The Bottom line ya sanaa ya kutongoza

Nakubaliana sana na Miss Juddy kwa theory yake ila nataka kuongezea mawili matatu hv ambayo yapo sana cku hz
1.Siku hizi kuwadi namba moja ni simu na email
2.Wadada wengi wenye upendo wa dhati huvutiwa na wanaume wa mvuto wao kama umbile,urefu,utanashati na caring
3.Wadada wasio na mapenzi ya kweli huangalia mshiko,aina ya maisha ya juu ya mtongozaji zaidi bila hata kujali vigezo vingine vya watongozaji
4.Kwa wanaume wengi utongozaji hutawaliwa na tamaa kwanza na mvuto wa mwanamke..fursa ikipatikana ndo utakuta wanaume wanaanza kufungua pazia la pili kujua mambo mengine kama elimu,tabia,kazi nk
5.Wapo pia wanaume wachache wanaotegemea mvuto wao kuwavutia wanawake mapenzini lakini hawa wengi huishia kuwaumiza wanawake mioyo ama hata kuwachuna...mfano vijana wa Congo na Nigeria
Ni mtazamo tu..hasa ukizingatia maisha ya sasa mapenzi yamekuwa cheap sana na aibu katika kutongozana haipo tena kama enzi zile alizokuwa anasoma Miss Juddy
nakupa big up kwa mada hii..natafakari nitumie mbinu ipi kati ya ulizotaja nikamilishe sanaa hiyo kwa kumpata ndege wangu,na ukizingatia ndege wa siku hizi wote wajanja mno kabla hujarusha jiwe yeye keshajua zamani nia yako!
 
Nakubaliana na wewe Miss Judith 100% Wanawake wanatongoza siku hizi si kama zamani ila sasa wao ni kwa vitendo si kwa maneno kama wanaume hiii imetulia sana
 
Nakubaliana sana na Miss Juddy kwa theory yake ila nataka kuongezea mawili matatu hv ambayo yapo sana cku hz
1.Siku hizi kuwadi namba moja ni simu na email
2.Wadada wengi wenye upendo wa dhati huvutiwa na wanaume wa mvuto wao kama umbile,urefu,utanashati na caring
3.Wadada wasio na mapenzi ya kweli huangalia mshiko,aina ya maisha ya juu ya mtongozaji zaidi bila hata kujali vigezo vingine vya watongozaji

4.Kwa wanaume wengi utongozaji hutawaliwa na tamaa kwanza na mvuto wa mwanamke..fursa ikipatikana ndo utakuta wanaume
Wanaume hupenda kwa macho si kwa moyo
 
Hii thread imekaa vizuri sana judith
tunategemea na nyingiene kutoka kwako:a s 112:




katika umri wangu wa miaka 26 nimetongozwa na hata kutongoza sana. Na kwa kweli napenda sana kutongoza na kutongozwa. Kwangu mimi kutongoza/kutongozwa ni njia ya kupanua mawasiliano miongoni mwa watu mbalimbali katika jamii. Hii ndiyo silaha ama nyenzo kuu inayosaidia kuanzisha mahusiano ya kimapenzi kati ya waume kwa wake ingawa siku hizi kutokana na mporomoko wa maadili, unaweza kukuta mahusiano ya jinsia moja.

Hapa najaribu kuweka wazi uzoefu wangu katika sanaa hii ambayo wengi wetu tumepitia. Kama una chochote cha kuongeza basi kitafaa sana. Pia nataka kuweka wazi mapema kuwa wanyama wote majike kwa madume hutongoza, ila hapa nitazingatia zaidi wanadamu.

Kutongozaa ni sanaa. Kama zilivyo sanaa nyingine zote kuna wanaoimudu zaidi yaw engine kutokana na utofauti wa vipaji mbalimnali. By definition naweza kuiita kuwa ni sanaa ambayo kwayo mtu anajaribu kupenya “ngome ya gereza” ambamo moyo wa mtu fulani umewekwa mahabusu. Hapa nataka wote tuchukule kuwa moyo ama nafsi ya mtu inayotakiwa kuridhia mapenzi ni sawa na mahabusu aliyefichwa kwenye gereza lenye ulinzi mkali na kuingia humo lazima hatua zote za usalama zichukuliwe ili kujiridhisha kuwa haitakuwepo hatari yoyote. Hatua hizi ni pamoja na kukaguliwa na kupekuliwa nk. Kwa hali ya juu sana na ikiwapo dalili ya wasiwasi wowote, basi anayetaka kuingia hurudishwa nyuma au kukataliwa kabisa. Sasa hapo ndipo kuna sanaa mbalimbali hutumika kuwahadaa walinzi walio kwenye mlango wa hilo gereza na wakati mwingine hujikuta wameruhusu hata watu hatari kuingia humo gerezani na wakati mwingine kuutesa huo moyo humohumo gerezani ulimofungiwa.

mbinu za mwanaume
imezoeleka kuwa mwanumme ndiye anayetongoza zaidi na mara nyingi hutumia mbinu mbalimbali kama mazungumzo, nyimbo, miluzi, barua/email/sms, zawadi kama pesa, outgoings za shopping, dinner, lunch nk., maua, nguo, picha, uturi nk na hata ishara za mwili mfano kukonyeza, kutikisa kichwa, shingo, kuumua na kukamua uso/mashavu, kufanya baadi ya mtindo kama ya nywele na ndevu, kukitakita miguu chini kujitekenya mwenyewe ama kumtenkenya mwenzie, kujieleza ama kujisifu, kulalamika, kulia ama kuomboleza kwa lengo la kuvuta hisia na huruma ya mwenzie,kuomba msamaha kujenga hisia za uadilifu, kutoa msaada kama kumbebea vitu kama ndoo za maji, mikoba, mizigo mbalimbali nk, kujiweka karibu kimawasiliano na hata kutoa msaada kwenye familia ya msichana, kuonyesha vituko, utundu au ufundi na uhodari katika mambo fulanifulani kama michezo mbalimbali kama riadha, kucheza ngma,muziki, mpira, kuimba hata games kama karata, bao, draft nk, kuonyesha uhodari mfano kwenye kilimo, biashara, uvuvi nk. Yoote hayo kwa lengo la kupenya ngome iliyohifadhi moyo wa msichana.

mbinu za mwanamke
wengi huamini kuwa mwanamke hutongoza mara chache, lakini hii si kweli. Wanwake hutongoza mara nyingi sana na huenda mara yingi zaidi ya mwanaume. Tofauti ni kuwa mwanaume yuko active zaidi na mwanamke hutongoza akiwa passive zaidi. Hata wanaume wengi (kadiri ya 47%)hutongoza wasichana ambao tayari walishaanza kuwatongoza wao. Hii hutokea pale amabapo mvulana alikuwa hajiamini au amejaa woga wa kumuanza msichana kwa kuamini kuwa huenda akakataliwa au hisia kuwa msichana matawi ya juu. Sasa kama binti kampenda atamuanza yeye kwa kujiweka karibu yake na soon mwanume atapata confidence na kurusha ndoano ambayohata isipokuwa na chambo itadakwa na binti na mwanume atakuwa akiamini kuwa altongoza na kufanikiwa kupata kiulaini, kumbe hali halisi ni kuwa yeye ndiye aliyetongozwa na kunaswa kiulaini!

Tena wanawake hufanikiwa kunasa mara nyingi zaidi ukilinganisha na wanaume. Inakadiriwa kuwa zaidi ya 92% ya wanawake wanaotongoza hufankiwa huku wanaume wanaofanikiwa wakiwa 67% pekee. Ni wazi wahenga hawakukosea waliposema kuwa simba mwenda pole ndiye mla nyama!

Wanawake hutumia mbinu kama be the first to call strategy, kukuomba no. Ya simu, email nk, hukuomba msaada hata pale ambapo hana shida kabisa na huo msaada mfano, vocha au misaada ya kimasomo anaweza kukuomba umsaidie swali fulani hata kama hilo swali analijua vizuri pengine zaidi yako. Katika nchi zingine msichana anaweza kukushika kiuno mnapotembea barabarani, hapa kwetu anaweza kukushika mkono huku akikutekenya kiganja cha mkono wako, au anaweza kuzungumza nawe huku akikutazama au hata kukuchorachora kwa vidole vyake kifuani au mkononi, anaweza kuvaa nguo fulanifulani mfano za rangi ya zambarau au nyekundu hutumiwa sana, kukutembelea chumbani au nyumbani kwenu bila taarifa (japo wakati mwingine kwa taarifa) zawadi mbalimbali (kama mwanaume hapo juu), mzungumzo, nyimbo nk (ingawa si active kama alivyo mwanaume)

naona niishie hapa na naamini licha ya kuwachosha kwa maelezo marefu, kwa kiasi fulani nimeshare nanyi kauzoefu kangu kadogo katika masuala haya.

Stay blessed & good day
judy
 
Sijawahi kutongoza, ngoja nijaribu.
Ahsante miss jud kwa maujanja.


hebu anza na mimi Hus, mi mwenyewe sijawahi tuone itakuwaje

Thanks Miss Judith, Nimekumiss (sijui ndo nimeshatongoza apo?)
 
hebu anza na mimi Hus, mi mwenyewe sijawahi tuone itakuwaje

Thanks Miss Judith, Nimekumiss (sijui ndo nimeshatongoza apo?)

haha, inawezekana umeishaanza kunitongoza tayari! but kumbuka kuwa ni mpaka uwe na intention ya kuingia kule gerezani ulikofungiwa moyo wangu ndo unakuwa unatongoza. kama unasalimia tu au kunijulia hali, it all about that and no more.

mi nipo mkuu japo nimekuwa bize sana siku za karibuni, but i am available. tupe experience yako binafsi juu ya sanaa hiii please, utatusaidia wengi
 
haha, inawezekana umeishaanza kunitongoza tayari! but kumbuka kuwa ni mpaka uwe na intention ya kuingia kule gerezani ulikofungiwa moyo wangu ndo unakuwa unatongoza. kama unasalimia tu au kunijulia hali, it all about that and no more.

mi nipo mkuu japo nimekuwa bize sana siku za karibuni, but i am available. tupe experience yako binafsi juu ya sanaa hiii please, utatusaidia wengi

me too miss Judith,

hapo nilikuwa namaanisha kwamba haiingii kwenye kategori ya kutongoza kwa kujali nk...yaani medani zile za kivita za kutongoza? na how do we know kwamba hapa ni salamu za kawaida tu nk,maana kwa upande mmoja, utachukulia ni salamu, upande mweingine unaweza ukawa 'hey.c;mon, this guy is up for something'

hivi hapa online unaweza kumtongoza mtu japo hujamwona...? In the strict sense? ngoja nipate uji narudi (mi bado mdogo)
 
Kwa maana fupi ya ujumla ktk hili mi naona ni kutongoza ni kushawishi ili kufanyiwa lile unalotaka. Hiyo ni ya kiujumla but unaweza kuispecify ktk mapenzi au hata ktk mambo mengine.

kama hiyo ndo maana(hapo kwenye red) then nimetongoza mpaka wasichana wenzangu.......
 
nimeipenda hii article, hasa pale ulipochambua mbinu za kutongoza za wanawake. Mimi napenda pale mwanamke anaponitongoza kwa kunipa ishara mbalimbali. anyway...ninacho-question ni hizo statistics zako tu dada! Hujaweka reference yeyote kutuonyesha zimetoka wapi...
 
Juddy nataka kujifunza practicaly uzoefu wako.......ebu jaribu kunitongoza please.
 
aiseee i was right about you.....

nashukuru sikuwahi kukutongoza......

siku zote niliona you are way smarter than you pretend to be....

sasa nimeona .......

thanx anyway...........

ningekutongoza pengine ungeni tumia as research case lol..........
 
Jamani kutongoza kazi zamani...siyo haya ya sms, chat....

Enzi hizo midume lazima nipagane mshindo ndio anapata demu au kwenda kuwinda simba kufanikiwa kumkill simba we kidume mademu wa kijiji wote wanakutafuta.....

Judith hebu jaribu kufanya analysis ya kwenye cultural/era dimensions.
 
Maxence Melo anasema "sharing is caring", i have shared with you what i have because i care for you all ma brothers and sisters. stay blessed!

Glory to God!
 
Mwanamke anayetongoza mwanaume anatumia nguvu nyingi, hali na mali, ili kuhakikisha huo uhusiano unasimama. Mahusiano machache yaliyoanza hivi hudumu.
 
Maxence Melo anasema "sharing is caring", i have share with you what i have because i care for you all ma brothers and sisters. stay blessed!

Glory to God!

Tunashukuru sana Miss Judith kwa elimu hii, ila sasa nafikiri hata nikimsalimu mkaka atasema namtongoza...lol!!
 
Tunashukuru sana Miss Judith kwa elimu hii, ila sasa nafikiri hata nikimsalimu mkaka atasema namtongoza...lol!!

HAHA, usijali dada Keren, usiache kusalimu kaka zako kwa kuhofia kuonekana unatongoza. kumbuka nimetumia mfano wa gereza lenye linzi mkali. siku zote walinzi hodari wanaojua vizuri kazi yao,hata wakiona mpita njia tu anageuzageuza shingo hma watamsaili wajue anatafuta nini maeneo yale hatari! so ni kawaida na usihofu, ni mvuto wa asili aliotukirimia Mwenyezi Mungu. kumbuka "kila mwanamke anavuta kushinda ulimbo. hakuna hata sumaku inayoweza kuvuta kama afanyavyo mwanamke". ndiyo maana mwanamke akimtazama mwanaume machoni direct mwnaaume hupata "hofu" hata kama ni mkewe aliyemzoea. I always glorify God when men flirt on me. Mungu ni mwema sana na mwingi wa rehema na uaminifu wake wadumu vizazi hata vizazi

Glory to God
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom