Sanaa shuleni

Feb 6, 2024
40
51
SANAA YA MUZIKI HAIPEWI NAFASI MASHULENI LIKIJA SUALA NZIMA LA UIPUAJI WA VIPAJI MASHULENI TOFAUTI NA ZAMANI..

Serikali imekuwa ikiimiza michezo mashuleni ili kuibua vipaji na kuendeleza , kuchochea ufaulu mashuleni na kuondoa utoro kwa wanafunzi...

wanafunzi hushiriki katika michezo mbalimbali kwa lengo la kuwajengea kujiamini na kudumisha urafiki miongoni mwao. Michezo inasaidia kujenga na kuibua vipaji vya wanafunzi..

Lakini vile vile kupitia michezo, vijana wanajitengenezea nafasi za ajira na kuondokana na tatizo la kusubiri kuajiriwa ambalo ndio Tatizo Kubwa sana linalolikabili Taifa letu kwa sasa.

Wahatimu ni wengi mtahani ambao wanauelewa/ tahaluma ya mambo mbalimbali , tahaluma ambazo zinaweza kulisaidia Taifa letu la Tanzania kukuwa kiuchumi bila kutengemea wasomi kutoka nje ?

Maana hapa kwetu Tanzania kuna sekta mbalimbali ambazo vijana wetu wa hapa hapa Tanzania wanaweza kufanya na kulitea Taifa tija kwa 100%.

Lakini KWA leo nilikuwa napenda kuzungumzia suala la kuibua vipaji kwa wanafunzi kwenye upande wa sanaa ya Muziki na hasa najikita kwa waimbaji ..

Imekuwa ikiaminika kila wakati hisabati, Kiingereza, na sayansi ni masomo muhimu na muhimu zaidi ya yaliyomo kwenye elimu. Wanafunzi ambao walikuwa mahiri katika kutatua shida na shughuli ndio waliangaza zaidi. Kwa upande mwingine, kulikuwa na wanafunzi ambao walipendelea muziki na sanaa lakini mara nyingi hawakujulikana sana maybe itokee sherehe ama hafla shuleni ndio walipewa nafasi Tofauti na hapo walimu na wazazi walikuwa wakiwanyima nafasi ya kufikia ndoto zao kwa kuwaeleza maneno ya kuwakatisha Tamaa.

Aina ya Sanaa ninayoiona kwa sasa ikipewa nafasi mashuleni ni uchoraji ( maana mara zote lazima kuna uhitaji wa uchoraji wa baadhi ya vitu muhimu Darasa kwenye masomo kama vile sayansi nk.) ..mchezo wa mpira wa miguu KWA upande wa jinsia ya kiume na 🥅 netball kwa upande wa jinsia ya kike.

Kilicho wazi ni kwamba masomo upewa nafasi zaidi kuliko sanaa. Na mara nyingi ukiona kijana ameendelea kipaji chake cha Muziki mara zote huwa ni juhudi zake binafsi kuna dhima ya jamii kuwa Muziki humfanya mwanafunzi kuwa muhuni Tofauti na sanaa zingine mashuleni.

inaonekana kuwa katika miaka michache muziki na sanaa hazitakuwa na nafasi katika mfumo wa elimu kwa kuwa kila wakati wana masaa machache na ndio kuwa hiari..

Kama ilivyo katika maisha ya kila binadamu huwa na ndoto ya kufanikiwa na kuwa na maisha mazuri hapa duniani, tumeona watu wengi kutoka katika maisha ya chini wakifanikiwa kupitia katika shughuli mbalimbali, zikiwemo biashara, ujasiliamali na hata kuajiriwa na taasisi mbalimbali pamoja na serikali, mbali na hivyo kuna watu wamefanikiwa katika shughuli za sanaa na muziki mfano; Jay z, Kanye West, Bob Marley, Michael Jackson, Ambwene Yesaya (A.Y), Hamisi Mwijuma (Mwana FA), Naasib Abdul (Diamond Plutnumz) Ally Kiba na wengine wengi kote. Kwahiyo muziki ni biashara kama ilivyo biashara yoyote ambayo mtu humwezesha kujipatia kipato kupitia biashara hiyo, mwanamuziki hujipatia kipato kutokana na kuuzwa kwa kazi zake, maonesho na hata kutangaza biashara za makampuni na taasisi. Kwahiyo mwanamuziki hupata pesa nyingi kupitia maduka ya kimtandao ambayo huuza kazi zake duniani kote..

#funguka mdau wa sanaa.

Kwanini Muziki HAIPEWI NAFASI MASHULENI
 

Attachments

  • images.jpeg
    images.jpeg
    27.5 KB · Views: 3
Back
Top Bottom