Mtanganyika ni nani?

Mkandara

JF-Expert Member
Mar 3, 2006
15,772
8,958
Katika mila na desturi za Kiafrika kuna maswala ambayo yamehodhi jadi za matukio ambayo yaliakisi Makabila hayo kujinasibisha na mahala kuwa makazi yao ya asili kutokana na fursa zilokuwepo.

Na historia ya makabila haya imetokana na koo zile zile za Wakulima, Wafugaji na Wavuvi kutengana aidha kutokana na vita, ukame, maradhi, maafa ama kuhamia sehemu nyingine salama wakitafuta riziki zao.

Wakati mwingine Uwindaji, malisho bora ya mifugo ilikuwa sababu pia ili mradi hesabu kamili ya utu wa mwafrika hautokani na nchi bali tumeshehena mila na tamaduni zinazofanana kama jamii ya Wakulima, Wafugaji, Wavuvi, Wawindaji na Wachuuzi waloishi kama jamii eneo moja likaitwa nchi yao.

Kwa mukhtadha huo, mbali na uzio wa Makabila ya asili kuna Utaifa ambao ni jumuiko la watu wenye makabila yao wakiishi pamoja ndani ya himaya moja kutokana na shinikizo la mahitaji mbali mbali ya Ujima na biashara. Kwa maana hii tunaposema Tanganyika ni eneo la nchi ambalo wakazi wake wana makabila mbali mbali wakiishi kama jamii moja bila kujali asili zao ama walitoka wapi.

Hivyo basi, naposikia watu wakidai Tanganyika ya Watanganyika, hunielemea hoja ya kutaka kujua haswa tafsiri halisi ya madai haya na wakazi wake! - Mtanganyika ni nani?

Je, Mtanganyika ni kizazi cha watu walozaliwa kabla ya Muungano wa nchi mbili za Tanganyika na Zanzibar ama ni Wakazi wa leo wa Tanzania bara ambao hujinasibu kama wao ni wazawa wa bara? Bila shaka inaswihi tunapodai Tanganyika ni vema pia tukawajua warithi wake yaani Watanganyika ni kina nani?

Na kama sikosei mwaka jana niliandika makala nyingine nikiuliza MZANZIBAR ni Nani? Na sababu haswa zinatoka na tafsiri hasi isokuwa na historia nyuma yake isipokuwa kwa kutumia jina la nchi ili kutambua Watu wake. Kwa mfano Wakerewe sio Kabila bali kisiwa ndicho kinaitwa Ukerewe na wakazi wake wakaitwa Wakerewe.

Kuna hadithi nilipewa inasemekana asili ya Wakerewe ni Mkoa wa Kagera ama niseme jamii ya Wahaya waliokimbia Kagera baada ya ndugu wawili watawala wa kabila moja kupigana vita, kisha ndugu mmoja kukimbilia kisiwa cha Ukerewe kupata hifadhi na usalama wa watu wake.

Lakini pia Ukerewe haikuwa visiwa pekee bali utawala wake ulikuwa hadi nje ya visiwa hivyo mpaka sehemu ya Mkoa wa Mara haswa Mwibara ambako kuna makabila ya Wakwaya, Wajita, Waruri ambao pia naambiwa ni jamii ya Wakerewe. Na wao pia wakagawanyika katika koo nyingi zikaunda makabila mengineyo mengi kutokana na muingiliano na koo nyingine za kijamii.

Aidha hadithi hii iwe na ukweli ama laa hasha, lakini ndivyo makabila mengi yametokana na miingiliano ama migogoro ndani ya jamii moja kutengana na kisha kuzaliwa kwa kabila na himaya tofauti lakini zenye asili ya nasaba moja.

Na kwa bahati mbaya sana ndivyo yalivyo Makabila mengi ya Tanganyika na hata Zanzibar pia, nchi hizi hazikutokana na Utawala. Chukulia Utawala wa Zanzibar na Oman, ni urithi wa ndugu wawili watawala ambao sii tu wana asili moja bali walikuwa ndugu wa damu, isitoshe baba yao Said bin Sultan yeye pia aliikuta Zanzibar tayari ikiwa na wakazi wake. Zanzibar haikuwa Zanzibar kwa kutawaliwa, watawala waliikuta Zanzibar - Nasherehesha tu.

Nirudi katika hoja yangu ya leo, ndugu zangu Watanzania nawaasa sana tuwe makini sana na hii mihemko ya Utanganyika na Ikumbukwe kwamba Mwalimu Nyerere aliwahi kutuasa katika moja ya hotuba zake akisema haya:-

"Tunataka Rais ambaye si Mkabila, si Kaburu. Makaburu wa Tanzania ni wale wanaojiita wazawa. Ni makaburu tuu, mimi siwaonei haya hata kidogo ni makaburu tuu.

"Kwa sababu kama una mawazo yaleyale kama ya kaburu wa South Afrika ila tofauti yako kwamba ni mweusi ni kaburu tu."

" Wazungu wa South Afrika tulikuwa hatuwapingi kwa rangi yao, tulikuwa tunawapinga kwa Ubaguzi wao. Hatuwezi kuwa na makaburu hapa halafu tukawaheshimu kwa sababu weusi. Ni Makaburu tu"
- Mwisho wa nukuu

Kwa undani wa nasaha hii ya mwalimu imegawanyika sehemu mbili ambazo hatumhitaji kiongozi wa aina hii MKABILA au KABURU na wote kwa ujumla wanahodhi sifa za KIBAGUZI. Aidha atajali watu wa kabila lake na atawatenga watu wengine katika haki na maendeleo yao.

Na tunapodai Tanganyika ni Tanganyika ipi?
1. Ile kabla ya Mjarumani.
2. Ya Mjarumani yenye nchi za Burundi na Rwanda,
3. Ya Muingereza alokabidhiwa na Umoja wa Mataifa baada ya kugawanywa vipande.
4. Au Tanganyika ya miaka mitatu ilopewa Uhuru na Muingereza na kutambuliwa na Umoja wa Mataifa kuwa kigezo tusikubali badiliko jingine lolote la Utaifa baada ya Muingereza!.
- Ni Tanganyika ipi tunayodai?

Hivi ni kweli Tanganyika haikuwepo hata kabla ya ukoloni mpaka ilipogumbuliwa na mzungu aitwaye Speke ambaye hata jina Tanganyika halikuwa katika ulimi wala lugha yake! Nini chanzo na maana ya Tanganyika ikiwa sisi wenyewe hatufahamu asili yake isipokuwa ile tulofundishwa na Wazungu.

Ndugu zangu, Mwalimu Nyerere siintu alituasa bali ametuachia tunu kubwa ya Utaifa wetu kuwa nchi hii inaitwa Tanzania. Ni jina walochagua waasisi wetu na wakaamua wenyewe kuunganisha nchi zetu mbili kama ilivyo asili ya ndoa zetu tukazaliwa sisi. Hatuwezi badilisha Ubini wetu kwa sababu ya urithi wa mali.

Tuwaenzi viongozi wetu mwalimu Nyerere na Sheikh Abeid Karume kwa kuheshimu kazi kubwa waloifanya kabla ya Uhuru na baada ya Uhuru kwa sababu walitambua umuhimu wa Muungano wetu sii wa dini wala Makabila bali jamii ya WATU wenye tofauti zao.

Kuhitilafiana kupo hata kwa ndugu hutokea lakini katu kizazi hakiwezi kupoteza historia yake kwa matakwa ya mali na urithi. Tusitumie mapungufu na makosa ya baadhi yetu kuwa sababu ya utengano kwa sababu hakuna Mtanganyika wa Miaka mitatu tu (1961-1964) isipokuwa unatokana na asili ya wazazi watu.

Tuwaheshimu wazazi wetu
Maasalaam.
 
Kwasababu Tanzania ni fake.

Uhalisia ni Tanganyika na Zanzibar
Ukizungumzia Fake, je unajua kama Zanzibar ni mji sio nchi?

Wala katika historia hakuna nchi ilokua ikiitwa Zanzibar.
 
Tuache huu uongo, Zanzibar ni nchi, ina rais wake, katiba yake, wimbo wa Taifa nk
Kwa hiyo nchi hii imeanza mwaka gani? Maanake kama Tanzania ni fake basi hata Zanzibar ni fake!
 
Watanganyika ni wananchi wote wanaopatikana upande wa pili wa Muungano. Na Muungano huo ni kati ya Tanganyika na Zanzibar wa tarehe 26/04/1964.

Hivyo hizo story zako za Ukerewe, sijui kabla ya Wajerumani, na bla bla nyingine, ni za kufurahisha tu genge. Na utambue fika Watanganyika tuna akili timamu. Hivyo hatubabaishwi na hizi porojo zenu za kutaka kutotoa kwenye mstari.
 
..TANGANYIKA iliyopata Uhuru Dec 9 1961 na kuungana na Zanzibar April 26 1964.
Kwa hiyo Tanganyika ya miaka mitatu ambayo tayari.kulikuwa na Wazanzibar ndani ya chama na Serikali.

Ujue watu wengi hawafahamu hata harakati za Uhuru kwamba Kuna Wazanzibar walishiriki na wengine Wanachama wa TANU.

Hata historia ya hii CCM nyuma ilianza mwaka 1927 na chama cha African Association ambacho kilikuwa na matawi Mjini Zanzibar, Dar na Dodoma.
 
Watanganyika ni wananchi wote wanaopatikana upande wa pili wa Muungano. Na Muungano huo ni kati ya Tanganyika na Zanzibar wa tarehe 26/04/1964.

Hivyo hizo story zako za Ukerewe, sijui kabla ya Wajerumani, na bla bla nyingine, ni za kufurahisha tu genge. Na utambue fika Watanganyika tuna akili timamu. Hivyo hatubabaishwi na hizi porojo zenu za kutaka kutotoa kwenye mstari.
Watanganyika ni Wananchi wanaopatikana upande wa pili wa Muungano! mbona haieleweki. Upande wa kwanza wa Muungano ni upi?

Je, Mmasai anayepatikana Zanzibar huyu sio Mtanganyika! Au Mpemba anayepatikana Dar huyo sio Mzanzibar?

Na kwa tafsiri hiyo, Huyu rais wa Zanzibar Hussein Mwinyi ni Mzanzibar au Mtanganyika!
 
Back
Top Bottom