Tanzania tuna Adui mmoja tu, Ujinga, nyingine zote ni porojo za ujinga wetu tu

Hili la adui ujinga nimeliandika mara nyingi hapa JF kwenye posts tofauti.

Kwa miaka mingi sasa huwa nauliza na kujiuliza "hivi hizo shule mlienda kusomea ujinga?" Kuuliza kwangu siyo kwa kukisia au kwa kenehi au kejeli, ni swali la ukweli kabisa.

Kilichonisukuma kuandika haya, ni yote yanayojiri sasa hivi. Tumefikikia kubishana kijinga kabisa, kuna watu wanabishana kuhusu biashara, hajawahi kyufanbya biashara toka kuzaliwa. Kuna watu wanabishana kuhusu bandari hajawahi kuiona hata bahari. Ni ujinga tu.

Kuanzia jana nimekaa natazama wanasheria weu wamakwenda baraza la usuluhushi la Kimataifa, mpaka kichefuchefu, mtu unajiuliza walienda kufanya nini kama siyo kuendelea kututia hasara?

Hivi walilazimishwa kuongea Kingereza? Si wangeomba watapta? Mpala nimeona kichefuchefu, hivi waziri aliyewapeleka hauoni huu utu mbi wanaoufanya huko? Dah! Inatisha.

Naamini kabisa kutoka ndani ya moyo wangu, hatuna adui umasikini, hatuna adui maradhi. Adui yetu ni mmoja tu, ujinga. Watanzania tu wajinga wa hali ya juu.

Ujinga unatufanya tuwe na maradhi, ujinga unatufanya tuwe masikini, ujinga unatufanya tuwe wezi, ujinga unatufanya tuwe na kila baya.

Tufanye nini kuondokana na adi ujinga?

Nasubiri majibu ya kijinga.
adui wa Tanzania ni sisiemu. vingine vinarekebishika.
 
Bahati nzuri mimi siyo Mtanzania. Mimi ni Mtanganyika, sijawahi kuukana Utanganyika wangu.
Hongera sana
FB_IMG_1702085740919.jpg
 
Back
Top Bottom