DOKEZO TCU tunaomba msaada, Chuo cha St. Joseph kinatoza ada na direct costs kwanza ndipo uweze ku-confirm udahili wako

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Leo tarehe 25.08.2023 TCU wametoa majina ya wanafunzi wa kidato cha sita waliochaguliwa kujiunga na vyuo mbalimbali.

Kama inavyojulikana, kuna ambao hupata "multiple selections", yani mwanafunzi mmoja anadahiliwa na vyuo zaidi ya kimoja kwa kozi tofauti au kwa kozi ileile.

Hii ni stage ambayo mwanafunzi amekuwa ameshalipia application fee, hivyo hategemei kutozwa gharama yoyote ile kabla ya kuripoti chuoni.

Cha kushangaza chuo cha St. Joseph University College of Health and Allied Sciences hawajaweka link ya kuconfirm kwa wale ambao wana multiple selections.

Ukiwapigia wanakupa sharti la kulipia installment ya milioni 2 na direct costs ya laki 5 ndipo wakupe link ya ku-confirm kitu ambacho kiko nje ya taratibu na miongozo ya udahili wa vyuo kwani kwa mujibu wa almanac ya TCU kwa sasa ni step ya confirmations kwa walio na multiple selections.

Hii step haihitaji ulipie chochote kwani mwanafunzi anakuwa ameshalipia application fee, sasa inakuwaje unamnyima access ya kuconfirm chuo mpaka alipie ada na direct costs wakati siyo utaratibu?

Tunaomba mamlaka zinazohusika zisaidie, kwani hii si sawa hasa ukiangalia bodi ya mikopo (HESLB) bado wapo kwenye mchakato wa kupokea maombi ya hawa wanafunzi.

Si sahihi kuwalipisha wanafunzi ada na direct costs muda huu angali michakato bado mibichi kabisa haijafika hata nusu.

============

Kitu kingine ambacho watu hawakijui hasa wanafunzi ni kuwa wale ambao wanapata nafasi ya kupata kwenye chuo zaidi ya kimoja wakati wa maombi, hata kabla ya mchakato wa Maombi ya Mkopo kukamilika, kuna michezo michafu inafanywa na vyuo mbalimbali.

Kuna source mmoja kutoka katika chuo kingine kilichopo Dar es Salaam anasema "Mara nyingi michezo hiyo tunaifanya sana sisi watu wa chuo na hata mimi ni mmoja wa watu tunaofanya hiyo michezo michafu.

"Ipo hivi, kama tukiona kuna mwanafunzi amefanya maombi na amechaguliwa katika vyuo zaidi ya kimoja, tunachokifanya tunaingia kwenye system na ku confirm kwa niaba yake, yaani kama yeye alichaguliwa chuo AA, BB na CC, sisi chuo chetu tunaingia kwenye mfumo na ku fonfirm kuwa ameridhia kusoka chuo CC.

"Yeye Mwanafunzi akiingia kwenye mfumo anakuwa haoni link ya ku confirm, anaishia kuona chuo kimoja tu ambacho ni hicho CC tulichomchagulia kwa niaba.

"Hilo linafanyika ili Mwanafunzi akose option ya kuchagua chuo kingine katyi ya vile ambavyo amechaguliwa na kama ni process zote anatakiwa kuzifanya kwa kuzingatia chuo kile kilichomchagua.

"Mfano vipo vyuo hasa vya private kama nilivyosema vinakulazimisha ulipe sehemu ya ada na gharama nyingine ili kupate confirmation kisha uendelee na harakati zako nyingine za kujiunga chuo na kupata mkopo.

"Ikitokea umepata mkopo na tayari umeshalipa, hiyo hela hairudi bali mtafidiana huko juu kwa juu.

"Hii michezo inafanyika sana tu na Wanafunzi na wasimamizi wao wanaishia kuteseka, mamkala za Serikali na hata hao TCU wapo tu hakuna wanachokifanya wakati wanajua kinachofanyika.

"Kuna vyuo vinajiona vina nguvu ndio maana wanavyanya wanayoyafanya ili kufanikisha nia yao."

Pia Soma > TCU yasema hakuna Mwanafunzi atakayelazimishwa kusoma katika chuo ambacho hakitaki
 
Leo tarehe 25.08.2023 TCU wametoa majina ya wanafunzi wa kidato cha sita waliochaguliwa kujiunga na vyuo mbalimbali.

Kama inavyojulikana, kuna ambao hupata "multiple selections", yani mwanafunzi mmoja anadahiliwa na vyuo zaidi ya kimoja kwa kozi tofauti au kwa kozi ileile.

Hii ni stage ambayo mwanafunzi amekuwa ameshalipia application fee, hivyo hategemei kutozwa gharama yoyote ile kabla ya kuripoti chuoni.

Cha kushangaza chuo cha St. Joseph University College of Health and Allied Sciences hawajaweka link ya kuconfirm kwa wale ambao wana multiple selections.

Ukiwapigia wanakupa sharti la kulipia installment ya milioni 2 na direct costs ya laki 5 ndipo wakupe link ya ku-confirm kitu ambacho kiko nje ya taratibu na miongozo ya udahili wa vyuo kwani kwa mujibu wa almanac ya TCU kwa sasa ni step ya confirmations kwa walio na multiple selections.

Hii step haihitaji ulipie chochote kwani mwanafunzi anakuwa ameshalipia application fee, sasa inakuwaje unamnyima access ya kuconfirm chuo mpaka alipie ada na direct costs wakati siyo utaratibu?

Tunaomba mamlaka zinazohusika zisaidie, kwani hii si sawa hasa ukiangalia bodi ya mikopo (HESLB) bado wapo kwenye mchakato wa kupokea maombi ya hawa wanafunzi.

Si sahihi kuwalipisha wanafunzi ada na direct costs muda huu angali michakato bado mibichi kabisa haijafika hata nusu.
😂😂😂 Wanataka wajihakikishie mapema

Ni upuuzi tu maana kulipa pesa chuo ni karibia na chuo kufunguliwa/usajili
 
Hivi chuo ni hicho tu?
Mbona vyuo vingi sana, achana nao waendelee na taratibu zao.
 
Ningekuwa na mamlaka kwenye hii nchi, elimu ingekuwa huduma. Madhara ya kuifanya elimu kuwa biashara ni makubwa sana,sijui kama wote mnayaona kama mimi ninavyoyaona.
Yes Mimi ni mmojawapo ndio maana nimewatoa watoto wangu English Mediums na kuwaleta Kayumba
 
Hapo HESLB jamani pana tatiza sana kwenye ujazaji wa maombi ya mkopo. Ukifikia stage ya DEMOGRAPHIC INFORMATION, kitu kina load tu , hakitumi.
Shida ni nini. Hata ukisubiri labda usiku itatulia , wapii, kwa wiki 2 mfululizo nimejaribu kila siku , na sijafanikiwa. Sijui nifanye nini ..
 
Birth verification number usisahau kuweka BV mwishoni pale chap tu
 
Back
Top Bottom