Bibi Titi Festival Ikwiriri, Rufiji: Mwanzo wa Bibi Titi katika kupigania uhuru wa Tanganyika 1954

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,925
30,273

Ilikuwa wakati Nyerere yuko Musoma ndipo John Hatch kutoka Chama cha Labour cha Uingereza alipokuja Tanganyika kama mgeni wa TANU.

TANU ilifanya mkutano mkubwa sana Mnazi Mmoja na Hatch akawahutubia wananchi.

Inakisiwa takriban watu 20,000 walijitokeza kwenye mkutano huo. Ali Mwinyi Tambwe alikuwa mkalimani wa Hatch.

Denis Phombeah pamoja na Katibu mkuu wa TANU, Oscar Kambona vilevile walihutubia halaiki ile.

Hii kutanguliza ‘’Bibi’’ kabla ya jina la Titi mtu wa kwanza kulisema kwa msisitizo alikuwa Oscar Kambona katika mkutano mmoja wa kuwavuta wanawake waiunge mkono TANU.

Hatch akiwa anaunga mkono ukombozi wa watu weusi aligundua kuwa TANU haikuwa na tawi la akina mama.

Katika dhifa ya chai iliyoandaliwa na TANU kwa heshima yake, Hatch alilieleza tatizo hili kwa Schneider Plantan na John Rupia.

Hatch alimwambia Schneider kwamba ili kuwa na chama chenye nguvu TANU isiwaache akina mama nyuma.

Hatch alimwambia Schneider kwamba huko Uingereza Chama cha Labour kilikuwa kimejikita kwa wanawake kama moja ya nguzo yake kuu.

Schneider alimwendea Bibi Tatu binti Mzee akamwomba kuanzisha tawi la akina mama kwa ajili ya TANU.

Bibi Tatu binti Mzee alimpendekeza Bibi Titi Mohamed ndiye afanye kazi hiyo kwa sababu ya tabia yake ya ucheshi na kupenda kuchanganyika na watu na ukweli kwamba toka hapo alikuwa mwanachama wa ‘’Bomba Kusema,’’ chama cha akina mama wa mjini Dar es Salaam.

Scheneider akamfuata mumewe Bibi Titi Bwana Boi Suleiman kumuomba mkewe ajiunge na TANU.

Hivi ndivyo Bibi Titi alivyojiunga na chama cha TANU.

Inasemekana kuwa kama nafasi ile ingempita Bibi Titi basi ingechukuliwa na Bibi Halima bint Khamis ambao wote wawili walikuwa na vipaji sawa katika kushawishi na fasaha ya uzungumzaji.
1700405542745.jpeg

Mwalimu Nyerere na Bi. Halima Khamis, Dimaond Jubilee Hall, 1990

1700405644853.jpeg
 
Kumbe kulikuwa na wakristo kwenye harakati za tanu!!!
Mnachi...
Kulikuwa na Julius Nyerere Territorial President na mtu aliyemfikisha kwa Abdul Sykes Act. TAA President na Secretary 1952 alikuwa Joseph Kasella hawa wote wawili Wakristo na Waasisi wa TANU.

Alikuwapo Dennis Phombeah, Mnyasa kutoka Nyasaland kadi yake ya TANU No. 5 na alikuwapo Dome Okochi Budohi Mluya kutoka Kenya kadi yake No. 6.

Walikuwapo Steven Mhando na mdogo wake Peter Mhando.

Alikuwapo Robert Makange...wengi walikuwapo.

Hukuyajua haya kwa kuwa historia ya kweli ya TANU haikuwa imeandikwa.

Soma kitabu cha Abdul Sykes utakutana na wengi wala wewe hujapata kuwasikia.
 
Mnachi...
Kulikuwa na Julius Nyerere Territorial President na mtu aliyemfikisha kwa Abdul Sykes Act. TAA President na Secretary 1952 alikuwa Joseph Kasella hawa wote wawili Wakristo na Waasisi wa TANU.

Alikuwapo Dennis Phombeah, Mnyasa kutoka Nyasaland yake ya TANU No. 5 na alikuwapo Dome Okochi Budohi Mluya kutoka Kenya kadi yake No. 6.

Walikuwapo Steven Mhando na mdogo wake Peter Mhando.

Alikuwapo Robert Makange...wengi walikuwapo.

Hukuyajua haya kwa kuwa historia ya kweli ya TANU haikuwa imeandikwa.
Kwahiyo kumbe ni kama timu ya taifa ya tanzania ambayo kwasasa imefuzu afcon ambayo ndani yake wachezaji wengi ni waislamu halafu baadae atokee mtu aseme kuwa waislamu ndio wameifanya taifa stars kufuzu afcon?
 
Ungesoma kitabu cha Abdul Sykes ungeshangazwa na mengi.

Usingekuja na mfano huo.

Kama maswali ungeniuliza maswali mazito kutaka kujua zaidi.
 
Mnachi...
Ungesoma kitabu cha Abdul Sykes ungeshangazwa na mengi.

Usingekuja na mfano huo.

Kama maswali ungeniuliza maswali mazito kutaka kujua zaidi.
Unapimaje maswali mazito na yasiyo mazito? Ni hivi mfano niliokupa ni sawa na huo wa Tanu na taifa stars...huku mtwara waislamu ni wengi mno kwa takwimu ya haraka haraka wilaya yenye wakristo wengi ni masasi na kidogo nanyumbu illa kuanzia newala,tandahimba,mtwara ni uislamu tupu mwaka 2012 tulianzisha vuguvugu la gesi na hamasa zagesi isitoke zilianzia kwenye majukwaa ya kisiasa na ilifika hadi kwenye misikiti yote ya hapa mjini mtwara ila hakukuwa na kitu kama hicho kwenye kanisa lolote lile, hatimaye yakatokea yale yakutokea na mwisho umati wa watu ulijaa pale kwenye uwanja wa mashujaa kwa ajili ya kusoma al badr kumshitakia Allah kwa dhuluma iliyofanyika...sasa je hizi zilikuwa harakati za kiislamu au zilikuwa harakati za wakazi wa mtwara?kwasababu kulikuwa na wakristo wengi ambao walijumuika pia kudai gesi isitoke
 
Kwahiyo kumbe ni kama timu ya taifa ya tanzania ambayo kwasasa imefuzu afcon ambayo ndani yake wachezaji wengi ni waislamu halafu baadae atokee mtu aseme kuwa waislamu ndio wameifanya taifa stars kufuzu afcon?
wewe wa miaka ya 2000 unataka kubishana mzee mudi? chukua maarifa kwa kusoma vitabu vihusio historia upate maarifa na kujua mambo hayo mengine unakimbilia tu na umri wako mdogo
 
wewe wa miaka ya 2000 unataka kubishana mzee mudi? chukua maarifa kwa kusoma vitabu vihusio historia upate maarifa na kujua mambo hayo mengine unakimbilia tu na umri wako mdogo
Mimi ningetembelea mitaa ya kwao mama yako ningekuwa nimemuoa
 
Unapimaje maswali mazito na yasiyo mazito? Ni hivi mfano niliokupa ni sawa na huo wa Tanu na taifa stars...huku mtwara waislamu ni wengi mno kwa takwimu ya haraka haraka wilaya yenye wakristo wengi ni masasi na kidogo nanyumbu illa kuanzia newala,tandahimba,mtwara ni uislamu tupu mwaka 2012 tulianzisha vuguvugu la gesi na hamasa zagesi isitoke zilianzia kwenye majukwaa ya kisiasa na ilifika hadi kwenye misikiti yote ya hapa mjini mtwara ila hakukuwa na kitu kama hicho kwenye kanisa lolote lile, hatimaye yakatokea yale yakutokea na mwisho umati wa watu ulijaa pale kwenye uwanja wa mashujaa kwa ajili ya kusoma al badr kumshitakia Allah kwa dhuluma iliyofanyika...sasa je hizi zilikuwa harakati za kiislamu au zilikuwa harakati za wakazi wa mtwara?kwasababu kulikuwa na wakristo wengi ambao walijumuika pia kudai gesi isitoke
kiongozi,
nionacho mimi hapa anachofanya mzee mudi ni kuchambua historia ya wale ambao ana interest nao kwa upande wake na kuangalia nini kiliwasukuma wao kufanya hivo hususan kwenye hay mambo makubwa.. kama na wewe kuna ambao unawaona mzee mudi hawagusi kwa namna moja au nyingine na walikuwa na umuhim mkubwa hasa kwa masuala ambayo mzee mudi anawazungumzia nawe walete hapa au fanya kama anavofanya mzee mudi kwa wewe kutuletea hao wakwako ila ukianza upopoma hapa wakusema hawa sijui wale si takuona huna lolote isipokuwa kihelehele cha mikono yako kutaka kuandika hapa
 
Back
Top Bottom