Tanzania ya sasa ni ile aliyoona Oscar Kambona, Mwalimu Nyerere alikosea sana

Duuuh

1) Lyatonga Mrema wakati wa jaribio la Mapinduzi 1964 alikuwa na miaka chini ya 18

Fanya marekebisho Mkuu

Mrema kaja kuwa Waziri awamu ya Mwisho ya Baba Hussein

2) Bibi Titi hakushtakiwa kwa uhaini kwny jaribio la 1964, ugomvi wa Nyerere na Bibi Titi ulianzia 1967 kwny Azimio la Arusha, ukakolea 1968 kwny kuanzishwa kwa Bakwata, akakamatwa yeye na wenzie kadhaa akiwemo Mzee wangu Mzee Lifa Chipaka wakafungwa maisha.

Akina Bibi Titi hawakusamehewa bali Mahakama ya EA iliwakuta hawana hatia Serikali ikagoma kutii mahakama baadae 1971 akaigiza kuwasamehe

3) Kambona alirejea kwny Jeneza 1997 na cha ajabu Nyerere alikuwa bado na kinyongo nae akakataa hata kushiriki Msiba walau kutoa pole kwa wana Familia na best man wa ndoa yake…angekuwa hai angepaswa ajifunze ustaarab huo kwa Ngoyai na Jakaya…pamoja na mabif yao wanajuliana hai na kusabahiana panapokuwa na majanga
 
Namaanisha kilichofanyika kilishafanyika waliopokea kijiti “wangerekebisha” miaka 35 sasa.. Ni kama kulilia ukoloni ulitunyonya ndo maana hatuendelei wakati wakoloni walishaondoka miaka na miaka
mimi nacholilia ni kwamba kabla ya kupokea hivyo vijiti watambue watu waliotoa mchango mpaka kijiti hicho kikapatikana sio kujaribu kuwafuta kwenye historia ya nchi, kamwe hawawezi kurekebisha chochote! kilichpotea kimepotea
 
Umeandika uongo mtupu. Uliza historians wakuelezee vizuri. 1964 kipindi cha uasi wa jeshi Lyatonga wala alikuwa hajulikani. Kambona aliondoka nchini 1967 wakati wa vuguvugu la Azimio la Arusha. Unachanganya kesi ya uhaini ya washirika wa Kambona kina Bibi Titi Mohamed, Gray Mataka na wengine walioshtakiwa na kukutwa na hatia ya kupanga kumpindua Nyerere na wakahukumiwa kifungo cha maisha.

Nchi ina historia inahitaji maandishi ya kina yenye utafiti wa kutosha kwa kuwahoji watu waliokuwepo wakati huo. Bahati mbaya wengi wao hawapo duniani sasa.
 
Aisee una hoja pia. Sikua nimeiwaza sana hii hoja.
Tatizo ni kwamba, ubepari tumeshindwa na misingi ya umoja wa kitaifa iliyopaliliwa na ujamaa nayo tumeshindwa.

Viongozi wa sasa wanafanya mistake kubwa sana kwa kufikiri kwamba kazi ya kujenga umoja wa kitaifa ilishamalizwa na Mwalimu Nyerere.

Hii ni kazi ya kuendelezwa na kila kizazi.

Hata nyumba ukijenga itataka kufanyiwa ukarabati kila mara, kubadilishwa paa, kupakwa rangi, kufagiliwa na kusafishwa.

Tulipofikia sasa hivi, watu wanataja mambo ya ukabila wazi kabisa, watu wanataja mambo ya udini wazi kabisa. Hata Mwalimu Nyerere miaka ya mwisho ya uhai wake alionya kuhusu haya qkiona kazi nzuri aliyofanya ya kujenga umojq wa kitaifa watu wanazembea kuiendeleza. Alilisema hili kwenye hotuba zake.

Inaonekana viongozi wetu wa sasa wanadharau.

Tumeshindwa ubepari, tumeshindwa ujamaa, tunawayawaya bila muelekeo kwa kumsikiliza mtu mmoja tu.
 
Kwa miaka ile ya uhuru, ujamaa ulikuwa ni essential sana kwa jamii yetu kwasababu taifa lilikuwa ni changa na hatukuwa sawa.

Ujamaa ulileta hali ya usawa na umoja katika kujenga taifa. Tukawa na lugha moja ya kiswahili na leo unaona faida yake unakwenda mkoa wowote na kuongea na watanzania wenzako bila pressure.

Pia kwa nyakati zile kulikuwa na baadhi ya watanzania walishaanza elements za matabaka, watu kama wachagga walikuwa na mifumo ya uchief akina mangi ambao waliamini ndio top position na waliiheshimu but Hayati baba wa taifa alifanya jitihada sana kukemea watu kujiona sio sehemu ya umoja wa taifa imagine leo bila kuwapo umoja wa taifa, kungekuwa na jamii zinawadominate wengine kwa ubabe na kuhodhi rasilimali kisheria kabisa bila kupingwa. Ila leo hapa ukiongea huo upuuzi kwanza kila mtu atakuona Takataka.

Kwahiyo ninyi watoto wa kizazi hiki cha sasa mkiwa mnaambiwa haya mastory ya ajabu ajabu ya sijui nani alifanya nini tumieni na akili zenu kuangalia kipi kinatija kipi hakina.

Sasa mfano unataka kwenye historia tuwaongelee wazee waliokuwa wanataka kumpindua nyerere kama akina bibi titi akina nani sijui yule aliyefia kigamboni ambao wao sera yao wamebeba maneno ya udini ndani yake kuwa waislaam ndio waligombania uhuru wa taifa hili.... Sasa unajiuliza huyu mtu anataka kila mtu aishi kwa misingi ya dini anayoiamini yeye au tumualeweje?!

So ni ubinafsi. Unapomuongelea nyerere hebu jaribu kwanza kumjua. Yule mzee alichofanya ni kutuwekea misingi bora sana ya jamii, sera ya ujamaa kwa nyakati zile ilikuwa muhimu sana katika kutuimarisha kama taifa changa lililotoka katika usimamizi wa wakoloni, sasa tungelianza hili taifa na sera za kibaguzi za kabila fulani liwe juu ya makabila mengine si ajabu leo katiba ungesema wasukuma, wachagga au wahaya au wahehe, au wazanaki, au wagogo ndio jamii teule ambayo inatakiwa kuwa katika uongozi. Au basi katiba ingesema dini ya usislam ndio dini ya taifa wengine nyie ni makafiri mtasali kwa maelekezo ya viongozi wa dini ya kiislam.

Haya yote nyerere aliyazima mapema sana. Na hao watu ambao unasikia walifutwa katika vitabu vya history sio kwasababu hawakuwa na mchango katika mapambano na harakati za uhuru, ila walikuwa na ajenda zao binafsi na za kimakundi.

Nitakupa mifano, wakati nyerere anakwenda kudai uhuru wa Tanzania nzima, kuna chifu sijui mangi nani yule alienda kudai uhuru wa wachaga tu baaasi, yaani kilimanjaro nadhani na Arusha kuwe ni taifa huru wasihusiane na jamii zingine, sasa huu ufala wewe unataka uandikwe katika history.

Kuna wapigania uhuru walitaka mpindua nyerere na kuanza harakati binafsi wao wakataka nyaraka za uhuru zitambue Tanzania ni jamii ya kiislam kama vile kule Sudan, somali, wakati kwa miaka ile karibu 90% ya watanzania hawapo katika Imani moja wala uislam. Sasa unataka vitabu vya history viwaongelee wapuuzi kama hawa hata kama walikuwa na harakati?!

Nyerere hata anafariki tazama maisha yake na familia yake, hivi unaweza fananisha na familia za akina mwinyi, mkapa, kikwete, na huyu wa sasa, hivi hata wanafanania.... Tazama walivyojiweka mbali na siasa za sasa. Tazama namna hawajihusishi na maswala ya uongozi au kuwa kiherehere.

Hivi mfano hili taifa lingekuwa Baba wa taifa ni kikwete, hivi 90% ya watendaji wa serikali si wangekuwa wakerewe, na katika noti hata ridhiwani angewekwa kama mtoto wa taifa. Maana sio kwa tamaa zao.

So, as much as tutamsema huyu mzee lakini, tukubali ana mema yake na ametufikisha hapa kwa wema tu sio hila wala nia mbaya. Na tunamsingi mzuri sana wa kujipanga na kuwa taifa bora afrika.

Huyu wa sasa anakosea kuleta sera za kijamaa za miaka ile nyakati hizi ambapo haziendani na nyakati hizi za mifumo ya uchumi ya soko huria.

Na tusipende kutumia neno uchumi wa kibepari bali tuseme uchumi wa soko huria.....

Tuendelee kuheshimu n akuenzi mema ya Baba wa taifa mwalimu J. K. Nyerere, na tujitahidi kuondoa huu mfumo wa ujamaa wa kifukara tujenge ujamaa wa kisasa wa soko huria ambapo tutashare mitaji, mbinu, ili tupambane na mataifa jiarani katika kuwa super economy wa afrika.
 
sikatai juu ya hilo, lakini mwisho wa siku TZ ya sasa ivi ni ile ya kambona tungelifanya hili mapema tungekua mbali sana...watu wengi wanamsapoti nyerere kwa kigezo cha kwamba kaleta "umoja" lakini sio kweli suala la umoja halihusiani na siasi za ubepari au ujamaa wala siasa ya vyama vingi au kimoja, angalia nchi kama marekani
Kawaulize Kenya na ubepari wao wanaendeleaje, ungejua wanavyotutamani watz
 
Nyerere atabaki kuwa hero, kuingia katika mfumo wa capitalism bila maamdalizi tungelia kama Kenya kumiliki kieneo hata square metre moja ni ndoto
ujamaa ulikua na maandalizi gani? ni either you do it au you dont hakuna kitu lichokua kinahitaji maandalizi baada ya uhuru, tulikua tunaanza from scratch
 
Mwalimu is overrated, wale waliomfadhili kipindi anapigania Uhuru aliwageuka, maduka ya ushirika yalitesa watu, baada ya kufeli vibaya akaamua kuachia madaraka kuepuka aibu lakini anavyoimbwa unaweza kudhani alikua malaika
Hakuachia madaraka kwa kutaka,bali ilikuwa shindikizo la ndani na nje ya nchi.
Serikali ya Marekani ikiongozwa na Raisi Ronald Reagan ,huku waziri mkuu Margaret Thatcher wa Uingereza walimsumbua na kutuwekea vikwazo vya kiuchumi.
Ndani wananchi walimchoka wakipanga kumpindua mara kwa mara.
World Bank,IMF walikuwa mbogo sana.
 
..But I did learn a lot regarding this period from Paul Bjerk's "Building A Peaceful Nation: Julius Nyerere And The Establishment of Tanzania 1960-1964".
Asante kwa hiki Kitabu. Ngoja nikipitie neno kwa neno...pages 392
 
Asante kwa hiki Kitabu. Ngoja nikipitie neno kwa neno...pages 392
Kipitie, kina madini mengi sana.

Kwa mfano, sikujua kwamba Nyerere ndiye alikuwa kiongozi wa kwanza kuanzisha vikwazo vya kiuchumi dhidi ya utawala dhalimu wa makaburu wa Afrika Kusini, baadaye karibu dunia nzima ikamuunga mkono.

Siku hizi nikisikia tuna rais anahimiza ubaguzi wa rangi miongoni mwa watu wake kwa kusema atapendelea wanawake weupe zaidi ya weusi, kwenye hotuba ya kikazi, najiuliza swali moja.

How did we get this low?
 
Nyerere atabaki kuwa hero, kuingia katika mfumo wa capitalism bila maamdalizi tungelia kama Kenya kumiliki kieneo hata square metre moja ni ndoto

Nyerere alikuwa na mawazo ya ajabu kama jiwe mfano alikataa kuanzishwa kiwanda cha Coke, wakati wake hata kupata soda ilikuwa kazi
tembelea youtube uangalie Maisha ya wakenya,waganda na wacongo miaka ya 60 mpaka 70 uone watu walivyoishi vizuri alafu linganisha na Tanzania, wakati wa Nyerere hata mtu kumiliki Gari tu ilikuwa ngumu sana ukilinganisha na nchi jirani
 
Kambona hakuwa mjamaa alikuwa mbepari na fikra zake zilikuwa za kibepari na Kama hawangetofautiana na Nyerere tungekuwa mbali Sana na anayesema alikuwa mjamaa anajua kwa nn aliishi uhamishoni?
 
Nyerere alikuwa na mawazo ya ajabu kama jiwe mfano alikataa kuanzishwa kiwanda cha Coke, wakati wake hata kupata soda ilikuwa kazi
tembelea youtube uangalie Maisha ya wakenya,waganda na wacongo miaka ya 60 mpaka 70 uone watu walivyoishi vizuri alafu linganisha na Tanzania, wakati wa Nyerere hata mtu kumiliki Gari tu ilikuwa ngumu sana ukilinganisha na nchi jirani
Shida kubwa kwa kizazi cha sasa ni kwamba, kuna somo linaitwa sayansi kimu sikuhizi halifundishwi shule za msingi.
Misingi minne ya uzalishaji mali(four factors of production) nguvu kazi,ardhi,mtaji na usimamizi ni mhimu Sana kuwekewa kipaombele cha kipekee.
Ardhi ndiyo inayoshikilia misingi yote ya uzalishaji Mali.
Taifa ambalo liliheshimu msingi huu tangu enzi za kupata uhuru,wananchi wake wanafurahia.
Leo hii Tz unaweza kupata ardhi hata hekta 1000 kwa urahisi kabisa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom