Muammar Gaddafi

Konzo Ikweta

JF-Expert Member
Oct 3, 2013
735
1,464
NI OPERATION JERUSALEM, ILIYO MUINGIZA IKULU YA AL-SENUSIA, NA NI OPERATION BENGAZI (UNIFIED PROTECTOR) ILIOMFURUSHA IKULU KIFEDHEHA; MUAMMAR GADDAFI KIONGOZI ALIYE IJENGA NCHI KUTOKA JANGWA MPAKA KUWA BUSTANI ILIYOFAA KWA KILIMO.

Na Comred Mbwana Allyamtu
Saturday- 21/9/2019.
Marangu,Kilimanjaro -Tanzania.

Muammar Gaddafi ni kiongozi alieacha historia kubwa sana barani Afrika, moja ya mambo atakayo kumbukwa katika uhai wake ni kuiondoa taifa lake kwenye ufukara ndani ya jangwa mpaka ukwasi na maendeleo ndani ya taifa lilokuwa likinuka ufukara na umasikini wa kutupa, ni yeye aliye ibadilishwa nchi kuwa aridhi yenye rutuba yenye kuota mimea yote iotayo duniani, pia ukumbukwa kwa uhodari na misimamo mikali dhidi ya mataifa ya kibeberu.

Muammar Gaddafi alichukua madaraka kwa njia ya mapinduzi kwa kumpindua mfalme Idris l mwaka 1969, mapinduzi yale yaliitwa "White revolution au One September revolution" (tutaona baadae kwanini yalipewa jina hilo) mapinduzi hayo yaliyo muingiza madarakani Muammar Gaddafi yaliratibiwa na mkakati uliopewa jina la "Operation Jerusalem", hii Jerusalem ni mji ambao upo nchini Israel, ndani ya mji huo imejengwa hekalu kubwa inayo itwa Al-Aqsa, hekalu hili takatifu lilojengwa na mfalme Suleiman.

Hivyo wakati wa upangaji mapinduzi hayo Gaddafi aliona ni vyema mpango wake wote wa kutekeleza mapinduzi yale ayapatie jina la Jerusalem, alifanya hivyo kumanisha utakatifu wa mji wenyewe na kuyalinganisha na mapinduzi hayo, kwani yeye aliona kuwa mapinduzi hayo ni matakatifu ndio maana hata baadae yaliitwa White revolution kwakua haya kumwaga damu yoyote, lakini pili, operation hiyo ilipewa jina Jerusalem kwakua mpango wa kuinjini mapinduzi hayo yalitokana na chuki ya askali wa Libya kufatia mfalme Idris l wa nchi hiyo kuungana na Israel kwenye vita ya siku sita "Six day war" ambapo Israel ilishinda vita hiyo (hili tutaliona baadae).

Taifa la Libya ni moja ya mataifa ya kale huko ukanda wa kaskazini mwa Afrika, wakazi wake wa asili walikuwa ni kabila la Waberber ambao kiasili ni wafugaji wanaoishi ukanda wote wa kusini mwa Libya. Kutokana na kustawi kwa biashara ya ukanda wa kaskazini mwa Afrika (Sahala long distance trade) eneo hilo la Libya likashuhudia wahamiaji wageni wa kabila la Wafoinike upande wa magharibi na Wagiriki upande wa mashariki.

Hatimaye Libya ikamezwa na Dola la Roma miaka ya 370-420 AD, na Ukristo ukaenea sehemu yote ya kaskazini mwa Libya, baada ya dola hilo ya Roma kuanguka, Wavandali waliteka sehemu kubwa ya nchi hasa eneo la kaskazini na mashariki mwa Libya, katika karne ya 7 Waarabu walivamia ukanda wote wa Libya wakitokea Misri, waliingiza Uislamu na utamaduni wao. Mwaka 1551 Waturuki walifukuza Wazungu kutoka Tripoli wakatawala eneo hilo hadi karne ya 20.

Mapema mwanzoni mwa karne ya 20, nchi ilivamiwa na kutawaliwa na Waitalia tangu mwaka 1911 hadi 1941, kipindi hiki Italian alikumbana na kizuizi kikali kutoka vikosi vya Senusia vilivyo ongozwa na Omar Al -Mukhtal ambae hata hivyo alishindwa vita hivyo, baada ya vita ya pili ya dunia Libya iliangukia mikononi mwa Waingereza ambao waliitawala Libya mpaka mwaka 1951 walipo amua kuiacha nchi mikononi mwa mfalme Idris l.

Hadi kufikia miaka ya 1960s serikali ya Mfalme Idris l ilikuwa inapingwa vikali na wananchi wa Libya, staili yake ya uongozi ambao alijilimbikizia madaraka makubwa mno na familia yake ili aweze kufaidi utajiri wa mafuta wa nchi iliwachukiza sana watu wa Libya.

Ilifika kipindi suala la maandamano nchini Libya likawa la kawaida, Kila kukicha kulikuwa na mahali watu wanaandamana kupinga ufalme wa Idris l, watu waliandamana na kuvamia visima vya mafuta na kufunga shughuli zilizokuwa zinaendelea, Kosa moja kubwa ambalo mfalme Idris alilifanya ilikuwa ni kufungamana na nchi za magharibi, hii ilipelekea mwaka 1967 baada ya Misri kushindwa vibaya na Israel katika vita maarufu ya ''The Six Day War'' wananchi wa Libya wakaelekeza hasira zao kwa utawala wa Idris wakimtuhumu kuwa ni mshirika wa Israel.

Hii ikapelekea kuundwa kwa kikundi cha vuguvugu kilichoongozwa na Gaddafi, kikundi hicho kilipewa jina la "Free Officers Movement" kikundi hiki kiliongozwa na maafisa kadhaa wenye ngazi za kawaida jeshini ambao walikuwa na fikra za vuguvugu la kiarabu (Arabic nationalism) kikundi hiki kiliundwa Ili kuijinia vuguvugu la kuupinga utawala wa mfalme Idris l kufatia utawala wake kuonekana ukiunga mkono utawala wa Israel, hata hivyo kikundi hicho kilizidi kuungwa mkono na askali wengi jeshini na raia mtaani japokuwa kiliratibu mambo yake kwa siri mno.

Japo kuwa CIA wamekanusha sana, lakini upo ushahidi wa kutosha kuonyesha kwamba walikuwa wanajua nyendo za Gaddafi na vuguvugu lake la Free Officers Movement, moja ya ushahidi ulikuja kutolewa na Uingereza mwaka 1970 kupitia shilika la kijasusi la nchi hiyo M16 likiitaja CIA kujua karibu mikakati yote ya kundi hilo la "Free officers movement", lakini wenyewe CIA wanakanusha na kusema kwamba wao waliyekuwa wanamfuatilia nyendo zake ni, Abdul Aziz Shelhi kiongozi wa kikundi kingine cha vuguvugu kilichoitwa "Black Boots" na sio Muammar Al Gaddafi.

Katikati ya mwaka 1969 nchi ikiwa bado haiko kwenye utulivu kutokana na maandamano ya kila kona, Mfalme Idris akasafiri kuelekea nchini Uturuki na Ugiriki kwa ajili ya mapumziko ya msimu wa joto bila kujua kuwa kuwa hiyo ndio safari yake ya mwisho kurejea nchini Libya, Gadaffi na washirika wake wa Free Officers Movement ambayo sasa ilikuwa na wafuasi wengi jeshini na hata uraiani waliona hii ni fursa adhimu kutimiza matarajio yao na ya wananchi wa Libya, ndipo hapa Gaddafi akaongoza wafuasi wake kutekeleza oparesheni ya kijeshi ambayo aliita *"Operation Jerusalem"*.

Siku ya Tarehe 1, September 1969 Gaddafi alitawanya wafuasi wake kuteka sehemu zote za kimkakati kwenye miji ya Tripoli na Benghazi maeneo muhimu mno kwenye nchi ya Libya, washirika wake waliteka viwanja vya ndege, vituo vya polisi, vituo vya redio na majengo ya ofisi za serikali kwenye miji hiyo, yeye mwenyewe Gaddafi aliongoza kikosi ambacho kilienda kuteka kituo cha kijeshi cha Berka mjini Benghazi eneo ambalo baadae linalokuja kubeba historia kubwa ya kumuondoa madarakani.

Rafiki yake Omar Meheisha aliongoza kikosi ambacho kilienda kuteka kituo cha kijeshi cha Tripoli. Na swahiba wake mkubwa wa tangu utotoni walipokuwa shule ya sekondari, Abdul Salam Jalloud aliongoza kikosi kilichoenda kuteka mitambo ya kijeshi ya kudungua ndege (antiaircraft battery) iliyopo Tripoli, mpaka hapo karibu sehemu muhimu zikawa zimedhibitiwa chini ya vikosi vya Free officers movement.

Pia Gadaffi alituma kikosi kilichoongozwa na rafiki yake aliyeitwa Khweldi Hameidi kilichoenda kumkamata Mwana Mfalme (crown Prince) Sayyid Hasan ar-Rida al-Mahdi as-Sanusai, huyu ndiye alikuwa anatarajiwa kumrithi baba yake Mfalme Idris l. Baada ya kukamatwa akalazimishwa kuikana hadharanj haki yake hiyo ya kurithi ufalme kutoka kwa baba yake, mwana mfalme huyo alikana hilo hadharani na kisha kuamriwa kuondoka nchini, ambapo alitorokea ufaransa kisha Uingereza.

Mpaka hapo mapinduzi yakawa yame kamilika na mpaka kufikia hatua hii ya zoezi hili la mapinduzi, hakukuwa na damu yoyote iliyomwagika (hakukuwa na vifo vya watu katika maeneo yote mapinduzi yalipo fanyika), hii ndio sababu iliyopelekea mapinduzi hayo huko mbeleni kujulikana kama "White Revolution" kabla ya hapo baadae kubadilishwa jina na kuitwa "One September Revolution" ili kuakisi siku hii muhimu ambayo Mfalme Idris l na utawala wake waliondolewa kutoka madarakani kwenye hekalu la kifalme la Al-Senusia lililopo Jijini Tripoli.

Baada ya sehemu zote hizi za kimkakati kutekwa na kuwa chini ya washirika wa Free Officers Movement, huu ukawa ni muda muafaka kabisa kufanya hatua inayofuata, Gaddafi akaelekea moja kwa moja mpaka kwenye kituo cha Radio cha taifa kuwajulisha ni nini kimetokea kwenye nchi yao, ni siku hii ya tarehe moja September 1969, kwenye Redio ya taifa… Muammar Gadaffi akautangazia umma wa Libya kuhusu mapinduzi ya kumng'oa madarakani Mfalme Idris na na kuufuta utawala wa kifalme nchini humo.

Katika hatua hiyo Gaddafi akiwa ameambatana na maafisa wenzake wa jeshi walio unda Free office's movement walitoa hutuba kuifahamisha umma na dunia kwa ujumla juu ya mapinduzi yale, hutuba hiyo ilitolewa na Muammar Gaddafi mwenyewe kiongozi wa mapinduzi hayo yaliyopo ratibiwa na kuinjiniwa na mpango mkakati (operation) iliyoitwa operation Jerusalem, katika hutuba hiyo Ghadaffi alinukuliwa akihutubia kwa wananchi kupitia radio, siku ya mapinduzi, September 1, 1969.

"Watu wa Libya! Katika kuitikia matakwa yenu, matarajio ya ndani ya sakafu za mioyo yenu, kujibu mnachohitaji juu ya mabadiliko na kufanya upya kwa kizazi chetu, na kujibu kilio chenu cha siku nyingi ili kukomeshwa kwa udhalimu… hatimaye leo hii majeshi yenu ya ulinzi, yameondoa madarakani utawala wa kifedhuli uliotukandamiza sote kwa kipindi kirefu sana.! Kwa pigo moja tu na mkupuo mkoja tu majeshi yenu tumeondoa miungu watu na kuharibu sanamu zao. Kwa ligo moja tu tumeweza kuleta nuru kwenye giza nene la muda mrefu ambalo kwanza ilianza kutamalaki kwa uturuki, kisha ikaja kutawala kwa Italia, na kisha utawala huu dhalimu ambao si chochote zaidi ya wanyonyaji, watesaji, wadhalimu na wahaini.! Wananchi wa Libya leo hii Libya mpya inazaliwa.!"

Baada ya hutuba hiyo Mapinduzi yalikamilika rasmi, kesho yake Gaddafi akatangaza baraza la utawala la kijeshi ambalo kiongozi mkuu akiwa yeye, alihaidi mageuzi mengi ndani ya nchi, Gaddafi alisisitiza kuwa ili Libya istawi anahakikisha kuwa atatimiza majukumu yote yaliyo mbele yake ili kuijenga upya Libya kwa misingi ya tamaduni na imani yake, kuindoa kuwa kibaraka wa magharibi, na pia muhimu zaidi kuhakikisha kwamba wananchi wote wanafaidi matunda ya utajiri wa mafuta ambao nchi yao imejaaliwa.

Safari ya matumanini ya kuijenga upya Libya ikaanza chini ya utawala wa Muammar Gaddafi ambae baada tu ya kuingia madarakani alifanya mabadililo makubwa sana ya kimfumo na utawala wa Libya, kwanza kabisa alibadili kikundi chake cha vuguvugu cha Free Officers Movement na kuwa Revolutionary Command Council (RCC) ambayo ndiyo ikafanyika kuwa serikali mpya ya Libya, Muammar mwenyewe ndio akawa Mwenyekiti wa balaza la kijeshi la mapinduzi la RCC, katika kipindi hiki mapinduzi yakifanyika Muammar Ghadaffi alikuwa na cheo cha kijeshi cha Luteni, na akajipandisha cheo kutoka Luteni mpaka Kanali, sambamba na wenzeka watatu wakawa makanali.

Baada ya hatua hiyo akajitangaza kuwa mkuu wa nchi na Mkuu wa majeshi, pia akamchagua rafiki yake wa miaka mingi tangu utotoni Jalloud kuwa Waziiri Mkuu, Baraza lake la kwanza la mawaziri lilitokana na vijana kutoka jeshini na uraiani ambao walishiliki katika mapinduzi ya White revolution.

Ikumbukwe kwamba katika kipindi hiki cha mapinduzi, Muammar Gaddafi alikuwa na miaka 28 pekee hivyo alikuwa kijana mdogo, vivyo hivyo na marafiki zake wa RCC (ambayo ilikuwa Free Officers Movement) nao walikiwa ni vijana wadogo waliotokea familia za hali ya chini na wachache wa kipato cha kati, kwahiyo baraza lake la kwanza la mawaziri liliundwa na vijana wadogo, ambao karibu wote hakuna ambaye alikuwa amemaliza chuo kikuu.

Hivyo basi mwezi May 1970, serikali ya Gaddafi ikaitisha kongamano maalumu la wasomi ili kuwashawishi kuhusika katika serikali yao mpya, baada ya hapo akaanza kufanya mabadiliko ya kimfumo katika taifa la Libya, katika kuifuma upya nchi, akaanza na kuhamisha makao makuu ya nchi kutoka mji mkuu wa nchi wa awali wa Al-Beida na kuuufanya mji wa Tripoli kuwa mji mkuu mpya wa Taifa la Libya, awali Tripoli ilikuwa ni eneo la bandari na makazi ya walowezi wa Kiingereza

Kisha akabadili katiba na kufanya "Sharia" ya kiislamu kuwa ndio sheria mama ya nchi (yani Quran ikawa ni sehemu ya katiba), pia akavunja vyama vyote vya wafanyabishara na wafanyakazi na kuunda chama kimoja cha umma kitakacho shughurikia maslahi ya wafanyakazi na wafanyabiashara, pia akapiga marufuku migomo ya aina yoyote ya wafanyakazi kwa muda wa miaka 20 Ili kutengeneza nchi (presidential decree to prohibt demostration) kisha pia magazeti mengi yakafungiwa kuchapishwa ili kuzuia mianya ya kupandikiza chuki dhidi ya utawala uliopinduliwa.

Katika harakati za mageuzi ndani ya serikali Ghadaffi mmoja ya matukio ya kukumbukwa ni lile tukio la Mwezi September 1971, pale Muammar Gaddafi alipo jiuzuru kwa kuto kufurahishwa na kasi ya mabadiliko ndani ya utawala wake lakini alirejea tena madarakani mwezi mmoja baadae, na kisha mwezi February mwaka 1973, Muammar Gadaffi alijiuzuru tena na akarejea tena ndani ya mwezi mmoja, japo baadhi ya wachambuzi kadhaa waliichambua hiyo kama mbinu za kujiimalisha zaidi madarakani kwa kutengeneza misingi ya huruma kwa umma.

Baadae Gaddafi akaanzisha Sera ya "Mapinduzi ya Kijani" (Green Revolution) ili kuleta mabadiliko makubwa katika sera ya kilimo na kupunguza utegemezi wa Libya katika kutegemea kuagiza chakula nje ya nchi, kwa hiyo ikatengenezwa mifumo na miundombinu thabiti ya umwagiliaji na kuongeza ardhi kubwa ya kilimo nchini Libya, mifumo hiyo iliendelea sambamba na uchimbaji wa visima virefu vya maji ambavyo ndio vilikuwa visima virefu zaidi duniani, visima hivyo vilichimbwa eneo lote la nchi mpaka kwenye maeneo ya jangwani, ikanunua udongo wenye rutuba Afrika mashariki hasa Uganda na kupandikiza nchini kwakwe ili kuongeza eneo lenye rutuba litakalo faa kwa kilimo.

Pia serikali ya Gaddafi ikawanyang'anya ardhi walowezi wa Kiitaliano na Waingereza na kuigawa kwa wananchi wa Libya huku pia serikali ikitoa ruzuku lukuki kwa wananchi na mikopo nafuu ya kufanyia shughuli za kilimo, lakini, kwa kuwa pia nchi ya Libya inategemea mafuta kama bidhaa kuu wanayouza nchi za nje, mwaka 1970 Gaddafi akavunja mikataba yote ya mafuta na makampuni ya kigeni akieleza wazi kuwa mikataba hiyo haikuwa inainufaisha Libya, nchi za magharibi zikaishutumu vikali kwa hatua hiyo ya kuvunja mikataba ikiambatana na vikwazo vikali dhidi ya utawala wa Libya.

Mwishoni mwa miaka ya 1970 karibia nchi zote wanachama wa OPEC wakaunga mkono juhudi hizi za Muammar Gaddafi na kupelekea kupanda kwa kiwango kikubwa cha bei ya mafuta duniani, hii ikapekekea taifa la Libya kusaini mkataba mashuhuri uliojulikana kama "The Tripoli Agreement", ambao ulisaidia Libya kupata gawio kubwa zaidi kwenye uchimbaji wa mafuta, hatua hii ikasaidia serikali ya Muammar kupata zaidi ya dola Bilioni moja kutoka kwenye biashara ya mafuta katika mwaka wake wa kwanza madarakani kitu kilchopelekea serikali ya Ghadaffi kuanza kuijenga nchi yake upya kwa kuongeza miundombinu na huduma za jamii kwa kasi kubwa.

Baada ya Muammar kushuhudia makusanyo makubwa hivi ya Kodi katika mafuta, mwaka uliofuata akaanzisha mpango wa kutaifisha makampuni yote ya mafuta nchini humo yaliyokuwa yanafanya kazi nchini humo. Kampuni ya kwanza kutaifishwa ilikuwa ni British Petroleum kampuni ya Uingereza, makampuni mengine yaliyosalia na yale ambayo yalikuwa yabakusudia kwenda kufanya shughuli za uchimbaji mafuta nchini Libya, zilipewa sharti la 51% ya hisa zake kuwekwa chini serikali ya Libya.

Hii ikapelekea kukua kwa pato la mwaka kutoka dola bilioni 3.8 waliyoikuta mwaka 1969 mpaka kufikia dola bilioni 13.7 mwaka 1974 na kupaa hadi dola bilioni 24.5 mwaka 1979, kukua huku kwa Pato la Taifa, kuliboresha haswa kuongezeka kwa hali za maisha nchini Libya, Mfano katika muongo wa kwanza wa utawala wa Muammar (mwaka 1979) wastani wa pato la wananchi kwa mwaka lilikuwa mpaka kufikia dola 8,170 kutoka dola 40 kwa mwaka 1951, kiwango hiki kilikuwa juu ya viawango vya wastani wa vipato vya wananchi katika nchi nyingi zilizoendelea mfano, UK na Italia kwa kipindi hicho.

Kadiri ambavyo Muammar aliimarisha uchumi wa Libya ndivyo ambavyo pia alijitahidi kuimarisha hali za kimaisha za wananchi wake, moja ya mambo aliyoanzisha katika kuboresha maisha ya watu wake ni pale alipoanzisha ujenzi wa makazi ya kuishi ya wananchi wake na kupandisha mishahara kwa 100% (mara mbili) ambapo serikali ilikuwa inakata 40% au 30% kama kodi ya makazi, pia akachochea na kuenzi desturi za Libya, kwa kufanya kiarabu kuwa lugha pekee rasmi ya kiofisi nchini humo, kiasi kwamba mpaka alama za barabarani alizibadili na zikaandikwa kwa kiarabu, huku mifumo ya mahakama na mifumo ya elimu ikafanywa kwa lugha ya kiarabu,

Pia akahamasisha uvaaji wa mavazi asili ya Kilibya, pia klabu zote na makanisa yakafungwa nchi nzima, jambo jingine lilofuata ni jambo ambalo wengi hawakulitegemea ni nia ya kukomesha kabisa utamaduni uliozoeleka nchini humo wa kuwakandamiza wanawake, Kwanza akapitisha sheria ya kuamuru usawa maeneo ya kazi kati ya wanawake na wanaume na usawa katika ujira, lakini pia sheria hii ikapiga marufuku wanawake kuolewa chini ya miaka kumi na sita, pia sheria hii ilipiga marufuku utamaduni wa waarabu kuwaoza watoto wao wa kike bila matakwa yao, chini ya sheria hii binti mwenyewe alitakiwa kukubali ndoa ndipo aozwe.

Chini ya utawala wa Gaddafi alifadhili kuanzishwa kwa Libyan General Women Federation, mabadiliko haya yalienda sambamba na mabadiliko katika sekta ya afya, kwani mpaka kufikia mwaka 1978 idadi ya hospitali nchini Libya zilikuwa zimeongezeka kwa 50% kulinganisha na mwaka 1968. Lakini pia idadi ya madaktari ilikuwa imeongezeka kutoka madaktari mia saba mwaka 1968 mpaka kufikia madaktari zaidi ya elfu tatu mwaka 1978, Libya pia ikafanikiwa kutokomeza magonjwa ya Malaria, trakoma na kifua kikuu ambayo yalikuwa tishio kwa kipindi hicho.

Elimu ya msingi ikaongezwa kutoka miaka sita mpaka miaka tisa, akajenga chuo kikuu cha Beida, na chuo kikuu cha Tripoli na Benghazi vikapanuliwa na Elimu kufanywa kuwa bure kwa ngazi zote toka elimu ya msingi mpaka chuo kikuu, lakini pia kwa miaka mingi Libya ilikuwa ikisumbuliwa na watu kubaguana kutokana na makabila na ukanda, hivyo basi kwanza kabisa Gadaffi akapiga marufuku viongozi wote wa kikabila nchini Libya na pia mipaka ya mikoa ikachorwa tena upya, ndani ya miaka kumi tangu Gaddafi kuingia madarakani aligeuka kuwa shujaa wa taifa kutokana na "miujiza" aliyoifanya kubadili mwelekea na hali ya taifa na wananchi wake.

Wananchi wa Libya wakaanza kumfananisha Muammar Gaddafi na Omar al-Mukhtar shujaa wa taifa la Libya wa miaka ya mwanzoni mwa 1900s ambaye kwa miaka ishirini aliongoza wananchi wenzake mashariki mwa Libya kupambana na ukoloni wa Waitaliano, ambae huko Libya hupewa heshima kama baba wa taifa la Libya

Wakati ambao wananchi wa Libya walikuwa wakimuona Muammar kama shujaa na mtu pekee mwenye uwezo wa kuijenga upya Libya, ambae kaitoa nchi kwenye jangwa na kuboresha uchumi wa nchi na raia wake mpaka kuifanya kuwa bustani yenye kufaa kwa kilimo, watu wa magharibi yani mabepari wao waliona ustawi wa Libya na kujiimalisha kwa Ghadaffi ni tishio na kuhatarishwa kwa maslahi yao, na hii iliwafanya waone kwamba kuna ulazima wa kitu kufanywa ili "kumdhibiti" Muammar Ghadaffi, kufatia hali hiyo mataifa ya magharibi yakaanza kuijinia mkakati wa kumuondoa madarakani.

Mpango wa kumuondoa madarakani Gaddafi ulianza kupangwa toka mwaka 1979, majaribio kadhaa ya kumuondoa madarakani yakafanyika, zaidi ya majaribio 20 yalizimwa yaliyotaka kumuondoa madarakani na karibu njama zote hizo ziliratibiwa na Uingereza na Marekani,mpaka kufikia mwaka 2002 serikali ya Gaddafi iliulaumu utawala wa Washington na London kupanga operation Convert section 6 ya kutaka kumuua, hata hivyo nchi hizo zilikanusha madai hayo.

Lakini ukweli ni kwamba mataifa ya magharibi yalikuwa yakipanga mikakati ya kumuondoa Ghaddafi madarakani kwani yalimtazama kama kikwazo katika mkakati wao wa kudhibiti soko la mafuta ukanda wa Afrika pamoja na kumuona kama adui wao kutokana na Gaddafi mwenyewe kuonekana kuwa mstari wa mbele kuunganisha Waafrika dhidi ya ubeberu na unyonyaji unaofanywa na mataifa ya magharibi, kwakua Ghadaffi mwenyewe alisisitiza kuchukuliwa mfano wa nchi yake namna alivyo wavusha wananchi wake kwa yeye kukataa kuwa kibaraka wa mataifa ya kibepari.

Taarifa za Pentagon, wizara ya usalama na jeshi la marekani inaeleza kuwa serikali ya marekani chini ya utawala wa Barack Obama ilitenga dollar za marekani $ billion 30 kufanikisha mkakati wa kumuondoa Muammar madarakani, kufatia hatua hiyo mataifa ya Marekani, Uingereza, Ufaransa na Canada yakaanza kuinjinia mkakati na mpango wa kuihujumu serikali ya Tripoli.

Mapema mwaka 2011 kuliibuka vuguvugu la mageuzi yaliyopinga utawala wa Gaddafi, vuguvugu hili safari hii liliongozwa na Mustafa Mohammed Abdul Jalil, taarifa za siri za serikali ya Libya zilimtaja Jalil kama agent maalumu wa CIA ambae aliandaliwa kupitia mkakati maalumu nchini Libya, ingawa serikali ya Marekani ilikanusha mwanzoni lakini baadae baada ya vuguvugu kupamba moto utawala wa Washington ulikiri kuhusika katika kuinjinia na kuratibu vuguvugu kwa kumuandaa Mohammed Abdul Jalil, jambo ambalo hata Obama alikuja kukiri na kuomba radhi kwa hatua ambayo Marekani ilichukua nchini Libya.

Wakati wafuasi wa vuguvugu liloipinga serikali ya Gaddafi wakiongozwa na Jalil walipoongeza maandamano dhidi ya utawala wa Gaddafi wakati huo, tayari Gaddafi alikuwa ameshatumia njia za nguvu kuyazima maandamano dhidi yake, maandamano ambayo baadaye yaligeuka na kuwa vita vya wenyewe kwa wenyewe, Mohammed Jalil alidai kuwa Gaddafi aliwakamata waandamanaji na kuwaua kikatili, hatua hiyo iliongeza hasira zaidi kwenye jamii za kimataifa.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na umoja wa mataifa, zilidai kuwa katika maandamano yale nchini Libya na machafuko yalioanza kupamba moto na kuzaa vita ya wenyewe kwa wenyewe ilipelekea karibu watu zaidi ya 30,000 waliuawa kwenye vita hivyo. Mara nyingi sana, Gaddafi alitoa matamko makali wakati wa vita hivyo dhidi ya viongozi walio ongoza vuguvugu hilo liloongozwa na Mohammed Jalil, ila linalojuilikana zaidi ni lile la kuwaita wapinzani wake kuwa ni panya.

Kwa kila hali utawala wa Gaddafi ulijaribu kuzima machafuko lakini wapi ndio kama ilikuwa ikiyachochea, yaliyotokea ni mambo ambayo hata Gaddafi mwenyewe hakuyatarajia asilani, kufatia hatua na machafuko kupamba moto ndani ya Libya, umoja wa mataifa kupitia azimio maalumu la balaza la usalama "United Nations Security Council Resolution 1973" wakaidhinisha kuivamia Libya kupitia operation BENGAZI (Operation Unified Protector).

Ndani ya operation hii ya Operation Unified Protector (Bengazi) mataifa ya Marekani,Uingereza, Ufaransa, Canada na Ujerumani yakatoa Majeshi kupitia operation ndogo zilizoitwa Operation Ellamy iliyo injiniwa na Uingereza (United Kingdom), Operation Odyssey Dawn iliyo injiniwa na Marekani, huku Canada ikiinjinia Operation Mobile, alafu Ufaransa ikaratibu Opération Harmattan, mpaka ilipofika December 2011 jumla ya gharama iliyotumika kufanikisha operations zote hizo inatajwa kufikia £212 million.

Mkakati huu wa Operation Unified Protector (Bengazi) ulifanikiwa kuufurumisha utawala wa Muammar Gaddafi ikiwa ni pamoja na kumuua Gaddafi mwenyewe ambae alikuwa akijaribu kukimbia kutoka katika eneo la Sirte, kwa mujibu wa mtu anayedaiwa kuwa alikuwa mlinzi wa Gaddafi kabla ya kumgeuka dakika za mwisho, saa 18 kabla kiongozi huyo wa zamani wa Libya kufariki dunia, alizitumia kusali na kuweka mikakati ya kuhama Jiji la Sirte, Mlinzi huyo alisema kuwa katika saa hizo 18 za mwisho, Gaddafi alizungumza na wanajeshi wachache waliokuwa wamebaki wanamlinda na kuwaambia kwamba hategemei kurudi kutawala Libya na hadhani kama ana maisha marefu.

Hata hivyo, Gaddafi “Aliwaambia wapigaji kwamba wakipata nafasi warudi kuitetea Libya na wasikubali vibaraka wa Marekani na Uingereza wafilisi mali za Walibya, mlinzi huyo alisema kuwa saa tatu kabla Gaddafi na timu yake, hawajaanza kutoroka, alizungumza na wanaye kwa muda mrefu lakini akawasisitiza: “Msiumie wala msifedheheke, wakati mwingine Shetani hutumia nguvu na kufunika haki dhidi ya batili.”

Operation Bengazi ambayo ndio iliyoratibu mauaji ya Gaddafi ilifikia tamati siku ya Alhamisi ya Oktoba 20, 2011, pale Gaddafi na timu yake, wakiwa kwenye magari ya kifahari, walikuwa wanahama kutoka Jiji la Sirte kuelekea mpakani, Inadaiwa walitaka kutorokea nje ya nchi, ingawa taarifa nyingine zinadai kiongozi huyo aligoma kuondoka na kusisitiza anangoja kufa kwenye ardhi aliyozaliwa.

Ilipo fika saa 2:30 asubuhi (saa za Libya), vikosi vya Nato na Ufaransa viliyashambulia kwa mabomu magari ya msafara wa Gaddafi. Magari 15 yaliharibiwa kwenye mashambulizi hayo, Gaddafi na timu yake walikwenda kujificha kwenye daraja la mtaro, saa 5:05 asubuhi, vikosi vya NTC ilitangaza kuwa ngome ya Gaddafi imekwisha na kilichobaki ni kutafuta masalia.

Mnamo saa 8:00 mchana, baada ya mapambano ya risasi kwisha, Gaddafi aligundulika yupo kwenye daraja la mtaro wa maji machafu amejificha, Ilipo fika saa 8:45 mchana mwanaume mmoja mkazi wa Sirte aliliambia Shirika la Utangazaji la Reuters kuwa alimuona Gaddafi akipigwa risasi tumboni kwa bastola yenye ukubwa wa 9 mm.

Ilipo fika saa 8:56 mchana, shirika la habari la Ufaransa Reuters ilitangaza kuwa Gaddafi alifariki dunia kutokana na majeraha baada ya mapigano ya risasi, mnamo saa 9:00 mchana, wapiganaji wa NTC walianza kuzunguka mitaani wanashangilia kukamatwa na kuuawa kwa Gaddafi, na ilipofika saa 10:31 alasiri, AFP ilitangaza kuwa mtoto wa Gaddafi, Muttasim amekutwa ameuawa jijini Sirte, na Ilipofika saa 11:52 jioni, mwili wa Gaddafi ulifikishwa Misrata.

Na majira ya saa 1:50 jioni, Aljazeera ilitangaza kuwa mtoto wa Gaddafi, Saif al Islam naye ameuawa kwenye mashambulizi hayo. Ingawa taarifa za baadaye zilisema kuwa Saif hakuuwawa ila tu alijeruhiwa mikono yake ambayo ilikatika vidole katika mashambulizi, na taarifa zilidai kuwa alifanikiwa kutoroka.

Mpaka kufikia hapo utawala wa Gaddafi ukawa umefikia ukingoni, neno la mwisho alilo sikika akisema Gaddafi kupitia simulizi za mlinzi wake ni kwamba Gaddafi alijitetea kwa maneno mengi ili asiuawe lakini kauli maarufu aliitoa kwa njia ya kuuliza, alisema “je, ninyi wanangu, mnaifahamu haki kwenye uongo? Naombeni msiniuwe nyinyi ni wanangu mimi ndio nimewalea hao wanawadanganya ili mniuwe wachukue utajili wenu”.

Na hii ndio ikawa mwisho wa hadithi za Muammar Gaddafi, kiongozi aliye ishi ndani ya matent, aligoma kuishi ikulu mpaka wananchi wake wa Libya wote wamiliki nyumba, raisi aliye wasomesha raia wake bure, aka waolea mabinti na kuwalipa mshahara na kuwafanya kuishi maisha bora kuliko hata raia wa mataifa ya ulaya, pamoja na yote hayo bado walimuua kama mbwa koko.....

Ukinakili kazi zangu kumbuka kufanya acknowledgment.
Wako Mjoli wa Historia na diplomasia ya ulimwengu.

Ndimi: Comred Mbwana Allyamtu (A. K. A Baba Farhat)

Copy rights of this article reserved
written by Comred Mbwana Allyamtu
•Napatika Kwa mawasliano
Comred Mbwana Allyamtu
Kwa Tanzania
+255679555526.
+255765026057.

Kwa Rwanda
+250733153930
+250788214234

Kwa DRC
+243 977 860 824

Kwa Msumbiji (Mozambique)
+27 874791033.
Email- mbwanaallyamtu990@gmail.com
 
Uandishi kama huu sijauona ndani ya JF kwa muda mrefu sana,ahsante mno mwandishi na hii ndio historia ya ukweli ambayo ni vema our next generations wakawa wanaifahamu ili wajue walikotoka,je swali moja kwa mwandishi M.Gaddaf historia itamwona kama ni moja wa ICON wa bara letu au ni Strong stateman?
 
Muamar gadafi simba wa afrika, walibya watajuta sana kumpoteza huyu mtu
 
Walimlalamikia Gaddafi sana, sasa wameona matokeo ya kuondoka kwake.

Safi saana mtoa mada.
 
Alifanya makubwa sana, a true definition of

A very good and atractive history...
 
noma
 
Back
Top Bottom