The rise and fall of Colonel Muamar Gadaffi

Mwiba

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
7,607
1,744
Habari za kuaminika zinadai kuwa Kiongozi Mkuu wa Libya Muammar Gaddafi amekalia kuti kavu, habari zinasema kuwa hali iliyofikia hairudi tena nyuma, nae atakurupushwa na kung'olewa kama shina la muhogo, kuna brigedi za kijeshi ambazo tayari zimeungana na wananchi, wazalendo wanasema wamefikia point of no return.

Hata hivyo upande wa Colonel Gadafi umezidisha nguvu na kutoa upinzani wa liwalo na liwe kama ni lawama iwe baadae kwa mikakati huo wanapiga risasi direct kwa wazalendo, habari zinazidi kutonya kuwa makao makuu ya Gadaf yaliopo Benghazi ambao ni mji wa pili kwa ukubwa, yameshachomwa moto na wananchi wanaelekea Tripoli ili kieleweke, kumbuka tu sasa kuna majeshi yalio pamoja na wananchi na wanatumia silaha na magari ya kijeshi katika kumng'oa Gadafi na mafisadi wenzake.

Vilevile muelewe kuwa Majeshi ya Gadaffi yapo katika mgawanyo, kuna kundi linaongozwa na mwanawe, hili ndilo ambalo linasemekana halitakuwa tayari kuachia madaraka kirahisi, hapo ndipo mapambano yatakapokuwa makali.
 
Haya kumekucha kumekucha.

Tunisia=Misri

Who is next?
Yemen or Iran?
Libya or Bahrain?
Tanzania or Uganda?
Zimbabwe or Ivory Cost?

Yetu macho
 
Hosni aliua watu 356 katika siku 18 za kumkataa, Gadafi kwa siku nne tu keshaua zaidi ya watu 200! Kama na yeye akifikisha siku 18 yatakuwa maafa makubwa sana. Mungu aepushe.
 
Protesters in Benghazi, Libya, send a car packed with explosives into a wall at a military camp, witnesses say. Security forces then fire on protesters as they attempt to breach the camp.
 
Hosni aliua watu 356 katika siku 18 za kumkataa, Gadafi kwa siku nne tu keshaua zaidi ya watu 200! Kama na yeye akifikisha siku 18 yatakuwa maafa makubwa sana. Mungu aepushe.
Kweli inaonyesha watu wengi sana watakufa.
 
Ghadaffi hana (mara)rafiki! sijui atakimbilia wapi? Wenzake Ben Ali na Mubarak angalau walikuwa na pakukimbilia.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom