Tanzania ni nchi ambayo raia wake hawana shida wala taabu yoyote.

Nazjaz

JF-Expert Member
Jan 20, 2011
7,684
8,833
Juzi tumeona majirani zetu wa Kenya na Uganda wakiandamana kupinga mfumuko wa bei, kupanda kwa bei ya mafuta na ugumu wa maisha kwa ujumla.
Tanzania tumekaa kimya, mafuta yanapanda bei kila uchao, umeme nao unapanda bila kuchoka. Vyakula havikamatiki kwa jinsi vilivyo panda bei.
Je haya nayaona kauzu mimi tu au hata nyie wenzangu mnaona?
Kwanini tusiandamane kuonyesha uchungu wetu?
Vigogo kwao maisha mazuri viyoyozi hadi kwenye mabanda ya mbwa wao.
 
Tuko usingizini subiri tukiamka...
 
Watanzania wote tumelala hivyo hatujui ni nani atamwamsha mwenzie. Dr. wa ukweli anajaribu kutuamsha ila wapi hatusikii kitu.
 
Dr wa ukweli akituamsha Dr feki anatuchoma tena nusu kaputi
 
Nazjaz,

Kila kitu kwa wakati wake!

Amani na utulivu vinamalizia muda wake.....kama nchi na viongozi wa nchi hawatabadilisha muelekeo.

Kuna msemo wa "kimya kingi kina mshindo mkuu."

Kila kiashiria cha kuwa watu wako hoi kiko wazi kwa mwenye macho kuona.

Kweli wananchi wana mifuko iliyotoboka. Hawana ajira, rushwa imeshamiri,haki inanunuliwa, ufisadi, ubadhirifu katika matumizi ya fedha za serikali/umma, mgao wa umeme wa dharura kila mwaka, ukandamizaji wa demokrasia kama kuzuia maandamano na mikutano ya vyama vya upinzani, kuwazuia wananchi wasijadili Muungano na muundo wake, dana dana katika kuandika Katiba mpya na kuundwa kwa tume huru ya Uchaguzi, Mikataba mibovu ya madini, bomoa bomoa makaazi ya wananchi, ukosefu wa tiba katika zahanati na mahospitali ya serikali mpaka watu wamejenga imani na tiba za "mababu", Ubinafsi na umimi badala ya jamii na taifa.na haya "maisha bora kwa kila mtanzania" aka ugumu wa maisha unaoengezeka ukali kila siku.

Muda ukifika mchanganyiko huu utafumuka na athari yake itawashangaza watu katika vipembe vya dunia wanaoiona Tanzania ni kisiwa cha amani.

Tatizo kubwa ni kuwa viongozi wetu, wengi wao ni wachafu, si safi na waliowazunguka pia ni aina hiyo hiyo. Na viongozi hawa wanakosa ujasiri wa kuua nyani. Inabidi wachore mstari mchangani na wawatizame manyani machoni ....kutokana na matukio katika nchi nyingi sasa ni wazi ni suala la muda tu, hayo yanayotokea nchi nyengine yatafika hapa Tanzania.

Viongozi ni wale wenye uoni na ujasiri wa kuchukua hatua mapema na sio kusubiri wakati wa dharuba, dharuba ikifika itawakomba na wao pia hata kama watafanya kama walivyofanya viongozi wa nchi nyengine kutumia polisi na jeshi.

Wakati nakubaliana na wewe kuwa bado watanzania tunakula amani na utulivu lakini si kuwa hatujui nini kinaendelea. Na kama viongozi watauchukulia ukimwa huu wa watanzania kuwa ni dalili ya kuridhika basi wanajidanganya.
 
Tanzania kwanza hakuna "Amani"Ila Tanzania pana "Utulivu"tu hakuna kingine.Wadau nisaidieni Tanzania na Kenya ni nchi ipi yenye mali asilia nyingi ambazo huwa zinakuza uchumi wa nchi??.
 
Mkuu Nonda umesema vema....siku watanzania watakapo ingia barabarani hakika kitakacho tokea wengi kitawashangaza, binafsi niliamini tarehe 16 - 04- 2011 ilikuwa mwanzo wakategua....
 
Tanzania kwanza hakuna "Amani"Ila Tanzania pana "Utulivu"tu hakuna kingine.Wadau nisaidieni Tanzania na Kenya ni nchi ipi yenye mali asilia nyingi ambazo huwa zinakuza uchumi wa nchi??.
Mkuu huhitaji kuwa na PhD kulitambua hilo.......
 
mpe pole jirani yako wa karibu anayejifanya mabosi wake wamevua gamba lakini tabia zilezile..
 
Hakika maisha ya walio wengi ni magumu ila watanzania ni waoga wa kudai haki... wengi wanadanganywa eti wakiandamana amani itavunjika. Kidogokidogo watu wanaanza kuelewa amani ni pamoja na maisha bora. Kama hali ya maisha itaendelea kuwa ngumu watanzania watashindwa kuvumilia na woga utawatoka, maandamano makubwa yatafanyika kwa lengo la kuiondosha CCM madarakani.
 
mpe pole jirani yako wa karibu anayejifanya mabosi wake wamevua gamba lakini tabia zilezile..

Serikali ya magamba ni miongoni mwa kero zetu. Kwa kuwa wao wameishikilia mihimili yote ya dola, wanafanya yale yasiyopendeza machoni pa binadamu na Mungu pia. Kijijini kwetu eneo la msitu wa matambiko kapewa mwekezaji wa kigeni eti analiendeleza.
Kafyeka msitu wote na matokeo yake hadi leo hatujapata masika tangu mwaka jana.
 
Nazjaz,

Kila kitu kwa wakati wake!

Amani na utulivu vinamalizia muda wake.....kama nchi na viongozi wa nchi hawatabadilisha muelekeo.

Kuna msemo wa "kimya kingi kina mshindo mkuu."

Kila kiashiria cha kuwa watu wako hoi kiko wazi kwa mwenye macho kuona.

Kweli wananchi wana mifuko iliyotoboka. Hawana ajira, rushwa imeshamiri,haki inanunuliwa, ufisadi, ubadhirifu katika matumizi ya fedha za serikali/umma, mgao wa umeme wa dharura kila mwaka, ukandamizaji wa demokrasia kama kuzuia maandamano na mikutano ya vyama vya upinzani, kuwazuia wananchi wasijadili Muungano na muundo wake, dana dana katika kuandika Katiba mpya na kuundwa kwa tume huru ya Uchaguzi, Mikataba mibovu ya madini, bomoa bomoa makaazi ya wananchi, ukosefu wa tiba katika zahanati na mahospitali ya serikali mpaka watu wamejenga imani na tiba za "mababu", Ubinafsi na umimi badala ya jamii na taifa.na haya "maisha bora kwa kila mtanzania" aka ugumu wa maisha unaoengezeka ukali kila siku.

Muda ukifika mchanganyiko huu utafumuka na athari yake itawashangaza watu katika vipembe vya dunia wanaoiona Tanzania ni kisiwa cha amani.

Tatizo kubwa ni kuwa viongozi wetu, wengi wao ni wachafu, si safi na waliowazunguka pia ni aina hiyo hiyo. Na viongozi hawa wanakosa ujasiri wa kuua nyani. Inabidi wachore mstari mchangani na wawatizame manyani machoni ....kutokana na matukio katika nchi nyingi sasa ni wazi ni suala la muda tu, hayo yanayotokea nchi nyengine yatafika hapa Tanzania.

Viongozi ni wale wenye uoni na ujasiri wa kuchukua hatua mapema na sio kusubiri wakati wa dharuba, dharuba ikifika itawakomba na wao pia hata kama watafanya kama walivyofanya viongozi wa nchi nyengine kutumia polisi na jeshi.

Wakati nakubaliana na wewe kuwa bado watanzania tunakula amani na utulivu lakini si kuwa hatujui nini kinaendelea. Na kama viongozi watauchukulia ukimwa huu wa watanzania kuwa ni dalili ya kuridhika basi wanajidanganya.

Mkuu Nonda " I LOVE YOU MAN"...
 
Mimi sitetei lakini Watanzania wana akili!! Serikali haiwezi kulalamikiwa kwenye swala la mafuta kwasababu hizi bei ni za kimataifa na hata sisi hapa USA bei inapanda!!. Vita vya Libya vinachangia kwa kiasi kikubwa sana na viongozi wa Africa wanatakiwa kumpa offer Ghadaffi aondoke.
 
acha pumba wewe kwahyo unataka kusema nini mbona rwanda'burundi zambia mafuta rahisi na ya pita hapa tz'
 
Mkuu Majani huyu jamaa anayejifanya anatoka USA hana kichwa kizuri... sababu analeta upuuzi watu wanapojadili mambo ya msingi, hizo nchi zisizo na bandari na zinapitishia shehena yao ya mafuta tena kwa magari hapa kwetu wanatoa wapi!!
 
Back
Top Bottom