Tanzania ya sasa ni ile aliyoona Oscar Kambona, Mwalimu Nyerere alikosea sana

Kila mrengo unafaida na hasara zake, Mwalimu kwa Sera ya ujamaa angalau Ardhi, elimu na afya tunafaidi japo kadri miaka inavyosonga Elimu inakuwa ghali kuipata ile nzuri, Ubepari nao unamabaya yake waone Kenya na Zambia baada ya Rais Kaunda ndo utajua kwanini kila Sera inamabaya na mazuri yake

Mfumo sahihi ambao hata Mungu aukubali ni ubepari.Ubepari unakuza uchumi,unakuza mapato ya Kodi 10 times tena kwa haraka zaidi,ubepari unapunguza unamaliza tatizo la ajira kwa haraka Sana.Usaidia upatikanaji wa bidhaa na huduma kwa bei ya chini na kwa wingi zaidi.
Case study China baada ya kuruhusu ubepari tu uchumi wa china umekimbia kwa speed ya 10G.
 
Kila mrengo unafaida na hasara zake, Mwalimu kwa Sera ya ujamaa angalau Ardhi, elimu na afya tunafaidi japo kadri miaka inavyosonga Elimu inakuwa ghali kuipata ile nzuri, Ubepari nao unamabaya yake waone Kenya na Zambia baada ya Rais Kaunda ndo utajua kwanini kila Sera inamabaya na mazuri yake
sikatai juu ya hilo, lakini mwisho wa siku TZ ya sasa ivi ni ile ya kambona tungelifanya hili mapema tungekua mbali sana...watu wengi wanamsapoti nyerere kwa kigezo cha kwamba kaleta "umoja" lakini sio kweli suala la umoja halihusiani na siasi za ubepari au ujamaa wala siasa ya vyama vingi au kimoja, angalia nchi kama marekani
 
Kupanga ni kuchagua! Wengi wa wale walioanza na ideology ya Ubepari wakati nchi zao bado ni changa wameishia kupata matabaka either ya kikanda au kikabila! Inawezekana ukaona kuwa tumechelewa sana lkn amini kuwa misingi aliyoijenga mwalimu ndio leo tupo wamoja hivi unavyoona hatuulizani makabila wala dini. Sasa kama kujenga nchi tuanzie hapo baada ya kujenga Amani na Umoja wa Kitaifa.
Aisee una hoja pia. Sikua nimeiwaza sana hii hoja.
 
Wewe mtoto uliezaliwa juzi huwezi kuona umuhimu wa ujamaa tulioufuata hapa Tanzania. Bwabwaja maneno humu Jf , ila nenda Kenya fuatilia madhara ya ubepari walioufuata,maana hata kupata kipande cha ardhi kulima mboga mboga ni tabu.
 
sikatai juu ya hilo, lakini mwisho wa siku TZ ya sasa ivi ni ile ya kambona tungelifanya hili mapema tungekua mbali sana...watu wengi wanamsapoti nyerere kwa kigezo cha kwamba kaleta "umoja" lakini sio kweli suala la umoja halihusiani na siasi za ubepari au ujamaa wala siasa ya vyama vingi au kimoja, angalia nchi kama marekani

Njaa haiwezi leta umoja,sema alileta ukondoo.Ukondoo sio umoja.
Huwezi ukawa na njaa ukawa mzalendo.
 
nimesusanya dots za hapa na pale nkasoma stories zake , cha ajabu wale ambao walishuhudia haya yote kwa macho yao huwezi kuskia wakiongelea haya mambo watuambie ukweli
Nimesikitika sana kusoma kitabu cha Mkapa, hajaeleze ma kabisa ugomvi wa Kambona na Nyerere.

Wakati yeye ndiye alikuwa katikati kama mhariri wa gazeti la serikali wakati huo, akipata ubuyu wote kutoka kwa waandishi wake na kumpelekea Nyerere.

Mama Joan Wicken kaandika kitabu ila kaacha wosia kisichapishwe mpaka miaka kadhaa itakapopita baada ya yeye kufariki. Inaonekana kaandika mengi humo.
 
Kambona alibobea zaidi katika masuala yapi na ndani ya Tanu Kambona alikuwa na nafasi ipi? au enzi hizo Chama hakikuwa na mfumo wa vyeo/nyadhifa kama ilivyo sasa?

Sent from my SM-G610F using JamiiForums mobile app
 
kambona aliamini ubepari na siasi ya vyama vingi, nyerere aliamini ujamaa na siasa ya chama kimoja
At the end Kambona ndie aliyeshinda hata Nyerere alikuja muelewa kambona akiwa ameshachelewa ,Thus Nyerere baada ya kuyatambua makosa yake alitoa speech na vitabu vingi Sana akiponda falsafa zake japo mfano vitabu Kama Tujisahihishe, Uhuru na maendeleo, kuruhusu vyama vingi ambavyo aliviuwa, speech maarufu ya "hatari ya kutawaliwa na dikteta kwa katiba hii" nk.
Naamini hata mwanafunzi wake atakuwa Mwalimu mzuri siku mfumo ukimtupa maana huwezi yaona makosa yako uwanjani kwenye mechi ni Hadi Ukiwa nje ya uwanja ukizama recorded. Si ajabu atajishahihisha kwa kutuletea katiba mpya na tume huru ya uchaguzi.
 
nitafarijika sana kama siku moja mzee Mohamed Said ataandika makala maalumu ya kumuelezea kambona kama vile anavyofanya katika kuwaandikia makala wazee wake wa kariakoo walioshiriki katika harakati za kisiasa kabla na baada ya uhuru.

najua uwezo huo unao ila hajajisikia tu kufanya hivyo. labda kwa kuwa kambona hakuwa mwenzetu kiimani.

Kwani Kambona ni Muislamu? Maana babu analazimisha udini utadhani analipwa, anakera kwa kweli!
 
Mwalimu is overrated, wale waliomfadhili kipindi anapigania Uhuru aliwageuka, maduka ya ushirika yalitesa watu, baada ya kufeli vibaya akaamua kuachia madaraka kuepuka aibu lakini anavyoimbwa unaweza kudhani alikua malaika
Je, aliwageuka ili kujinufaisha yeye binafsi ???

Maana naona soon tunaingia kwenye siasa za misikitini.
 
Kambona alibobea zaidi katika masuala yapi na ndani ya Tanu Kambona alikuwa na nafasi ipi? au enzi hizo Chama hakikuwa na mfumo wa vyeo/nyadhifa kama ilivyo sasa?

Sent from my SM-G610F using JamiiForums mobile app
alikua sekretari mkuu wa chama cha tanu yaani yeye ndo alikua mratibu mkuu wa shughuli zote za chama ni kama vile bashiru na magufuli kwa sasa yaani anaeendesha chama ni katibu mwenyekiti yupo tu kama political figure japo yeye ndo ana maamuzi ya mwisho, yaani yeye na mwalimu walikua na uwezo kana kwamba walikua wanaweza wakaamua kitu wao na kikapita bila kupingwa, kambona baadae akawa waziri wa kwanza wa mambo ya nje
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom