Kingsmann
JF-Expert Member
- Oct 4, 2018
- 4,448
- 16,313
Ni jambo la kushangaza kidogo lakini hali halisi ndiyo iko hivyo. Wanafunzi wanaosoma vyuo binafsi kada za afya wamenyimwa "Ada" huku wale wanaosoma kada zingine mfano ualimu wakipewa japo kitu kidogo.
Ndiyo mmewapa pesa ya kujikimu lakini kama mwanafunzi hawezi kujilipia ada yafaa nini?
Mtoto wa masikini amejifahidi kasoma science akiamini huko mbele anaweza kufika tamati kwa kupata mkopo kutoka HESLB kwani wazazi hawana uwezo. Ila mwisho wa siku anaishia kupata pesa ya kujikimu pekee huku akiachiwa zigonla ada la milioni 3 ambalo kamwe ni ndoto kulilipa hata wakichangishana ukoo mzima.
Nina mfano hai wa chuo kimoja kinachotoa Nursing na Pharmacy, awamu ya kwanza walipewa pesa ya kujikimu tuu. Dirisha la appeal lilipofunguliwa wameappeal ila hakuna hata mmoja aliyepewa ada. Hakuna hata mmoja.
Kada za afya huwa ni priority, ni nini kimetokea mwaka huu mpaka muwanyime hawa watoto ada?