TBC imemuita nani hamnazo?

Mbaga Jr

JF-Expert Member
May 28, 2018
19,104
41,610
Kwa walioangalia taarifa ya habari leo TBC watanielewa.

Kwa kawaida jina au neno ‘hamnazo’ linamaanisha mtu mjinga, mpumbavu pia asiye na akili timamu.

Leo baada ya Taarifa ya Habari ya TBC, huwa kuna kipindi nadhani cha dakika zisizozidi tano kiitwacho “Tafakuri” ambacho kinatangazwa na Shaban Kisu na huelezea mambo mbalimbali. Sasa, leo kipindi kilimuelezea mtu aliyepewa jina la “Hamnazo”.

Ndugu Hamnazo alikuwa ndani akiwa amevaa Msuli bila nguo yoyote ndani yake, akaamua kwenda shambani kwake huku akiwa bila viatu. Aliingia ndani ya shamba lake huku akikimbia na shamba lake limejaa mbigiri (miiba) hivyo mbigiri zile zilimchoma lakini ndugu Hamnazo aliendelea kukimbia kuingia katika shamba lake. Baada ya kuchomwa sana na zile mbigiri akaamua kukaa chini (tukumbuke alivaa msuli bila nguo yoyote ndani yake) hivyo zile mbigiri ziliendelea kumchoma hata huko makalioni. Alilia kwa uchungu bila msaada wowote, hivyo ndugu Hamnazo akafariki.

Baada ya sehemu hiyo ya ndugu Hamnazo ikafata sehemu inayoelezea kuwa: Mbigiri ni sawa na ugonjwa wa Corona, shamba ni Nchi na huyo ndugu Hamnazo ni kiongozi ambaye hakuchukua hatua kudhibiti mbigiri zilizoota shambani kwake hivyo kupelekea kifo chake.

Mwisho, mtangazaji wa kipindi hicho cha Tafakuri (ndugu Shaban Kisu) akawashauri watu wajilinde dhidi ya ugonjwa wa Corona ili wasife kizembe kama ndugu Hamnazo.

TBC1 hapa walimlenga nani kwa kumuita Hamnazo.?
 
Back
Top Bottom