWAMTAKI maana YEYE ALITAKA KUIFANYA LIBYA NI MALI YAKE!CCM mmeitawala nchi hii kwa miaka 50 LAKINI mpaka sasa Tanzania hakuna Elimu,Afya,Maji wala Umeme BURE achilia mbali mambo ya kuoa!

Now,if that is the situation who is/was very likely to go before the other? Definitely is CCM! Ghadafi stays 42 years in Power with all necessary needs given FREELY to all Libyans. CCM is now 50 years in Power with all necessary needs NOT availed FREELY to NOBODY achilia KUTOPATIKANA kwa hizo huduma muhimu!!

CCM jiandaeni kufungasha virago mapema before 2015. Muziki wa 2015 hamtauweza asilani.

Mungu ibariki Tanzania.Mungu ibariki Africa.
 
Tusichanganye mambo! Ulaya na Marekani ni marafiki wa CCM sababu wana maslahi hapa Tanzania..

Msijidanganye hata siku moja kuwa Nato na US kuna siku wataitoa madarakani CCM kama walivyomtoa Gaddafi
 
Libya hapo baadae watamkumbuka gaddaf kwa mengi ...

Kwa jinsi alivyo-deal na wapinzani wake..,japo Ghadaffi allikuwa na nafasi kubwa tu ya kuzuia haya yote lakini akaishia kuwatukana,kuwadharau,kuwaweka kizuizini au na hata kuwaua wale wote waliokuwa na mtazamo tofauti naye, hakufanya hivyo.Kitu gani kilimshinda kuwaita na kukaa nao kujadiliana ni jinsi ya kuendesha nchi yao? Mwisho wa siku pamoja na NTC kusaidiwa na NATO bado kulikuwa na kachembe ka Ghadaffi kuchokwa na raia wake wakichochewa na mapinduzi yaliyotangulia ya Tunisia na Misri...
 
Tusichanganye mambo! Ulaya na Marekani ni marafiki wa CCM sababu wana maslahi hapa Tanzania..

Msijidanganye hata siku moja kuwa Nato na US kuna siku wataitoa madarakani CCM kama walivyomtoa Gaddafi

Chatu dume,

That is just a matter of time.

Osama was very close friend to the Americans. Even Ghadaffy for some time was a friend to the US!Sasa Osama na Ghadaffy wako wapi?Inaonekana hata hufanyi utafiti wa kutosha katika nyanja za kimataifa kisiasa na kiuchumi. Rejea mitandao ya WikiLeaks inavyoibua mauzauza ya viongozi wa Kiafrika na kwingineko!

Wewe subiri pale Tanzania tutakapoanza kuchimba MAFUTA na URANIUM yetu. Wenzako wanaangalia maslahi ya nchi zao na si vidampa kama CCM!
 
Wale Mabaeberu hatimaye wameweza kufanya waliyokusudia nacho ni kufurahia kutoa uhahi wa Shujaa wa Africa, Haitoshi wanaudhihirishia ulimwengu kwamba Unyama ndiyo jadi Yao, Muhamar Gadafi Daima utakumbukwa kwenye Historia ya Maendeleo na Mageuzi ya kisiasa na kiuchumi Barani Africa, Kapumzike salama Mbele ya haki wasalimie Nkuruma, Nyerere, Abdul Nasser,Chachage na Samola Machel, waambie Bara la Africa limetawaliwa na makuwadi wa Ubeberu Mamboleo. AMEN

Watanzania tuna matatizo ya kusahau haraka. Huyu unayemwita shujaa wa afrika ndiye aliyeshirikiana na Dictator Idd Amin Dada kuteka ardhi ya Tanzania na kuendesha vita iliyotugharimu maisha ya wananchi na askari na kubwa zaidi ilitugharimu uchumi ambao tumeshindwa kabisa kuurejesha katika hali yake ya kabla ya vita. Huyo shujaa wako wa afrika alifadhili vita za wenyewe kwa wenyewe kwenye nchi za Liberia na Ivory coast. Naomba usiwachafue mashujaa wa kweli wa africa kwa kuwachanganya na huyu gaidi na muuaji wa waafrika wasio na hatia. $@#...****???
 
Jana magamba na midictator mingine ilitokwa na jasho kuona Kanali akiomba msamaha kabla ya kuchinjwa . Hiyo ndio price ya mauzauza mnayowafanyia wananchi. And that is the power of people .
 
2011 ni mwaka wa historia kubwa sana ya ulimwengu huu....tumeshuhudia rais Behn Ally wa Tunisia na Hosni Mubarak wa Egypti wakitimuliwa ikulu
na wananchi wao. Tumeshuhudia rais Ghabo wa Ivory coast akitolewa shimoni alikojificha akiwa tumbo wazi na kufukuzwa ikulu....tumeshuhudia kifo
cha kiongozi gwiji wa magaidi duniani (Osama Bin Laden) alikamatwa,akauawa na kuzikwa baharini. Na jana tumeshuhudia kukamatwa kwa Ghadaffi
ndani ya karavati na kuuawa na wananchi wake!.....ama kweli mwaka 2011 una siri mzito sana kwa ulimwengu huu.
 
Chatu dume,

That is just a matter of time.

Osama was very close friend to the Americans. Even Ghadaffy for some time was a friend to the US!Sasa Osama na Ghadaffy wako wapi?Inaonekana hata hufanyi utafiti wa kutosha katika nyanja za kimataifa kisiasa na kiuchumi. Rejea mitandao ya WikiLeaks inavyoibua mauzauza ya viongozi wa Kiafrika na kwingineko!

Wewe subiri pale Tanzania tutakapoanza kuchimba MAFUTA na URANIUM yetu. Wenzako wanaangalia maslahi ya nchi zao na si vidampa kama CCM!

Wewe ndio nadhani ufanyi utafiti unadhani wazungu wapo kwa ajili ya kutetea watu? Huko ni kujidanganya kama wamepewa kuchimba migodi na CCM kwa miaka 99..

Jiulize kwa nini Nato na US hawajaenda kumtoa madarakani Mugabe? Hawana maslahi yoyote Zimbwabe..hivi unadhani Wazungu wapo tayari kufa kwa ajili ya kusaidia Waafrika?

Wazungu hawana chama sio CCM wala CHADEMA wenyewe wanataka mambo yao yaendee tu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom